Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

kama ulokuwepo lahau! ni serikali tatu au tugawane mbao. bravo maalim seif na amani karume. tukishirikiana tutagomboka. long live zanzibar. long live tanganyika. uadilifu muhimu.

ni mzenji halisi.

Hivi kuna watu wanaojulikana kama WAZANZIBARA???

Yaani kama yule rafiki yako, ustadhi Ali, asili ya wazazi Waruguru wa Kianga au Salum Mchole, yaani wazazi asili yao Mafyaaa, Saidi Mnyamwezi, baba asili Tabora, mama Kinyasini-Kaskazini Unguja lakini hawa wote na wengineo mlisoma madrasa ya Kwaalinatu pamoja, na mkachezea African Kid ya katika cenral league pamoja, lakini kila mwisho wa mwaka wakati shule zinafungwa huenda "makwao" kutembea, Mahenge, Mafya Chole-Zamvula, Tabora nk, nk na kwa hakika kabisa wanazijua na kuzithamini koo zoa vizuri kama alivyowaamrisha Mwenyezi Mungu na kama mjuavyo ni kwamba imewaharamikia wao kuzitupa koo zao za damu.

Wao na kwa mujibu wa imani zao, wanaotea na kutamani hasa kama huu muungano haukurekebishwa kuundoa bughudha dhidi ya Zanzibar, basi bora litote tugawane mbao. Zanzibar (Unguja na Pemba) ni zao zimo ndani ya roho zao kama zilivyo damu/koo zao na wanaipenda sana na nchi yao (Tanganyika kwa damu yao, na Zanzibar kwa (kwa damu na makuzi yao) watu wake kwa ujumla, nae ukimuona tabia zao, ukiwasikia lafudhi zao, loh!!! huwatafautishi, kiasi kwamba hata wakati wa safari zao kule "makwao" Mahenge, Cole, Tabora au wengine Kigoma (sikutoa mfano wake hapo juu) watoto wenzi wao kule waliwapachika majina ya "Mpemba" kwa ile lafudhi yao tamu ya kiZenji.

Zikiwa serikali tatu sawa, lakini muungano ukivunjika waende wapi??? au ndio direct "dual citizen"???
 
Wangazija (Comoro) kwa maneno jamani wala hutawaweza..matusi ndio jadi..Acheni hizi jamani Karume atawarudisha makwenu halafu tuone kama kutakuwa na Jeuri hii..
 
Field Marshall ES, are Serious?
Does Karume really has any leadership integrity/status worth comparing with anybody in the URT Government?
....Kuna watu/viongozi (Tanzania) zamani, walikuwa wakiitwa makatibu kata.......
Ta'adabu!
 
.

Mkuu Mkandara, Wanzanzibari waone hivyo hivyo, tena haswa inapotokea ni waarabu wa Pemba. Pamoja na Karume kuwa sio chaguo la Komandoo, ni Chaguo la Bara, kilichotokea anakijua, game lilivyochezwa kumdhibiti Komandoo na chaguo lake, analijua, na kilichomkuta Komandoo na chaguo lake na timu yake nzima sote tunakijua, (complete cut off).

Sasa Karume hataki yamkute yaliyomkuta mtangulizi wake, yeye naye analo chaguo lake, huku kukutana na Maalim ni caveat dhidi ya bara, just incase bara ina chaguo tofauti, then watamback Maalim moja kwa moja to hell with Muungano.

Karume has nothing to loose, siku zake zinahesabika anyway, hivyo kaamua bora Seif kuliko mgombea wa bara. Masharti ya siri baina yao yapo!. Anaeutaka urais wa Znz sio Karume ni Seif, aliyeumia ni Seif, aliyelialia ni Seif leo hawezi kwenda kumlamba miguu Karume for nothing huku watu wake wakiendelea kunyimwa Zan ID na japo walijitokeza kwa wingi day one baada ya mapatano, kesho yake waliendelea kususa kusubiri kauli. Mpaka sasa hakuna kauli yoyote kwa Seif waende, its not for nothing.

Seif naye hii ndiyo karata yake ya mwisho, bado anaamini alikuwa mshindi akipokwa tonge mdomoni, safari hii, alishajipanga sio asipokwe tena, bali kuwahamasisha Wapemba kususia kujiandikisha na kuhakikisha Pemba hakuna kitakachoendelea bora wakose wote at the expense ya damu za Wapemba. Walijipanga kufanya kitu mbaya, Huku kumuangukia Karume sii bure bali ni kuepusha yale yote waliyoyapanga.

Hapa sasa wanaozugwa ni Bara, lets wait for much surprises ahead.
Sometimes u can be good in analysis. Hebu na tuangalie hayo mawazo yako.
 
Mtajirusha wenyewe, roho na akili zenu
Kisemeni msizuwe, kilichomtoa kwenu

Na huku kaja mwenyewe, kajuwa hamna lenu
Ya bure yenu mayowe, huyu sasa siye wenu.
Chorus:Mtajirusha wenyewe roho na akili zenu na msema msizuwe kilicho mtoa kwenu.
Sawaa
 
Bado huna najiuliza kila siku na sipati jibu. tangu itokee maalim seif kumtambua mh karume, Cuf imekua inafanya sherehe mbali mbali kama vile maanadamano na mapongezano huku CCM wao wakikaa kimya bila ya kufanya sherehe? JEE KWANINI CUF WASHERHEKEE ZAID KULIO CCM?

****MBONA simpo tu mkuu!!! wananchi wa kawaida kusherehekea wanafikisha ujumbe kwamba wengi wao hawakuwa pamoja na uamuzi wa uongozi wao wa kutomtambua Karume=== kwahiyo ulikuwa ni uamuzi wa maalimu seif na wenzake wachache!! Pamoja na yote hayo, bado wananchi hao wa kawaida inaelekea wanampenda kiongozi wao, hivyo wasingependa aonekane kwamba ni mkorofi anayesababisha mifarakano Zanzibar!! Wananchi hawa wana kila sabau ya kusherehekea kv wanajua hivi sasa chama na uongozi wao hautaonekana tena kwamba ndio kikwazo cha muafaka!!
*****Uongozi nao hauna budi kusherehekea ingawaje ni wao wenyewe ndio waliamua kutomtambua Karume na ni wao wenyewe walioamua kulamba matapishi yao bila kushurutishwa!!! Lazima wafurahie kwa sababu si kazi ndogo kulamba matapishi, ni kama Mrema anavyoshindwa kulamba matapishi yake kwa kurudi CCM. Wanafurahia kwavile hivi sasa wanaamini lawama ya kikwazo cha muafaka itaonekana ni CCM! Ni kama wamekaanga mbuyu na kuwaachia CCM wazitafune wakati mbuyu zenyewe ni changarawe---zimekolea moto kishenzi.... kwamba, kuna busara yoyote itakayofanywa na CCM kama walivyofanya CUF?!Kwamba, CUF wameshaonesha njia nyeupeeee, ingawaje kwa chini imejaa mbigili, ingawaje hazionekani!!!! Je, CCM watapita kwenye njia hii iliyochongwa na CUF,ambayo kila mpenda amani kaiona, au watachelea mbigili ambazo hazionekani kwa wengine!!! Kwakifupi, hili ni changa la macho kwa CCM kwavile hawana thubutu ambayo hata CUF wenyewe wasingependa kuona CCM inaonesha thubutu hiyo!!! Leo SMZ ikiteu wawakilishi wa CUF kuingia kwenye baraza la mawazir, itakuwa wametegua kitanzi cha CUF na wao CCM kuwa washindi, lakini wasipowateua ( naamini hata CUF wenyewe wanataka wasiteuliwe) washindi watakuwa ni CUF, kwavile CCM wameshindwa kuonesha dhamira ya kweli kama walivyofanya CUf!!! SIASA bana, ni ujasusi mtupu!!
 
Nadhani 2010 Rais wa serikali ya mapinduzi zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi zanzibar si mwingine bali ni Maalim Seif Hamad wa CUF, Kuonana kwao aakuwa alipewa assuarance kuwa mwakani kura Haiziibiwi tena! Which means Seif na CUF tayari wanasherekea kuingia Ikulu.

Mapinduzi Daima!!!
 
Back
Top Bottom