Matokeo ya Kura za Maoni Igunga: CCM - Dr Kafumo, CHADEMA - Mwl Joseph Kashindye

MVUA GAMBA

Senior Member
Apr 13, 2011
102
63
Wana Jf Taarifa zilizonifikia sasahivi Vyama vya CCM na CDM vimemaliza zoezi la Upigaji kura za Maoni ktk jimbo la Igunga.

Matokeo na watu walioshinda kura za Maoni ni Mratibu wa Elimu wilaya ya Igunga Mwl Joseph Kashindye ameongoza ktk kura ndani ya Chadema.

Upande wa Chama cha mapinduzi ameshinda Dk Kafumo ambae ni kamishna wa Madini katika wizara ya Nishati na Madini.

Matarajio ni kuwa CCM watamsimamisha DK kafumo na CDM watamsimamisha Mwlimu Kashindye.

Naomba kuwasilisha.
 
Kwa vyovyote vile LEOPARD MAHONA wa CUF ana nafasi kubwa ya kuibuka kidedea, watu wengi wa vitongoji vya igunga wanamtaja zaidi MAHONA, muhimu MTATIRO na wenzake wajipange.
 
Dr. Kafumu namfahamu vizuri ni mwoga sana hana uwezo wa kujiexpress. Ijapokuwa sijajua uwezo wa mwalimu Kashindye najua atashinda kutokana na sababu zifuatazo;-

i) Dr. ameshindwa kuwasaidia wana Igunga kundoa adha za mgodi wa dhahabu ulipo wilayani hapo.

ii) Makazi yake pamoja na mke wake (mwalimu mama Kafumu) yako DSM, Igunga ni kama wageni waliopo matembezini.

ii) Mwalimu Kashindye ananafasi nzuri ya kushinda sababu amekuwa Igunga kwa muda mrefu ni mzoefu wa eneo husika.

iv) Kazi anayofanya itampa nafasi nzuri hasa kwa walimu akawatetee bungeni.

v) Kikubwa wananchi hawataki kupeleka mtu bungeni kupiga benchi bila hoja akiwa anashangilia mafisadi.
 
Safi sana kwa CHADEMA kwa kumpitisha Mwl Kashindye kwani kama mtu wangu hapo juu alivyoeleza kuwa yeye Mwl Kashindye ana uzoefu na anafahamu Geografia ya pale hasa ukizingatia ni mratibu Elimu wa pale big up sasa iliyobaki ni kujipanga tu hakuna kulala
 
Mamoboi naingana nawe kwa asilimia 100%, hali iliyopo Igunga ukifuatilia kwa umakini utakuta mgombea huyo wa CUF ndo anatajwa zaidi, na tangu jimbo limekuwa wazi yeye na MAHONA na timu za oganaizesheni za CUF wamekuwa ndani ya jimbo. Faida kubwa aliyonayo Mahona ni kuwa;
  1. Amegombea ubunge mwaka 2010 kwa tiketi ya CUF na kupata zaidi ya kura 11,000.
  2. Amefanya kazi na shirika la world vision kwa miaka kadhaa akilizunguka jimbo la Igunga.
  3. Ni mkazi wa Igunga na mzaliwa wa Igunga na anatoka kwenye familia maarufu tarafa ya Nsimbo.
  4. Ni mjenga hoja hodari huku akisimamia ukweli na matatizo ya wananchi.
  5. Ana elimu ya kutosha kuwashawishi wapiga kura - STASHAHADA YA JUU YA BIASHARA NA UTAWALA,
  6. Ni kijana mwenye umri wa miaka 29 tu na kivutio kikubwa cha akina mama.
  7. CUF inaonekana wamejipanga vizuri safari hii kwani Busanda CUF walienda kutalii wakati uchaguzi unaanza lakini kwa Igunga wamefanya Ground work ya kutosha.
  8. CUF wana mtandao mzuri ndani ya Igunga kuliko CDM.
  9. CCM hawana mtandao mzuri kwani RA alijijenga yeye kama yeye.
  10. Kama wananchi wanahitaji kiongozi na maendeleo watamchagua kijana MAHONA na kama wanahitaji SHOW ZA ANGANI watamchagua Mwl Kashinje au Dr wa kuchakachua madini.
  11. Tusubiri tuone wana igunga wanahitaji nini.
 
Kwa vyovyote vile LEOPARD MAHONA wa CUF ana nafasi kubwa ya kuibuka kidedea, watu wengi wa vitongoji vya igunga wanamtaja zaidi MAHONA, muhimu MTATIRO na wenzake wajipange.
<br />
<br />
kujipanga, kujipanga, kujipanga, mkuu fafanua kujipanga ndiyo nini, ni rushwaaa au ni nini hii kitu.
 
Msema kweli mpenz wa mungu,
Mimi sitaki hiki chama cha mashehe na wavaa kanzu na balagashia na mgombea wao MALEOPARD(MACHUI) ashinde, lakini nimesikitika sana leo nikiwa ndani ya Basi nilipopita Igunga mjini.

Kila kona imesheheni bendera za CUF, Benson Kigaila na wenzio ikiwa mnafanya mchezo huko na jimbo likaenda msikitini au mashehe wakawapita mtatafutia pa kujichimbia, hatutaki ujinga kabisa.

Nilikuja kampeni za busanda na mliwazidi CUF kwa kila kitu, kwa nini Igunga mjini yamejaa mabendera ya CUF na za CHADEMA ni za kuokoteza vijiwe viwili vitatu?

Yule Mtatiro bogus anawashinda nini hapo?
My take; KAMA MMESHINDWA KAZI KAMANDA ONDOKENI WAJE MAKAMANDA WENGINE!
Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeees! HATUTAKI JIMBO LIENDE MSIKITINI.
 
Safi sana kwa CHADEMA kwa kumpitisha Mwl Kashindye kwani kama mtu wangu hapo juu alivyoeleza kuwa yeye Mwl Kashindye ana uzoefu na anafahamu Geografia ya pale hasa ukizingatia ni mratibu Elimu wa pale big up sasa iliyobaki ni kujipanga tu hakuna kulala
<br />
<br />
inawezekana pia waalimu wakasimamia kwa ufanisi mkubwa zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura za mwanajamii wao, aidha rushwa inaweza kupata wakati mgumu kidogo kwa baadhi ya watumishi waadilifu.
 
Kutoka IGUNGA kura za maoni za CHADEMA
matokeo ni.

1..Joseph Mwandu
Kashindye kura 63..

2..Isabela
Makeremo kur 52...

3...Juma John
Wambura Chacha kura 43....

pipoz
power
 
ninavyoona CUF na CDM watagawana kura then mgombea wa CCM atapeta kiulaini. Ili upinzani ushinde inabidi CDM na CUF waachiane la sivyo mtakumbuka hii post yangu siku ya matokeo.
 
Faida kubwa alizonazo Mahona ni kuwa;
  1. Amegombea ubunge mwaka 2010 kwa tiketi ya CUF na kupata zaidi ya kura 11,000.
  2. Amefanya kazi na shirika la world vision kwa miaka kadhaa akilizunguka jimbo la Igunga.
  3. Ni mkazi wa Igunga na mzaliwa wa Igunga na anatoka kwenye familia maarufu tarafa ya Nsimbo.
  4. Ni mjenga hoja hodari huku akisimamia ukweli na matatizo ya wananchi.
  5. Ana elimu ya kutosha kuwashawishi wapiga kura - STASHAHADA YA JUU YA BIASHARA NA UTAWALA,
  6. Ni kijana mwenye umri wa miaka 29 tu na kivutio kikubwa cha akina mama.
  7. CUF inaonekana wamejipanga vizuri safari hii kwani Busanda CUF walienda kutalii wakati uchaguzi unaanza lakini kwa Igunga wamefanya Ground work ya kutosha.
  8. CUF wana mtandao mzuri ndani ya Igunga kuliko CDM.
  9. CCM hawana mtandao mzuri kwani RA alijijenga yeye kama yeye.
  10. Kama wananchi wanahitaji kiongozi na maendeleo watamchagua kijana MAHONA na kama wanahitaji SHOW ZA ANGANI watamchagua Mwl Kashinje au Dr wa kuchakachua madini.
  11. Tusubiri tuone wana igunga wanahitaji nini.

Hapo pana utata kidogo, huo mvuto unatokana na nini?! Kwaiyo kua na mvuto kwa kina mama kuwe ndio kigezo cha kua mgombea bora na kiongozi bora tarajiwa?!? Mbona muungwana ana sifa hiyo, je ni kiongozi bora?!

Anyway, hayo ya Igunga wanaigunga ndio waamuzi.
 
Pale igunga kuna jamaa yangu alisema kuwa sasa watu wa igunga hawataki kusikia chama kingine zaidi ya chadema.
 
Msema kweli mpenz wa mungu,
Mimi sitaki hiki chama cha mashehe na wavaa kanzu na balagashia na mgombea wao MALEOPARD(MACHUI) ashinde, lakini nimesikitika sana leo nikiwa ndani ya Basi nilipopita Igunga mjini. Kila kona imesheheni bendera za CUF, Benson Kigaila na wenzio ikiwa mnafanya mchezo huko na jimbo likaenda msikitini au mashehe wakawapita mtatafutia pa kujichimbia, hatutaki ujinga kabisa.

Nilikuja kampeni za busanda na mliwazidi CUF kwa kila kitu, kwa nini Igunga mjini yamejaa mabendera ya CUF na za CHADEMA ni za kuokoteza vijiwe viwili vitatu?
Yule Mtatiro bogus anawashinda nini hapo?
My take; KAMA MMESHINDWA KAZI KAMANDA ONDOKENI WAJE MAKAMANDA WENGINE!
Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeees! HATUTAKI JIMBO LIENDE MSIKITINI.
Acha udini wewe hakuna mwana CDM yeyote anaependa udini kama nyie magamba peleka ugamba wako ccm
 
Back
Top Bottom