Matokeo ya Kidato cha Nne: mimi pia ni Mhanga, naomba mchango wa Mawazo!

Baba JJ

Senior Member
Feb 15, 2013
194
98
Heshima mbele wana JF.

Nina mdogo wangu amemaliza form 4 juzi, lakini ni mmoja kati ya hao 67% waliopata Div 0, yaani ana point 34!!!!. Hii ni hatari sana kwake, hasa kwangu, maana mimi ndio nilikuwa namsomesha kuanzia form 1 na hana mtu mwingine wa kumsaidia. Matokeo ya MOCK alipata Div 2 akanipa matumaini kidogo, lakini haya ya NECTA ni balaa kubwa sana. Napata shida sana kufikiria kesho yake itakuwa vipi, hasa ukizingatia ni zile familia za wakulima haswaa.

Naombeni msaada wa Mawazo nifanye nini kumsaidia kupata kesho yake?

Nawasilisha kwa wana JF wenzangu kwa mawazo na Ushauri.
 
1. anzisha ngo ya kulazimisha waliohusika wote wajiuzuru
2. serikali irudishe waliofeli div 0 na iv miezi minne halafu wafanye mtihani kwa gharama za serikali. waitwe wasahihishaji kutoka nje na mtihani wapewe watu kutoka nje wapewe syllabus watunge kusahisisha
 
Kufeli mtihani mmoja sio mwisho wa maisha. Kama alipata 2 kwenye majaribio, tafuta vijisenti umwendeleze. Tafadhali usikate tamaa na mpe moyo mwisho atashinda.
 
Heshima mbele wana JF.

Nina mdogo wangu amemaliza form 4 juzi, lakini ni mmoja kati ya hao 67% waliopata Div 0, yaani ana point 34!!!!. Hii ni hatari sana kwake, hasa kwangu, maana mimi ndio nilikuwa namsomesha kuanzia form 1 na hana mtu mwingine wa kumsaidia. Matokeo ya MOCK alipata Div 2 akanipa matumaini kidogo, lakini haya ya NECTA ni balaa kubwa sana. Napata shida sana kufikiria kesho yake itakuwa vipi, hasa ukizingatia ni zile familia za wakulima haswaa.

Naombeni msaada wa Mawazo nifanye nini kumsaidia kupata kesho yake?

Nawasilisha kwa wana JF wenzangu kwa mawazo na Ushauri.

Hii nayo ni habari ya siasa?
 
mkuu pole sana mimi niona wawili wote wamepata zero mipango niliyonayo nikuwapeleka kwanza ufundi ili wapate angalau cha kuwasaidia kimaisha na hata kupunguza stress kwao na hata kwangu maana wote nilikuwa nawalipia ada
 
Hii nayo ni habari ya siasa?
Kwani ni kosa kuuliza? the source of this story imetokana na uongozi mmbaya wa CCM na serikali yake kijenga majengo na kuwa dump watoto wa walala hoi bila ya kuwa na walimu. Do you think it is fair?
 
kufeli mtihani huu co kufeli maisha, kama mock alipata division 2 kinachotakiwa ni kumtafutia kituo cha kulist kumbuka hiki ni kilio cha wa2 wengi hata mie ni miongoni mwa hao ingawa binafsi camini kama kweli wanafunzi hawa wamefeli wenyew
 
pole mkuu, nahc mwanao alipopata two huenda alibweteka akapunguza msuli, au inawezekana mitihani haina umakini kwa sababu walimu wanaotunga ni wa shule hizi hizi na kuna usimamizi hafifu kwenye mitihani ya mock, cha msingi kama unaamini ana uwezo darasani arudie mtihani, ila kama uwezo wake ni wa kubabaisha usipoteze rasilimali, anzisha miradi yako ya kilimo morogoro awe anasimamia
 
Mimi pia nimechoma zaidi ya 6m ada tu kusomesha mdogo wangu naye kaambulia zero ni maumivu kabisa na kuchoka,sijui aende wapi na hata VETA kuna kozi nzuri wanataka angalau awe na form four,mambo ya opportunity cost/benefit hayo.
 
Back
Top Bottom