Mateso na kufeli kwako ukiwasimulia Hufurahi mioyoni mwao; Mafanikio yako huwachoma

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
MATESO NA KUFELI KWAKO UKIWASIMULIA HUFURAHI MIOYONI MWAO; MAFANIKIO YAKO HUWACHOMA.

Anaandika, Robert Heriel

Hili wengine tulishalijua zamani za kale, Sisi wengine huwezi kusikia shida zetu, yaani Watu wakituona hutuona kama wala Bata, Maisha Safi, Watu tusio na shida. Muda wote tunafuraha na tunacheka ndio maana hatuzeeki, yaani Watu wa umri wangu wengi wao wanaonekana wazee Kutokana na kutojua Siri hizi. Sio kwamba hatuna shida, nop! Kwani sisi sio Binadamu? Sisi ni binadamu kama walivyo binadamu wengine. Lakini tuligundua kuwa mateso na kuanguka kwetu tunapowasimulia wengine hasa Watu wa karibu, na hapa nazungumzia ndugu, jamaa na marafiki, wengi wao hufurahia MIOYONI MWAO. Ingawaje sio wote lakini wengi wao.

Ni katika unafiki huo ndio tukaona kuwa tupambane na Maisha yetu kivyetuvyetu. Hata hivyo Kwa vile Taikon ninapenda kusoma, na nimesoma nyaraka na maandiko mbalimbali, na kuyatafakari, likiwemo andiko moja la Watu Kale lisemalo, Amelaaniwa amtegemeaye Mwanadamu na kumfanya kinga yake.
Pia yapo maandiko mengi ya Aina hiyo.

Vijana na mabinti, eleweni kuwa, matatizo yako ni yako, Ila Mafanikio yako mara nyingi hutakwa na wote. Bado hujanielewa? Subiri utanipata.

Watu wengi na sio wote, hupenda ukiwaelezea shida zako. Yaani usomi watajifanya wanakuhurumia na kujifanya kama wanataka kukusaidia lakini MIOYONI MWAO hucheka Sana, hufurahi na kushangilia.

Kijana ukiwa jobless alafu ukawa unatangatanga huku na huku, ukiwa unalalamika na kujitafuta, kadiri unavyoteseka na watu wa karibu wanavyokuona au Kupata habari zako, Roho zao hufurahi Mno. Huchekelea.

Taikon kama Watibeli wengine walivyo, tusiopenda mambo ya unafiki na kupindisha pindisha maneno, ninakuhakikishia, hao wanaokuzunguka asilimia 99.999% hujisikia Raha wakiona unateseka. Hiyo 0.001% sio ajabu asiwepo MTU huyo, labda wazazi wako ambao ninauhakika wengine NAO ni wabinafsi;

Ooh Mume wangu hanipendi, sijui ananitesa, sijui anamichepuko mingine, yaani nitamuacha. Nakwambia unapowaambia Watu mambo yako hasa binafsi wanazipenda habari kama hizo, ingawaje watajifanya kukupa pole na vishauri mshenzi kukupumbaza.

Hakuna taarifa Mbaya kwa Watu kama uwaambie Watu Umepata bingo au mchongo wa Pesa. Hakuna taarifa Mbaya kama hizo. Ni Mbaya jamani! Acheni tuu! Yaani ukimwambia MTU Umepata kazi au mchongo Fulani mchunguze usoni hata tabasamu atakaloonyesha kupitia macho yake litakuambia nikisemacho.

Unajua Sisi Watibeli tunamacho ya kuona mpaka ndani, yaani ukimtazama mtu tuu usoni kupitia macho yake, macho Kwa macho husema kweli yote.

Ndio maana Vijana niliwahi waandikia hapa, na sio ushauri wangu pekee Bali hata Watu kale walishasema kuwa usipende kueleza mambo yako Kwa Watu. Kwa sababu haina maana yoyote.

MTU anayeweza kukusaidia hata usipomwambia mambo yako utashangaa amekusaidia tuu.
MTU anayehitaji msaada anajulikana mbona. Hivi unafikiri Watu hawajui kuwa umesoma? Sijui unadegree au diploma Fulani. Hivi unafikiri Watu hawalijui Hilo?
Hivi unafikiri Watu hawajui kuwa huna mtaji, unafikiri hawajui?

Hivi ukisikia msemo usemao, kila MTU atabeba msalaba wake, unafikiri ni masikhara? Au ukiambiwa kila mbuzi ale Kwa urefu WA Kamba yake unafikiri ni mbuzi mee?

MTU pekee wa kuyasaidia Maisha yako ni wewe mwenyewe ndugu yangu.

Na kama unaomba msaada ni vizuri uonyeshe uwezo wako Kwanza na uoneshe nini unaweza kufanya ili unapoomba msaada Watu wenye Roho njema wakusaidie. Na wengi watakaokusaidia ni Watu wa mbali ambao huwajui na hujawahi kuwafikiria.

Unafikiri Yesu MTU m-bad alivyosema; adui WA MTU ni Yule wa nyumbani kwao, au mhenga aliyesema Kikulacho kinguoni Mwako unafikiri walikuwa wamelewa?

Elewa tabasamu na maana zake.
Elewa kilio na huzuni na maana zake.
Sio kila huzuni ni huzuni.
Na sio kila tabasamu ni tabasamu.

Jifunze Lugha za mwili hasa Lugha za macho maana haziongopi.
Mdomo usikudanganye Kwa maana unaweza ongea lolote na unaamrishwa na ubongo. Lakini macho ni lango la Nafsi.

Usipende kutangaza shida zako.
Wala usipende kuelezea mipango na Mafanikio yako.
Acha nipumzike sasa.

Ni Yule Shahidi, Kutoka Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kuna jamaa nikimsimulia "mafanikio" yangu huwa analoa na kupoteza uchangamfu. Jamaa yangu wa karibu alikuwa. Ukitaka kujua kama una rafiki wa kweli msimulie mafanikio yako halafu angalia reaction yake. Akifurahi bila unafiki huyo mwenyewe. Akiloa au akishangilia kinafiki piga chini.
 
Andiko zuri kabisa lenye mafundisho na Mazingatio mengi Sana.. Ahsante.

POINT OF CHALLENGE

Hebu kila mtu ajiulize kichwani mwake kuwa.. " hivi huyu rafiki mnafiki na mtu Mwenye tabia zote zilizozungumzwa kwenye andiko hilo la mtoa mada je huyu mtu
Ni Nani..? Yupo yupoje..? Ni jinsia gani ?. Anaishi sayari gani..? (Anakuja duniani na kuondoka kurudi sayari yake au tupo nao mitaani ??!!)

Kwa sababu me naweza Kuwa mnafiki wa mleta mada.., mleta mada naye anaweza Kuwa mnafiki kwa mtu mwingine huko.. vivo hivyo kwa watu wote wengine.. hatujui kila akuzatazamae anapata taswira gani kwako, huenda anakuona mnafiki au mwema.. hata kama wewe haupo hivo. Hii inabaki juu yake yeye(wewe).

MYTAKE IS:- Kila mtu kwa NAFASI yake ajitahidi kuwekeza sana kwenye " Elimu ya Emotions and psychology" ili aweze kujua na kumudu kuongoza hisia zake, hususa hisia zi sizo Nzuri kama vile Tamaa, Viwu, Chuki nk.. ili kupunguza hayo aliyo ainisha mtoa mada.

Vinginevyo Kila mtu na mtoa mada ukiwemo wote tutakuwa wenye tabia zenye kuendana na mada yako mbele ya macho ya watu wengine wanaotutazama.

Ahsante!
 
Je huyo mtu ni Mimi pia?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom