Mateja ni Noma.....

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
Ni jana majira ya jioni nikikatiza mitaa ya Msasani, nikakutana na mateja wako wachafu wamekaa kijiweni wakipiga soga. Mara akaijitokeza teja mmoja na kuanza kuniita kwa sauti ya mlegezo sauti ya mlegezo..., “Oyaa sister eee..hebu nisubiri basi nikuulize” mie sikumjibu wala kugeuka, niliendelea kuchapa mwendo.



Oyaa sister unajifanya uso wa mbuzi sio, niliendelea kuchapa mwendo bila kugeuka......


Baada ya kuona simjibu wala kugeuka, akaanza kumwaga maneno ya kifedhuli…….

Unajifanya mzuuuri kumbe huna lolote, uzuri wenyewe uko wapi? Sana sana unatumia mgorogo tu, we nini bwana ….. unadhani tuna shobokea mademu sisi,…… shika time yako, huna lolote mshamba tu wewe……

Tena sikiliza…. Ukizeeka na kuwa bibi kizee usije ukaniomba ugoro, maana hamkawii nyie, ukizeeka na kimkongojo chako……(akainama kuonesha mfano wa bibi kizee na mkongojo) lazima utakuja tu …. Kisha akaanza kuigiza sauti ya bibi kizee na kusema, “Mzee naomba kaugoro hapo nitulize kiu yangu”

Sitakupa ng’oooo…….. Ishia huko………

Kwa hisani ya Dada Koero Mkundi...Vukani Blog
 
Unamtumia teja kama kipazasauti kufikisha ujumbe kwa dada fulani, sio!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom