Matamko ya (baadhi) waislam (Dar na Mwanza)

Status
Not open for further replies.
Kama ni maprofesa wa chuo kikuu walioongea hayo mambo, basi ni hatari! Hicho chuo kichunguzwe, la sivyo tataangamia na mabomu ya kujitoa mhanga, siku si nyingi!
 
Nani alikwambia jiwe usafishwa kwa maji likatakata? ukidhani natania chukua maji lita milioni 4 safisha jiwe uone kama litatakata! Ndivyo walivyo wahadhili wa kiislamu awe wa chekechea au chuo kikubwa (sio kikuu) hawasaidiwi kwa elimu ya darasani. Ndio sababu tuna wakina Kikwete kwenye game!

Nafikiri kuna tatizo kwenye ile elimu wanayopata kule MADRASA; ndo inayoleta taabu zote hizi!!!
 
kwanini wamekalia kujenga madrasa nyingi ni kweli wanaongoza kwa kujenga madrasa kuliko huduma za jamii .

harafu kingine kikwete angesomea wapi wakati kasomea shule ya kanisa pale msoga?pia si wameona hospital hazibagui kutibu wagonjwa sasa wanataka wabaguliwe ili walaamike zaidi?huyo ndo proffesor sijui wa nini maana naamini ukisomea chochote ukabobea utakuwa ni mweledi kwa hata urguments zako sasa hao ni kama prof. wa akina maji marefu labda
 
ukiangalia historia ya hawa watu-utagundua kuwa haya malalamiko yao si ya leo.jana au juzi-ni tangu zamani wao wanalalamika tu-lakin cha ajabu-kuanzia muda huo wao wanalalamika kama wangeanza kusoma na kufanya kazi kwa biddi na ushirikiano-wangekuwa na nafuu ya maisha-ila as long wao wanapga kelele tu-watabaki hapo hapo walipo-na as long mashehe hawana elimu dunia-itakuwa ngumu kwa wao kuelewa kwa nini wakristo wanaendelea-ngoja wazid kupeana sumu wakistro wanazid kusonga mbele
 
Kusema kweli pamoja na yote nilitegemea tamko la waislaam angalau lilaani yale mauaji ya Arusha bila kujali nani kafa, nani katoa tamko gani na chama gani wanakipenda. NO. Hawakufanya hivyo kwa maana nyingine mtizamo wao kuhusu vifo vya Arusha ni sawa na Yusuf Makamba! Baada ya kulaani wangeendelea na mambo yao mengine ya kuwashutumu maaskofu wapendavyo ingawa kwa mtizamo wango msimamo wa maaskofu ni sawa kabisa. Maaskofu ni raia kama watu wengine ni wapiga kura. Wao kama wapiga kura wana haki ya kusema uchaguzi na mchakato mzima wa U-meya Arusha ni batili. Kwa nini wasiseme kama wapiga kura?

Pili ili la kumlaumu Pinda na Malecela ni "wivu tu wa kike". Serikali inajua ni nini kilitokea kule Sumbawanga na ndio maana ikatambua makosa na kuomba radhi. Mary Chitanda ni mtoto mtukutu ambaye lazima akaripiwe. Sasa nini kinawakera Maimamu. Kama nao wana manunguniko dhidi ya serikali watoe hoja nzito watasikilizwa sio mihadhara ya matusi na kejeli.

Shule na Hospitali ni pesa zetu wenyewe. By the way waislam ni matajiri sana. Kwa nini hawapendi kushirikiana katika vitu vya maendeleo? Juzi tulishuudia ngumi pale Mwenye kwa kugombania msikiti! Sio hapa Tanzania peke yake na Uganda hivyo hivyo! What do you expect?
 
Kusema kweli pamoja na yote nilitegemea tamko la waislaam angalau lilaani yale mauaji ya Arusha bila kujali nani kafa, nani katoa tamko gani na chama gani wanakipenda. NO. Hawakufanya hivyo kwa maana nyingine mtizamo wao kuhusu vifo vya Arusha ni sawa na Yusuf Makamba! Baada ya kulaani wangeendelea na mambo yao mengine ya kuwashutumu maaskofu wapendavyo ingawa kwa mtizamo wango msimamo wa maaskofu ni sawa kabisa. Maaskofu ni raia kama watu wengine ni wapiga kura. Wao kama wapiga kura wana haki ya kusema uchaguzi na mchakato mzima wa U-meya Arusha ni batili. Kwa nini wasiseme kama wapiga kura?

Pili ili la kumlaumu Pinda na Malecela ni "wivu tu wa kike". Serikali inajua ni nini kilitokea kule Sumbawanga na ndio maana ikatambua makosa na kuomba radhi. Mary Chitanda ni mtoto mtukutu ambaye lazima akaripiwe. Sasa nini kinawakera Maimamu. Kama nao wana manunguniko dhidi ya serikali watoe hoja nzito watasikilizwa sio mihadhara ya matusi na kejeli.

Shule na Hospitali ni pesa zetu wenyewe. By the way waislam ni matajiri sana. Kwa nini hawapendi kushirikiana katika vitu vya maendeleo? Juzi tulishuudia ngumi pale Mwenye kwa kugombania msikiti! Sio hapa Tanzania peke yake na Uganda hivyo hivyo! What do you expect?



walitaka kuhujumu mdahalo wa nkrumah wakaweka mkutano wao diamond jubilee kesho yake habari zao zikaandikwa na magazeti machache kwa ufipi hazikuwa coverage yakutosha hii ilinifurahisha sana kwa sababu watanzania wako tayari kusikia mambo ya maana ya wanazuoni wa kiislamu kama shivji na ulimwengu wanaotumia bongo wao sio hao mashee waliotumwa na RA
 
...wajumbe hao (wakiwemo maprofesa) walitoa shutuma kali kwa viongozi wa kanisa hasa kanisa katoliki wakidai kuwa kanisa ndiyo linaendesha serikali na kwamba serikali inafuata maagizo ya kanisa...


inawezekana ni maprofesa aina ya wale wa maji mafupi.
 
Hii ni aibu sana kwa waislamu wengine wenye ufahamu. Jopo la wale ambao kidogo wangetoa mwanga kwa kuongea vitu vilivyopimwa ndio hao! kama vile hata elimu ya msingi hawakumaliza. Sasa wanaosoma hicho chuo watakuwa na perception gani kwa nchi hii? Elimu hapa imechanganywa vibaya na matokeo yake ndio haya. Tunapoangalia maslahi ya nchi na wananchi wake tusiruhusu fikra na chuki za kidini zitawale mawazo yetu ama sivyo maamuzi ama matamko yanakuwa kama vile yametolewa na watu mbumbumbu kabisa.
 
Shida moja kubwa kwa uislamu ni ulalamishi. Hata ungemfanyia zuri lipi hatakosa kulalamika hadi lengo lake la kukulazimisha wewe kuwa muislamu litimie. Hii ni moja ya nguzo iliyojificha ya uislamu. Muhamad pia alikuwa na tatizo hili ambalo limelithiwa na waislamu wote duniani.
Hivyo basi usiwashangae hawa waislamu wa Tanganyika maana hata ukiwapa mahakama ya kadhi bado watakuja na kilio kile kile "waislamu tunaonewa....bla bla bla bla bla bla......
Malalamishi ya aina hii ndio yalimkimbiza kwao Macca kwenda kuishi Madina.
 
haya ya maprof wa mum ni kipimo sahihi dhidi ya elimu akhera na madhara yake kwa ndugu zetu hawa wazee wa kanzu na barakhashee! ni bomu linalosubiri kulipuka punde wataanza kujitoa muhanga wana eneo gani Tanganyika wanakoweza kudai ni kwao mpaka wajitenge mbumbumbu nyinyi wa fikra na uelewa ulio sahii!
 
Hizo fatwa unazoandika kuhusu Mtume SAW mashiko yake yako wapi? Tuambie na sisi tukasome. Na kama huna mashiko kwa ajili ya ushahidi, na umeyazua tu kwa ajili ya raha ya kukashifu, basi tunanyanyua mikono kumshtakia MMungu atushushie haki juu ya kashfa hii, amiin. Na yeye ndiye mjuzi na muweza.
 
aaah, watu wanalalamika bila sababu badala ya kuangalia suluhisho la matatizo ya wananchi wao wao wanafikiria eti kuimega nchi kwa ajili ya udini. huu ni ujinga na umbumbumbu wa hali ya juu kabisa (PhD in umbumbumbu)india na pakistani ziligawanywa kwa misingi ya udini lakini bado kuna vurugu za kidini. go to hell all those who think they protect God, God is the most powerfull to be protected by ******
 
Ama kweli ukistaajbu ya Musa utaona ya Firauni. Tuzidi kuwaombea maana hawajui walisemalo. Nawashauri wajenge shule, vyuo vingi na hata waboreshe huduma za jamii ili nao waweze kutawala nchi kama walivyodai kuwa wakristo ndo wanatawala nchi. Badala ya kulalamika kila siku, waombe misaada kwenye nchi za OPEC maana wana pesa nyingi za mafuta ili tuweze kuendeleza nchi yetu na huku wao wakitawala nchi badala ya wakristo.

Hata hivyo huu udini utatufikisha wapi? Ukiona dini yoyote inachochea machafuko badala ya kueneza amani iogope kama ukoma.
 
sitegemei kuona mtu bila elimu akaemdelea........waislamu mjitahidi kupeleka watoto shule za wakristu maana hata pale MUM bado mnababaisha hamna waalimu wazuri.
 
Kuhusu wabunge kuwa wengi wakristu. Nashauri vianzishwe viti maalum vya waislam maana wako nyumba sana kama....****ban***.
Kuhusu kugawana nchi nashauri igawanywe fasta halafu sisi wakristu tutajenga ukuta mkubwa kuliko ule waisrael waliowajengea wapalestina. Ukuta huu ni muhimu maana nchi watakayopewa hawa waislam na maprofesor wao hao wa morogoro haitatawalika wala haitakuwa na maendeleo yoyote. Sana sana itakuwa somalia,yemen au hata afghan nyingine. Hivyo nashauri kura ya maoni ipigwe upesi na waislam wepewe maeneo yenye rasilimali nyingi. Baada ya muda utaona ni watu gani watatamani kwenda nchi ya wenzao!
Unajuwa fedha na mali zoootee zilizopo hapa duniani tukigawana sawa kwa sawa kila mtu................Baada ya MUDA MFUPI tu zitarudi kwa wale wale wenye kujuwa jinsi ya kucheza nazo...............

Mtu anapolaumu kuwa wakatoliki wana hospitali nyingi sikuelewi kabisaaaaaaa................... Kama wanaona nguvu inatokana na mali walizonazo nao wawe na zao................... Halafu unalalamika na na ukiumwa unafunga safari kwenda KCMC.........PERAMIHO ......... LITEMBO............etc kutibiwa................ KWELI MWEHU SI LAZIMA AOKOTE NAKOPO.......KAULI ZINATOSHA SANA KUMTOFAUTISHA MWENYE AKILI NA ASIYE NAZO. ........................ CHA AJABU UNAWEZA UKAKUTA KUNA MUISLAMU SASA HIVI ANAUNGA MKONO MATAMSHI HAYO HUKU AKIWA HOI KWENYE HOSPITALI ZINAZOMILIKIWA NA WAKRISTU.

WANALALAMIKIA SHULE WAKATI WENGINE NI MAPROFESA WA CHUO CHA KUPEWA BWERERE NA SERIKALI...........
MNALALAMIKIA SHULE WAKATI MAKAMBA, JK, SALIMU A. SALIMU KASOMA SHULE ZA KIKRISTU NA HAWAKUBAGULIWA..............
 
Yote yatafumka na njama zote ambazo waislamu wanazipanga kwa ajili ya kuliangamiza taifa na nchi ya TZ vitakuwa bayana. Ni wakati wa miungu ya giza kuinua mikono juu na kumtukuza Mungu aliye hai kupitia, Yesu Kristo. Kelele zao ni injili inapita ndani yao. Ipo siku watasimama na kuulizwa mnajidai hamkumfahamu Yesu Kristo, mbona mlipanga na kutimiza vikao na mijadala ya kuwapinga Wakristo??. Sana sana, ninachukua fursa hii niwakaribishe kwa Kristo Yesu, watajua uzuri wake.
 
TAMKO LA WAISLAMU DHIDI YA KAULI ZA MAASKOFU

Utangulizi
Oktoba 31, 2010 Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu ambapo wananchi walipata fursa ya kumchagua Rais, wabunge pamoja na madiwani. Katika uchaguzi huo, Watanzania kwa ujumla wao walikichagua Chama cha Mapinduzi, CCM, kuongoza tena nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Hata hivyo, wakati wananchi wakiamini kwamba wanaongozwa na watu waliowapigia kura, matukio yanayoendelea hivi sasa yanaashiria serikali kutelekeza majukumu yake na kuwaacha maaskofu wakielekeza nchi wanakotaka.

Itakumbukwa kwamba awali kabla ya uchaguzi mkuu maaskofu walikuwa wametoa Ilani yao ya uchaguzi bila kueleza kipi chama chao kitakachosimamia na kutekeleza Ilani hiyo. Baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala, CCM, walishabikia Ilani hiyo na kuwatetea maaskofu. Kwa hakika taarifa za vyombo vya habari zilifahamisha kwamba baadhi ya watendaji waandamizi ndani ya serikali walishiriki katika kuandaa Ilani hiyo.

Ilipofika wakati wa kampeni hadi kuingia siku ya kupiga kura, ilikuwa imedhihiri kipi kilikuwa chama cha maaskofu ambacho walitarajia kitekeleze Ilani yao. Haikuwa tena jambo la siri kwani walisimama wazi wazi kuwaelekeza waumini wao wampigie nani kura. Na katika juhudi zao za kutaka wafuasi wao wawaelewe vizuri, maaskofu walithubutu hata kuweka kando mafundisho ya Biblia yao juu ya masuala ya uzinzi wakawahimiza waumini kumpigia kura mtu wanayemtaka bila kujali kwamba anakabiliwa na kashfa ya kupora mke wa mtu. Waliwaambia wasihangaike na maisha binafsi ya ndoa ya mgombea.

Hata hivyo, matokeo ya kura yalitoa majibu kwamba Watanzania walikuwa wameikataa Ilani ya Maaskofu.

Waislamu tumelazimika kukutana na kutoa tamko hili kwa sababu matukio yanayotokea hivi sasa yanaonesha kuwa wale ambao Watanzania walikataa kuwapa uongozi na Ilani yao iliyoandaliwa na maaskofu, ndio sasa wanaielekeza nchi pa kwenda huku viongozi wa CCM na serikali wakijitahidi kadiri ya uwezo wao kunyenyekea kwa maaskofu hao.

Tumeona na tumemsikia Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda akihangaika kuwapigia magoti na kuwaomba radhi maaskofu kule Sumbawanga. Tumesikia jinsi viongozi wanaojaribu kuwaambia maaskofu kwamba kama wanataka kuingia katika siasa wavue majoho na vyeo vyao vya kikanisa kama Padiri mwenzao waliyekuwa wakimpigania kuingia Ikulu, wanavyokemewa na kutakiwa wawaombe radhi maaskofu hao.

Lililo baya zaidi maaskofu walioshindwa kuwashawishi wananchi waipokee na kukubali Ilani yao, wamekuja na kampeni za kuchochea uasi kwa serikali iliyopo madarakani. Lakini pamoja na hali hiyo, viongozi wa CCM na serikali wamebaki wanagwaya. Hakuna aliyeweza kupata ujasiri wa kukemea hali hii. Kinyume chake Waziri Mkuu na Mzee John Samwel Malecela wanahangaika huku na kule wakiwapigia magoti maaskofu hao na kuwakemea wanaothubutu kuwakosoa.

Hali kama hii ni hatari kwa usalama na utulivu wa nchi. Ni hali ya kuchochea udini na kuweka ombwe la uongozi wa kisiasa ambao utazua balaa. Waislamu hatuwezi kukubali hali hii. Kwa hiyo, ama CCM na serikali vitekeleze wajibu wao wa kuongoza au kama wanaona hawawezi, basi waseme rasmi ili Maaskofu na wengine wenye Ilani zao za uchaguzi waingie tena ulingoni kuomba ridhaa ya Watanzania kuongoza nchi kuliko kuishi katika hiki kiini macho ambapo maaskofu na mawakala wao ndani ya serikali wameachwa waikokote nchi wanakotaka.

Kiini cha Hali hii ya Kisiasa
Hali hii ya kisiasa tunayoishuhudia leo nchini mwetu ni matunda ya mbegu liliyopandwa na kupaliliwa kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Wakoloni walikuwa na kanuni yao waliyoiita divide et impero yaani wagawe ili uwatawale. Huko Rwanda wakoloni waliwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila. Watusi ambao ni watawala wapewe elimu ya juu na wanfundishwe kwa Kifaransa, na Wahutu ambao ni watawaliwa wapewe elimu duni na wafundishwe kwa Kiswahili. Ubaguzi huo wa kuwagawa raia wa nchi moja ulipandikiza sumu iliyokuja kusababisha Wanyarwanda kuuana.

Hapa kwetu wakoloni walitugawa kwa misingi ya dini. Kabla ya uhuru wa Tanganyika, wakoloni kwa kushirikiana na makanisa waliwaona Waislamu kama ni mahasimu wao kidini na kisiasa. Na kwa sababu hiyo serikali za kikoloni zikaweka mikakati maalum ya kuwakandamiza Waislamu katika maeneo matatu: kwanza kuwawekea vikwazo katika kutangaza dini yao ili wasiongezeke; pili kuwabana katika elimu na ili kuhakikisha kuwa Waislamu wanabanwa jukumu la kuwaelimisha Waafrika likawekwa mikononi mwa makanisa na kazi ya serikali ni kuzigharimia tu shule hizo. Lengo likiwa ni kuwabatiza Waislamu wachache watakaoruhusiwa kusoma, na tatu kuwabana katika ajira serikalini kwa sababu makanisa yote yalisisitiza kuwa kuwaajiri Waislamu serikalini ni kusaidia kuenea kwa Uislamu..

Kwa kuwa ubaguzi huo haukuwa na kificho chochote, Waislamu wengi walijitokeza kupambana na ukoloni kwa matarajio kuwa serikali huru itaondosha chuki na uadui huo dhidi ya Waislamu. Lakini msiba mkuu wa taifa hili ni kwamba kinyume chake, baada ya uhuru msimamo ukawa ni ule ule wa kuwaona Waislamu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na mikakati ya kuwabana Waislamu katika maeneo yale matatu ikaimarishwa zaidi wakati wa utawala wa Nyerere. Kuanzia 1957 mkakati uliopangwa na Kanisa Katoliki ukawa ni kuhakikisha kuwa nafasi zote muhimu za uongozi na serikali zinashikwa na wao. [Taz. Confidential Diary – Tanganyika, March-April 1957, uk. 3-4 Maryknoll Central Archives, New York ]. Na ni mkakati huu ndio ambao Mwalimu Nyerere aliokuwa akimuhakikishia Askofu Rweyemamu mwaka 1970 kuwa anatumia mamlaka yake kama Rais na kama kiongozi wa TANU kuhakikisha kuwa anatoa upendeleo maalum kwa Wakristo ili wasimamie sera za Chama. Na kwamba amemteua padiri katika nafasi nyeti ya Chama si kwa sababu anajua siasa bali kwa sababu ni Mkristo safi. Lakini Nyerere huyo huyo akisimama hadharani alijidai kukemea udini. Na kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuliimarisha kanisa na kuwadhoofisha Waislamu, leo Kanisa lake limo katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa ni Mtakatifu!

Sivalon anaarifu katika kitabu chake kuwa mara baada ya uhuru Kanisa katoliki liliwahamasisha Wakristo wote na hasa watendaji wa serikali juu ya hatari ya Ukomunisti na Uislamu na walikusanya nguvu zao zote katika kukabiliana na maadui hao.

Matokeo ya Hujuma Hizo
Matokeo ya hujuma hizo za kichinichini ni kwamba katika sura ya nje na katika propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na kisiwa cha amani. Lakini uhalisia wa mambo ni kuwa Tanzania ni nchi yenye jamii kubwa mbili. Jamii ya Wakristo wanaopewa msaada, upendeleo, ulinzi na heshima, na jamii ya Waislamu ambao wanachukiwa, kudharauliwa na kudhoofishwa na serikali kabla na baada ya Uhuru. Ifuatayo ni mifano michache tu ya baadhi ya hujuma hizo baada ya Uhuru.

(1) Mwaka 1963 katika Barua ya Kichungaji, Kanisa Katoliki lilisema Waislamu walikuwa wanajenga umoja na mshikamano miongoni mwao, jambo ambalo ni "hatari kubwa kwa hatima ya Wakristo wetu" na Sivalon anabainisha kuwa Wakristo walimwomba Nyerere awasaidie kuvuruga umoja huo wa Waislamu. Ndio sababu ya Nyerere kutumia dola kuiparaganya EAMWS. Kwa kuwa Waislamu ni jamii inayotakiwa kuwa dhalili, hawatakiwi kuwa na umoja. Ndio maana tangu wakati wa Nyerere hadi leo, uchaguzi wa viongozi wa Waislamu husimamiwa na vyombo vya dola. Nia ikiwa ni kutokuwapa Waislamu uhuru wa kuwachagua viongozi wao. Katika taifa moja haki hiyo ni ya Wakristo peke yao. Sote ni mashahidi kuwa mwaka 1994 serikali ilimwagiza Naibu Waziri Mkuu Mh. Augustino L. Mrema kuhakikisha kuwa Bakwata inapitisha katiba mpya inayotakiwa na serikali. Na Maaskofu wakachangia gharama. Waislamu ni maadui kidini na kisiasa, lazima wadhibitiwe.

(2) Mwaka 1992 Serikali ya Tanzania ilitiliana saini Makubaliano ya Itifaki rasmi na Makanisa ya TEC na CCT. Kwa mujibu wa makubaliano hayo ambayo yalitiwa saini na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye wakati huo alikuwa Mh. Edward Lowasa serikali imewajibishwa pamoja na mambo mengine, kutenga nafasi za masomo kwenye vyuo vyake vya Ualimu mahsusi kwa ajili ya wanafunzi wanaopangwa kufundisha katika shule za Kanisa; pia kutoa ruzuku ya kuendeshea taasisi za Makanisa. Kuanzia 1992 hadi leo serikali imetoa mabilioni ya kodi za wananchi kwa Makanisa. Katika kipindi chote hicho Waislamu wamepinga ubaguzi huo. Lakini kwa kuwa lengo ni kuwaimarisha Wakristo ambao ni jamii inayotakiwa kupewa nguvu zaidi dhidi ya jamii ya Waislamu ambao wanatizamwa kama maadui, serikali imeyapuuza malalamiko ya Waislamu. Lakini propaganda zinaendelea kuwa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na ni kisiwa cha amani.

(3) Waislamu wameiomba serikali kujiunga na OIC kama njia mojawapo itakayowezesha nchi yetu kupata misaada itakayotumika kuinua hali za Waislamu ambao wameachwa nyuma sana katika elimu na uchumi. Makanisa yote kwa kauli moja yamepinga kwa nguvu zao zote pendekezo hilo. Sababu ya kupinga kwao ni kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanadhoofishwa katika kila hali, na ni makosa makubwa kuwaimarisha kiuchumi au kielimu maadui hao. Serikali ilipofanya utafiti wake wa kina ikajiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa na hakuna madhara yoyote. Na Mh. Bernard Membe alitamka hilo Bungeni. Mara akaitwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Cardinali Pengo na kukumbushwa mkakati wa kuwadhoofisha Waislamu. Msimamo wa serikali ukabadilika. Lakini propaganda za kuwazuga Waislamu zinasema Watanzania wote ni kitu kimoja na nchi hii haina ubaguzi!

(4) Kwa kuwa tangu wakati wa ukoloni hadi leo mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanaminywa kadiri iwezekanavyo katika nafasi za uongozi na ajira, ndio maana hadi leo, miaka 50 baada ya Uhuru Waislamu ni wachache sana katika nafasi zote za uongozi na ajira katika sehemu muhimu serikalini na katika vyombo muhimu vya maamuzi. Kisingizio kinachotolewa ni kuwa Waislamu hawataki kusoma. Lakini ukitazama orodha ya Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa na sifa zao, utaona dhahiri kuwa wapo Waislamu wengi wenye sifa bora zaidi ambao wangestahili kuwa ma-DC. Waislamu hawateliwi kwa sababu mkakati uliopo ni kuwatenga Waislamu na ikiwezekana kuwaondosha kabisa katika sehemu muhimu za uongozi, kwa sababu kama wao hawajui ukweli ni kwamba hawatakiwi kushika nafasi zozote muhimu za uongozi au ajira. Ndio maana asilimia 75 ya Ma-DC wote ni Wakristo na karibu wasimamizi wote wa Uchaguzi katika wilaya ni Wakristo. Wabunge asilimia 75 pia ni Wakristo, na hali ni hiyo hiyo katika Vitengo vya serikali na Mashirika ya uma. Ndio maana hakuonekani tatizo lolote pale taasisi yote inapokuwa na Wakristo watupu. Na kelele nyingi maadui wa serikali na Kanisa wanapopewa nafasi hata kama wana uwezo kiasi gani. Katika sura ya nje Tanzania ni taifa moja, katika uhalisia wake ni kuna mataifa mawili, moja nyonge na jingine lenye nguvu.

(5) Kwa kuwa Waislamu wanahesabiwa kuwa ni maadui, ule mkakati uliowekwa na wakoloni wa kuwawekea vikwazo Waislamu katika kutangaza dini yao unaendelea hadi leo. Ipo mifano mingi sana ya Waislamu kukamatwa, kutiwa ndani na kunyanyaswa na vyombo vya dola kwa sababu tu ya kulingania hadharani dini yao. Kwa kuwa Waislamu ni maadui, basi ni muhimu kuhakikisha kuwa hawaongezeki. Wakristo wanayo haki ya kuitisha mkutano wa hadhara na kutangaza kuwa Yesu ni Mungu. Wao ni jamii inayostahiki ulinzi wa dola. Lakini pindi Mwislamu atakaposema hadharani kuwa Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi siyo Yesu mwana wa Mariamu atakuwa amekashifu dini ya dola na atakamatwa na kubughudhiwa. Lakini kipropaganda, Tanzania ni nchi moja na inafuata katiba moja. Lakini uhalisia ni tofauti.

(6) Msimamo wa serikali na makanisa kuhusiana na mauaji ya Waislamu katika msikiti wa Mwembechai ni kielelezo kingine cha ukweli kuwa Tanzania ni mkusanyiko wa jamii mbili zenye haki na hadhi tofauti katika taifa moja. Kwa kushinikizwa na Maaskofu serikali iliwauwa Waislamu watatu Mwembechai pasi na hatia yoyote. Waislamu waliiomba Mahaka, Bunge na hata Rais aunde Tume ya uchunguzi. Mihimili yote ya dola ilikataa. Kiongozi wa Kanisa Katoliki akenda mbali zaidi. Akahalalisha mauaji hayo. Kwa sababu waliouliwa ni wale maadui wa ile jamii nyoge isiyotakiwa kustawi. Lakini alipouliwa mbwa "Imigresheni" mwaka huo huo wa 1998, Jaji Mkuu wa wakati huo Mh. Francis Nyalali aliamuru uchunguzi wa kuuliwa mbwa huyo na hakimu akaadhibiwa. Jaji Mkuu alichukua uamuzi huo bila kuombwa na mtu. Lakini wale waliowauwa Waislamu walipongezwa na kupandishwa vyeo. Uhasama wa serikali na makanisa dhidi ya jamii ya Waislamu ni wa kiwango cha kutisha. Msimamo ukawa huo huo walipouliwa Waislamu Unguja na Pemba 2001 kwa kuandamana kudai Katiba Mpya. Lakini kipropaganda tunaambiwa Watanzania wote wanahaki sawa.

(7) Rais wa Marekani George W. Bush alipotangaza Vita vya Msalaba dhidi ya Waislamu mwaka 2001, serikali ya Tanzania ikapata uhalali zaidi wa kuzidi kuwakandamiza Waislamu. Serikali ikawa radhi kuvunja Katiba ya nchi kwa kupitisha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya 2002 ili zipatikane fursa zaidi za kuwanyoongesha Waislamu. Waislamu waliipinga sheria hiyo kwa nguvu zao zote, lakini kwa kuwa wao ni jamii inayotakiwa kupigwa vita hawakusikilizwa. Bunge ambalo nalo lina Wakristo wengi likaipitisha haraka sheria hiyo. Naam, tangu imepitishwa hadi leo, sheria hiyo imetumika kuwadhuru Waislamu wasiokuwa na hatia yoyote, na kufunga taasisi zilizokuwa zikiwasaidia Waislamu. Misaada ni haki ya Wakristo, siyo Waislamu. Pamoja na madhila yote hayo Waislamu wanatakiwa waendelee kuamini kuwa Tanzania ni nchi moja inayojali raia wake wote.

(8) Wakati serikali ikidai kuwa Tanzania ni taifa ambalo raia wote wana haki sawa, lakini serikali hiyo hiyo kwa makusudi kabisa inafanya jitihada za waziwazi za kuwahamasisha Wakristo wawaone Watanzania ambao ni Waislamu kuwa ni maadui zao na maadui wa taifa lao. Januari 2001 Waziri Mkuu Mh. Frederick Sumaye alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa serikali inazo taarifa kuwa kundi la magaidi waliopata mafunzo nchi za nje limerejea nchini na magaidi hao wanapanga kuilipua hospitali ya Muhimbili. Kufuatia kauli hiyo Waislamu watatu wa Muhimbili ambao ni Waislamu akiwemo Profesa wa Micro-Biology walitiwa mbaroni. Japo baadaye waliachiwa kwani hawakuwa na hatia yoyote, lengo la serikali la kupandikiza sumu ya chuki lilikuwa limetimia. Tarehe 24 Agosti 2001 Waislamu walifanya maandamano kupinga kufungwa kwa Dibagula kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali kupitia jeshi la polisi likawatangazia wananchi wote kuwa Waislamu wamepanga kuyalipua makanisa siku ya Jumapili ya tarehe 2 Septemba 2001. Na serikali ikawahakikishia Wakristo kuwa itaweka maaskari wa kuwalinda na hiyo shari ya Waislamu. Lengo la uzushi huu ni kuwachochea Wakristo wawachukie Waislamu na hivyo waunge mkono hatua za serikali za kuwapa kipondo. Hivi sasa huo umekuwa ni mchezo wa kawaida. Kila baada ya muda Fulani serikali kwa kpitia jeshi la polisi hutoa taarifa za kuonesha kuwa kuna mpango wa shambulio la kigaidi. Na watuhumiwa siku zote ni Waislamu. Serikali na makanisa yanawachukia Waislamu kiasi cha kuwa tayari kushirikiana na wasiokuwa Watanzania katika kuwahujumu Waislamu. Ni dhahiri kuwa katika mazingira kama haya, Maaskofu wakipata kisingizio chochote watakuwa tayari kuwauwa Waislamu kama walivyoshiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda.

(9) Papa John Paul II alipoitembelea Tanzania mwaka 1990, Kanisa Katoliki lilimkabidhi Ripoti yenye anwani: Activities of the Church in Tanzania. Katika ripoti yake hiyo Kanisa Katoliki limetaja kuwapo kwa Tume ya Majeshi ya Kivita [Commission of Armed Forces] ndani ya Kanisa hilo. Tangu wakati huo hadi leo Waislamu wameitaka serikali iwaondoshe hofu kwa kuweka wazi kazi za Tume hiyo ya Majeshi ya Kivita ndani ya Kanisa. Serikali haijajibu na wala haijajishughulisha na taarifa nzito kama hizo. Hatujui kama Tume hiyo ya Majeshi ya kivita inafanya kazi ndani ya Jeshi la Wananchi au nje ya jeshi hilo. Lakini kwa muktadha wa hali ya uhasama wa serikali na hasa wa Maaskofu dhidi ya Waislamu wanaowahesabu kuwa ni maadui zao, si vigumu kukisia kwa nini Kanisa Katoliki limeunda Tume ya Majeshi ya Kivita. Lakini serikali ambayo haishughulishwi kabisa na Tume ya Majeshi ya Kivita ya Wakatoliki imekuwa na tabia ya kuwakamata na kuwatia ndani Waislamu kwa kesi za kuwabambikia zisizokuwa na kichwa wala miguu. Lakini propaganda zinasema Tanzania ni nchi moja yenye katiba inayolinda haki za watu wote. Mwenye mach haambiwi tazama.

Dalili ya Mvua ni Mawingu
Alipokuwa akitoa mada yake juu ya "Mifumo ya Viashiria vya Migogoro" katika Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ulioandaliwa na REDET mwaka 2003, Mh. Bernard L. Membe alisema kwamba migogoro mingi duniani na hasa vita vya wenyewe kwa wenyewe vina dalili na viashiria vyake. Akasema miongoni mwa dalili kubwa kuwa nchi karibu itaingia katika machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kutokea kwa mgawanyiko au kutokea kutoelewana kwa viongozi ndani ya chama au serikali tawala.

Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo mawaziri wakipingana hadharani juu ya maamuzi waliyoyafanya wenyewe. Lakini pia katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia pia mgongano wa waziwazi kati ya wabunge wa CCM na Chama chao. Na wote hao hawachoki kujisifu kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere. Lakini mwaka 1993, Nyerere katika Kitabu chake Tanzania! Tanzania! Aliandika na tunanukuu:

Ziko jitihada sasa hivi za kugombanisha Wabunge na chama chao kwa kutumia hoja ya hadhi ya Bunge. Ni nani huyu anayefanya kazi hii? Ni haki kabisa ya vyama vya upinzani kujaribu kugombanisha Wabunge wa chama kinachotawala na chama chao. Lakini viongozi wa chama kinachotawala pamoja na Serikali yenyewe wanapojaribu kufanya mambo ambayo yatagombanisha Wabunge wa CCM na chama chao, tuna haki ya kuwauliza viongozi hao wanafanya kazi hii kwa niaba ya nani, na chama chao ni chama gani? [uk. 41]
Pamoja na kuyajua yote hayo hivi sasa kuna msuguano ulio dhahiri kabisa baina ya Wabunge wa CCM na Chama chao. Kiashiria kingine alichokitaja Mh. Membe ni kwa serikali kushindwa kuyashughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi yanayoelekezwa serikalini.

Maazimio ya Waislamu
Kwa kuzingatia muktadha wa hali ya kisiasa ilipofikia hivi sasa, Waislamu tumefikia maamuzi yafuatayo:

(1) Maadam Mfumo Kristo umeimarika kiasi cha kuweza kuitisha serikali na viongozi wake na wakatishika, na maadam Mfumo huo Kristo una nguvu za kuweza hata kuvitisha na kuvikemea vyombo vya dola na vikasalimu amri, Waislamu tutake tusitake, kama alivyohadharisha Mh. Membe, ukweli unabaki kuwa hautapita muda mrefu, dhulma hii ya udini italisambaratisha Taifa letu, kama udini ulivyoisambaratisha Ivory Coast ambayo katika miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa mfano wa kuigwa.

Hivyo basi wajibu wetu wa mwanzo ni kuufikisha ujumbe huu kwa Waislamu wote nchini, na kuwataka wazingatie kuwa kwa kuwa wanabaguliwa na kudhalilishwa katika nchi hii kwa sababu ya Uislamu wao, basi ni wajibu wao na wao kushikamana kama Waislamu.

(2) Kwa kuwa kila wanchosema Maaskofu ndicho kinachofuatwa na serikali, na kwa kuwa Maaskofu wamekwishatamka hadharani na kwa sauti kali kuwa katika nchi yetu hakuna kabisa udini na atakayesema kuna udini basi ni yeye ndiye anayetaka kuleta udini, na kauli hiyo kudakwa na mawakala wa Maaskofu katika serikali, ni dhahiri kuwa dhulma za udini zinazoendelea kuwakandamiza Waislamu miaka 50 baada ya Uhuru hazitaondoshwa na Katiba mpya. Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa fidia.

(3) Kwa kuwa tangu ukoloni hadi leo Waislamu wanahesabiwa na serikali na Maaskofu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na wasiostahiki haki sawa na wengine, na kwa kuwa Waislamu wameazimia kutokukubali tena kudhulumiwa na kuonewa kwa namna yoyote ile iwayo, ni wazi kuwa hakuwezi kuwa na katiba itakayoweza kulinda haki za madhalimu na wadhulumiwa kwa wakati mmoja. Ingawa kwa propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja, lakini kiuhalisia ni nchi yenye jamii mbili zenye hadhi na haki tofauti kabisa. Umefika sasa wakati wa kugawana nchi ili Waislamu wanaochukiwa na kunyimwa fursa sawa na Wakristo waishi katika maeneo yenye Waislamu wengi na Wakristo waishi katika maeneo yenye Wakristo wengi. Mwalimu Nyerere alipigania kwa nguvu zake zote Nigeria igawanywe ili Wakatoliki ambao walikuwa wanadhulumiwa Nigeria wajitenge na waruhusiwe kuishi katika nchi ya Biafra. Na katika kijitabu alichokiandika 1966 Nyerere alisema madai ya kuhifadhi umoja wa kitaifa wa Nigeria hayana maana yoyote pale ambapo baadhi ya raia wa taifa hilo wanadhulumiwa. Ushahidi wa dhulma za Waislamu upo wazi. Kugawana nchi kutawawezesha Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC bila ya kuwakera Maaskofu. Ni wajibu wetu kulifikisha hili kwa Waislamu wenzetu nchi nzima ili lijadiliwe zaidi kabla halijafikishwa rasmi

(4) Kwa kuwa hakuwezi kuwa na amani ya kweli bila ya haki, na kwa kuwa amani ya Tanzania inashikiliwa na Waislamu walioruhusu dhulma hiyo, Waislamu tunayo dhima kubwa kwa kustawi kwa Mfumo Kristo ambao sasa hapana shaka yoyote unalisambaratisha Taifa. Lakini kama alivyosema Nyerere, anayedhulumiwa ni mtu anayeteseka. Asipopambana na huyo dhalimu, yeye ataendelea kuteseka wakati dhalimu anastarehe kwa amani. Akiamua kupambana, wote yeye na dhalimu watateseka. Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.


WABILLAHI TAWFIQ
 
Safi sana Waislam ila tatizo tamko lenu halina solution ya matatizo inaonekana mlitaka kututisha tu. Nashauri mje na tamko linalosema kwa mfano nchi igawanywe kutoka sehemu fulani hadi sehemu fulani. Kwa tamko mlilotoa inaonekani ni daganya toto tu! Na kama hili ndilo tamko lililotolewa na Wanazuoni wa Kiislam basi mnayo khasara kubwa kwani lime-expose udhaifu wenu kwa kiwango cha juu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom