Maswali muhimu: Kwa mfumo na hali iliyopo, Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi itakuwaje? Itapatikanaje?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Nazisoma,sehemu mbalimbali,hoja za kutaka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi. Wajengahoja wanadai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ya sasa si huru kutokana na muundo wake;mtindo wake na utendaji kazi wake. Kubwa ni kuwafanya Wakurugenzi na wateule wengine wa Rais au Waziri kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.

Sina haja ya kubishia ukweli kuwa Tume huru ya Uchaguzi ni muhimu. Tume huru hulinda demokrasia kwa kuwafanikishia wapigakura kuwachagua viongozi wawatakao. Tume huru inalinda thamani ya kura na mchakato mzima wa kiuchaguzi. Kwahiyo,naunga mkono uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi.

Kwa mfumo na hali ya kisiasa iliyopo hapa nchini mwetu Tanzania,Tume hii itapatikanaje? Wajumbe na wafanyakazi wake wapatikanaje? Utendaji wake uwaje? Iwe na Wajumbe na wafanyakazi wangapi?

Waione: Pascal Mayalla, Chakaza, Retired MsemajiUkweli, Daudi Mchambuzi,Nyani Ngabu,Salary Slip na wengineo
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi apatikane kutoka Bungeni,Bunge lipige kura kumtafuta nani awe mwenyekiti wa Tume,Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atachagua wakurugenzi wake

Wakati wa uchaguzi mawakala wote wanaoviwakilisha vyama vya siasa vilivyojiandikisha kupiga kura lazima waweko vituoni,Ikiwa kama itatokea mawakala wanaowakilisha chama fulani wamekosekana katika kituo husika basi kituo kituo hicho kisitumike kupiga kura...

Kama itakuwa hivyo kuna uwezekano mkubwa haki itapatikana kwa vyama vyote,Bunge ndio serikali,Bunge linawakilisha vyama vyote vya siasa,Raisi ni taasisi ya chama fulani cha siasa,kama Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atachaguliwa na Raisi basi kuna umwezekano mkubwa kupendele upande wa Raisi...

Nawakilisha
 
Bunge wampigie kura mwenyekiti kutoka majina gani? Lazima kutakuwa na mamlaka nje ya Bunge wenye mamlaka ya kupendekeza na kuteua.

Pili unavyokataa wakurugenzi wa halmashauri wasishiriki, unataka kuajiri watu wawe wanakula pesa ya bure, kazi yao ni uchaguzi tu ?
 
Nazisoma,sehemu mbalimbali,hoja za kutaka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi. Wajengahoja wanadai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ya sasa si huru kutokana na muundo wake;mtindo wake na utendaji kazi wake. Kubwa ni kuwafanya Wakurugenzi na wateule wengine wa Rais au Waziri kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.

Sina haja ya kubishia ukweli kuwa Tume huru ya Uchaguzi ni muhimu. Tume huru hulinda demokrasia kwa kuwafanikishia wapigakura kuwachagua viongozi wawatakao. Tume huru inalinda thamani ya kura na mchakato mzima wa kiuchaguzi. Kwahiyo,naunga mkono uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi.

Kwa mfumo na hali ya kisiasa iliyopo hapa nchini mwetu Tanzania,Tume hii itapatikanaje? Wajumbe na wafanyakazi wake wapatikanaje? Utendaji wake uwaje? Iwe na Wajumbe na wafanyakazi wangapi?

Waione: Pascal Mayalla, Chakaza, @jokakuu,Retired MsemajiUkweli, @nguruvi3,Daudi Mchambuzi,Nyani Ngabu,Salary Slip na wengineo
Navipi tulio apa kuilinda kwa kufa na kupona katiba iliyopo? kubadili katiba si kuninyang'anya tonge nawakati bado nalihitaji?
 
Nazisoma,sehemu mbalimbali,hoja za kutaka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi. Wajengahoja wanadai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ya sasa si huru kutokana na muundo wake;mtindo wake na utendaji kazi wake. Kubwa ni kuwafanya Wakurugenzi na wateule wengine wa Rais au Waziri kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.

Sina haja ya kubishia ukweli kuwa Tume huru ya Uchaguzi ni muhimu. Tume huru hulinda demokrasia kwa kuwafanikishia wapigakura kuwachagua viongozi wawatakao. Tume huru inalinda thamani ya kura na mchakato mzima wa kiuchaguzi. Kwahiyo,naunga mkono uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi.

Kwa mfumo na hali ya kisiasa iliyopo hapa nchini mwetu Tanzania,Tume hii itapatikanaje? Wajumbe na wafanyakazi wake wapatikanaje? Utendaji wake uwaje? Iwe na Wajumbe na wafanyakazi wangapi?

Waione: Pascal Mayalla, Chakaza, @jokakuu,Retired MsemajiUkweli, @nguruvi3,Daudi Mchambuzi,Nyani Ngabu,Salary Slip na wengineo
Ukweli mtupu.
Tunapiga kelele ila hatutoi mapendekezo itapatikana vipi maana kwa jinsi hali ilivyo ni kwamba itaitwa huru kujifirahisha ila haitakuwa huru.
 
Mbona wapo wabobezi waliobobea katika masuala ya katiba na muundo wa hizo Tume za uchaguzi.kikubwa kinachotakiwa ni upatikanaji wa Tume itakayokuwa huru na si kuongizwa na ushawishi wa chama tawala.
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi apatikane kutoka Bungeni,Bunge lipige kura kumtafuta nani awe mwenyekiti wa Tume,Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atachagua wakurugenzi wake

Wakati wa uchaguzi mawakala wote wanaoviwakilisha vyama vya siasa vilivyojiandikisha kupiga kura lazima waweko vituoni,Ikiwa kama itatokea mawakala wanaowakilisha chama fulani wamekosekana katika kituo husika basi kituo kituo hicho kisitumike kupiga kura...

Kama itakuwa hivyo kuna uwezekano mkubwa haki itapatikana kwa vyama vyote,Bunge ndio serikali,Bunge linawakilisha vyama vyote vya siasa,Raisi ni taasisi ya chama fulani cha siasa,kama Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atachaguliwa na Raisi basi kuna umwezekano mkubwa kupendele upande wa Raisi...

Nawakilisha
Umekosea sana kusema Mwenyekiti wa Tume akapigiwe kura na Bunge wakati unajua kabisa wabunge wengi ni wa chama gani......kama ni kwenda kupigiwa kura bungeni labda vyama viteuae idadi ya wabunge sawa kwa maana kuwa upinzani wawe na wabunge 20 na chama tawala wawe na wabunge 20 harafu wanaopigiwa kura wasiwe na historia ya kujihusisha na vyama vya siasa
 
Bunge wampigie kura mwenyekiti kutoka majina gani? Lazima kutakuwa na mamlaka nje ya Bunge wenye mamlaka ya kupendekeza na kuteua.

Pili unavyokataa wakurugenzi wa halmashauri wasishiriki, unataka kuajiri watu wawe wanakula pesa ya bure, kazi yao ni uchaguzi tu ?
Hakuna nchi ambayo ina tume huru ya uchaguzi halafu watendaji/wafanyakazi wake ni makada wa chama cha siasa, tena chama chenyewe ni chama tawala tu.

Tukiwa na Tume Huru ya Uchaguzi, Tume itakuwa na waajiriwa wake wa kudumu na wa muda mfupi, ndivyo nchi nyingi zinavyofanya.

Sioni kama kutakuwa na upotevu wa pesa kama wafanyakazi wa tume wa kudumu watakuwepo kuanzia ngazi ya Wilaya.

Kwa sasa tuna watu wengi ambao wanalipwa pesa nyingi kuliko watakayolipwa wafanyakazi wa NEC. Tuna watu kama Wakuu wa Wilaya ambao kwa sasa kazi yao kubwa ni kuvuruga uchaguzi na kuwafunga watu masaa 48, hawa nafasi zao zinaweza kufutwa. Maslahi ya Mkuu wa Wilaya yanaweza kuwa ni sawa na ya watumishi wa tume ya uchaguzi watano.
 
Tume kuwa na waajiriwa wa kudumu ngazi ya wilaya ni upotevu wa pesa. Yaani upo tayari kumlipa mtu mshahara wa bure ila haupo tayari kurudia uchaguzi, huu ni unafiki.

Pili, vipi kuhusu mwenyekiti?
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi apatikane kutoka Bungeni,Bunge lipige kura kumtafuta nani awe mwenyekiti wa Tume,Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atachagua wakurugenzi wake

Wakati wa uchaguzi mawakala wote wanaoviwakilisha vyama vya siasa vilivyojiandikisha kupiga kura lazima waweko vituoni,Ikiwa kama itatokea mawakala wanaowakilisha chama fulani wamekosekana katika kituo husika basi kituo kituo hicho kisitumike kupiga kura...

Kama itakuwa hivyo kuna uwezekano mkubwa haki itapatikana kwa vyama vyote,Bunge ndio serikali,Bunge linawakilisha vyama vyote vya siasa,Raisi ni taasisi ya chama fulani cha siasa,kama Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atachaguliwa na Raisi basi kuna umwezekano mkubwa kupendele upande wa Raisi...

Nawakilisha
Mwenyekiti ateuliwe na bunge kwa kura zilizozidi theluthi moja ya wabunge wote (kuna ambao watakuwa na khofu na idadi ya chama tawala lakini tukiweka misingi mizuri ya demokrasia hilo sio tatizo).

RAS na DED wasiwe wasimamizi wa uchaguzi.

Wafanyakazi wowote wale wa tume wasiwe wamewahi kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa kabla na baada ya kushika madaraka kwenye tume ya uchaguzi.

Sheria iruhusu uchaguzi wa Rais kupingwa Mahakamani.

Wakati wa uhesabuji kura wagombea waruhusiwe kuchukua tukio zima kwenye picha za mwendo
 
Judge mkuu aunde tume ya judges. Top officials wachaguliwe na wawe responsible kwenye tume ya Judges. Wawee confirmed na bunge. Wafanyakazi wengine waajiriwe kawaida kwa mfumo wa serikali
 
Mkuu, niliwahi kujiuliza sana kuhusu kupatikana kwa Tume Huru na mpaka leo sijapata jibu:

Kamati hii ya Uteuzi inaweza kweli kutupatia Tume Huru ya Uchaguzi? - JamiiForums
Mimi naona kabila ya kwenda kwenye kutengeneza tume huru... Tuanze kwanza na kutatua changamoto ndogo ndogo za chaguzi zinazosimamiwa na hii tume ya sasa..Tukianza mchakato wa tume huru ya uchaguzi hautaisha Leo na muda umeshatutupa mkono Kumbukeni mwakani tunauchaguzi wa serikali za mitaa .Changamoto kubwa ninayoiona mimi na ambayo ingeweza kurekebishwa kwa haraka kabila ya uchaguzi wa mwakani wa serikali za mitaa...ni kuwaondoa wakurugenzi wa wilaya,manispaa na majiji... wasiwe wasimamizi wakuu wa uchaguzi katika maeneo yao..Wakurugenzi wa majiji,manispaa,wilaya..wanafanya wanayofanya kwa hofu ya kuenguliwa kwenye nafasi zao... Tume ya uchaguzi iwe na mamlaka ya kusimamia uchaguzi mpaka ngazi za vijiji.. Ichague yenyewe msimamizi mkuu kwenye kila jimbo la uchaguzi... Asiyefungamana na upande wowote..
Lingine kubwa na muhimu...elimu itolewe kwa jeshi letu la police na vyombo vingine vya usalama kuhusu kutenda haki kwa vyama vyote..bila kuegemea upande wowote.
 
Back
Top Bottom