Maswali muhimu: Kwa mfumo na hali iliyopo, Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi itakuwaje? Itapatikanaje?

Ongezea RC, DC etc wasijihusishe kabisa na uchaguzi, wawe observers tuu. Kila kitu kifanywe na tume. Pili hii tabia ya kujaza mapolisi wengi in full military gears ipigwe marufuku coz it threatens voters. Kituo cha kupigia kura kiwe na police wachache wengine wawe mbali ili kama kuna uhitaji waitwe.
Hizo nafasi zao ni vyema kuzifuta kabisa zisiwepo.
 
Hawa wanaoitwa Viongozi hupenda sana Kutawala badala ya kuongoza,hawato kubali Mamlaka zao zipokwe na kurudishwa kwa Wananchi.Na ndio sababu kwa sasa Wananchi ndio wana watumikia Viongozi-Watawala.Tupo hapa Soon hizi kelele Jiwe atazijibu tena kwa Ukali sana.
Watawala kamwe hawataacha/hawatopenda mamlaka zao zipokwe.

Jukumu letu ni kuweka mizania ya hao watawala/viongozi wetu.
Na swala la msingi ni jinsi gani tutafikia hilo huku watawala wakiwa hawataki
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi apatikane kutoka Bungeni,Bunge lipige kura kumtafuta nani awe mwenyekiti wa Tume,Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atachagua wakurugenzi wake

Wakati wa uchaguzi mawakala wote wanaoviwakilisha vyama vya siasa vilivyojiandikisha kupiga kura lazima waweko vituoni,Ikiwa kama itatokea mawakala wanaowakilisha chama fulani wamekosekana katika kituo husika basi kituo kituo hicho kisitumike kupiga kura...

Kama itakuwa hivyo kuna uwezekano mkubwa haki itapatikana kwa vyama vyote,Bunge ndio serikali,Bunge linawakilisha vyama vyote vya siasa,Raisi ni taasisi ya chama fulani cha siasa,kama Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atachaguliwa na Raisi basi kuna umwezekano mkubwa kupendele upande wa Raisi...

Nawakilisha
Nawasilisha, na sio NAWAKILISHA
 
Nawasilisha, na sio NAWAKILISHA
Nawakilisha mawazo za fikra zangu,Mawazo na fikra zako wewe ziwasilishe.:D
Muhimu ni kufahamu maudhui ya hoja yangu,kuwasilisha na kuwakilisha(Submit and Present),hayo maneno hayana umuhimu wowote katika hoja yangu

Unaonaje kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi atachaguliwa katika mfumo huo(Bungeni)?,Je watanzania wapiga kura wanaweza kupata haki zao?Je Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi atajisikia huru na kuwaweza kuamua kwa haki bila ya upendeleo?
 
Back
Top Bottom