Maswali kwa Waziri Mkuu Hayana Tija Tena

maswali ya papo kwa papo kwa mtoto wa mkulima yalipangwa ili yatoe mwanya kwa serikali kutoa mawazo ya nini kinaendelea Arusha,
yule mbunge mwanjelwa aliyeshutumiwa kuiba mataulo Hotelini Arusha ndiye aliyepewa kazi ya kuuliza kuhusu mwafaka na nini kifate baada ya hali hii'
ccm mmechoka kwelikweli

Dola noma ! na hapa ndipo maandishi matakatifu yanapo thibitishwa

Kamati KUU nzima mnadanganya!!!!!! Hii aaibu ya Mwaka. Nyambafuuuuuuu
wewe ndio nyambafuuu, Pinda amezoea kupotosha na anaendelea kulindwa na yule nyambafu mwingine Ndugai, asingemzuia Silinde ampe taarifa waziri mkuu au amruhusu Mnyika aendelee kutoa maelezo yake kuhusu upotoshaji wa Pinda.

Wewe umesikia huyo aliyepinda wenu akipotosha na hamtaki kusikiliza upande wa Chadema, halafu unahukumu eti kamati kuu imedanganya.

Utapewa nyingi, naona tano hazikutoshi.

a NAMI NIMEMUONA YULE MWIZI WA MATAULO HOTELINI ARUSHA AKIULIZA MASWALI AMBAYO KWA TUNAOMJUA ATAKUWA KAPEWA KABLA ILI AYAULIZE. MWIZI WA MATAULO HANA GUTS ZA KUULIZA SWALI KAMA LILE UNLESS KAPEWA TU AULIZE ILI AONGEZE CV YAKE. MASWALI YALIPANGWA MAKUSUDI ILI KUTAKA KUUA NGUVU YA MKUTANO WA CDM ARUSHA LEO. MAGAMBA MMECHEMKA. ARUSHA HAWADANGANYIKI KWA MAGAMBA YENU NG'O. WANAJUA WANACHOKIFANYA WANAARUSHA.

NAE NDUGAI AKACHOMEKEA KUWA MADIWANI WALICHAGULIWA KWA NGUVU YA UMMA NA WAMEONDOLEWA KWA NGUVU YA VIKAO VYA CHAMA. KWAKE ANAONA WALITAKIWA WAONDOLEWE KWA NGUVU YA WANANCHI, LABDA. KWA SHERIA IPI HAPA TANZANIA? LABDA TUNGEKUWA NA SHERIA YA 'RECALL'. MTOTO WA MKULIMA AT LAST KAWAAMBIA WALE MADIWANI WALIOFUKUZWA WAENDE KORTINI NA AMEKANA YALE MAZUNGUMZO ALIYOFANYA NA MBOWE NA DR WA UKWELI.
hao ni CCM ; mfa maji haishi kutapatapa............................watajaribu mbinu zote lakini bila kutatua kero za mtanzania wa kawaida , kifo chao ni inevitable!
Kwani CCM hawaoni kuwa wanapotaka kuwavua baadhi ya wanachama wao magamba..hao wanachama na wenyewe si walichaguliwa na wananchi? ma zombie bana!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amemshangaa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kuwa kuna Mazungumzo ya Muafaka baina yake na mgogoro wa kisiasa wa Arusha.

Pinda akijibu maswali ya Papo kwa papo amesema alishituka sana kuona Taarifa ya kamati kuu ya CDM kuwa kuna mazungumzo baina yake naa CDM.

Anasema alikutana na Mbowe nyumbani kwake akiwa na Katubu wake Dr Slaa baada ya kuomba waonane nae,Mbowe alimwambia pinda kuwa kuna mgogoro kisiasa Arusha anaomba Waziri Mkuu aingilie kati,Pinda akamwambia kama kuna mgogoro huo basi mshirikisheni Msajili wa vyama vya Siasa.

Pinda amesema hakuna mazungumzo yoyote yanayo endelea kati yake na CDM juu ya Siasa za Arusha!

hao ni CCM ; mfa maji haishi kutapatapa............................watajaribu mbinu zote lakini bila kutatua kero za mtanzania wa kawaida , kifo chao ni inevitable!
Kwani CCM hawaoni kuwa wanapotaka kuwavua baadhi ya wanachama wao magamba..hao wanachama na wenyewe si walichaguliwa na wananchi? ma zombie bana!

Hicho ndicho kiini cha wananchi kutowapenda. Lakini wao wanan'gan'gana na uwongo tuu siku zote.

Job Ndungai wakati anatoa kile alichoita ufafanuzi wa kanuni ya 133, kwa Mh Mnyika sikupenda approach aloitumia kwa mbunge mwenzie.. Maneno kama ''KAA CHINI'' Tena yakitamkwa kwa jazba kana kwamba anaembiwa hakusikia.
Kwani Mh Mnyika angeambiwa kwa maneno kama.... tafadhali keti.., Huyo naibu spika angepungukiwa nini?

Mmmmh basi kazi ipo sasa Mbowe alitoa ripoti ya kuwa na Mazungumzo ya Muafaka ili iweje? Au ilikua ni danganya toto kwa wanachama wa CDM?

Mi pia naamini kuwa maswali ya leo yalipangwa kabla. Mh. Pinda alipokuwa akijibu swali la Mh. Hokororo kuhusu pembejeo za kilimo cha korosho ameonyesha viashiria vya kuwepo kwa upangaji wa maswali kabla. Inasikitisha kweli jamani... loh! Kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu kitakosa mvuto punde tu kikianza kutumiwa kwa maslahi ya chama fulani.

Na ndio maana akajibu "ningelijua kabla" kumbe maswali mengine anayafahamu kabla.

Ni huyo huyo Pinda aliyemshangaa Jairo alipobainika anahonga wabunge na hakuchukua hatua yoyote zaidi ya kulalamika mpaka Luhanjo alipomsimamisha kazi Jairo! Siidhani ka Pinda ni mtu wa kumtilia maanani kwani inaonekana hajui kutumia madaraka yake kwa hio sishangai hata akimshangaa Mbowe. Kwani Pinda anafikiri Mbowe na Slaa waliyoenda kumwona walikua wanazungumza ka viongozi wa CDM na yeye ka kiongozi wa CCM (na Serikali) au alifikiri wote walikua wanazungumza ka viongozi wa familia zao! Hivi Pinda anaposema mshirikisheni Msajili wa vyama vya siasa hayo hayakua mazungumzo baina ya CCM na Chadema kuhusu jinsi ya kumtumia Msajili kutatua matatizo ya mgogoro wa Arusha au Msajili alikua ashirikishwe kwenye mazungumzo ya matatizo ya familia zao?

Masikini CHADEMA kumbe KELELE zote zile NI UONGO WA kamati KUU .......mhhhhhh

Hapo kwenye red; very interesting. Usishangae soon hawa jamaa (CHADEMA) wakaja na ushahidi wa nguvu juu ya uwepo wa mazungumzo kati yao na PM. Tuombe Mungu kwamba majibu ya PM yalikuwa sahihi, kweli tupu, na thabiti otherwise sijui itakuwaje ushahidi ukiletwa. Kwa muda sasa kauli nyingi za CHADEMA zimethibitika na kwa hili la Arusha, siamini kama walidanganya na, in fact, sidhani kama walikuwa na sababu ya kudanganya.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amemshangaa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kuwa kuna Mazungumzo ya Muafaka baina yake na mgogoro wa kisiasa wa Arusha.

Pinda akijibu maswali ya Papo kwa papo amesema alishituka sana kuona Taarifa ya kamati kuu ya CDM kuwa kuna mazungumzo baina yake naa CDM.

Anasema alikutana na Mbowe nyumbani kwake akiwa na Katubu wake Dr Slaa baada ya kuomba waonane nae,Mbowe alimwambia pinda kuwa kuna mgogoro kisiasa Arusha anaomba Waziri Mkuu aingilie kati,Pinda akamwambia kama kuna mgogoro huo basi mshirikisheni Msajili wa vyama vya Siasa.

Pinda amesema hakuna mazungumzo yoyote yanayo endelea kati yake na CDM juu ya Siasa za Arusha!

kama walikutana na akaombwa kutoa ushauri na akautoa kuwa wamshirikishe msajili wa vyama inamaana na yeye anautambua ndiyo maana akatoa wazo hilo,je hayo sio mazungumzo yanayoendelea?pili sishawishiki kuwa walipokutana waliongea kwa sekunde tano kama jibu alivyolitoa lilivyofupi,je nini kingine kilichojili kwenye hichokikao chao mbona hajaeleza?w/mkuu anakwepa kulielezea swala la arusha kwani yeye mwenyewe,chama chake na serikali walisha sema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki,sasa kuongea kinyume na hapo ni kujifunga kwao.utoto wa kisiasa watauacha tu.peopleiz power.

Kama walikutana ni kweli waliliongelea hilo na siku zote msipokuwa na makubaliano katita jambo fulani jibu huwa majadiliano yanaendelea sasa anakana nini?angesema hatujakutana sawa tungejua mbowe muongo.aache ujinga yeye ni kiongozi mkubwa wa serikali na jue jinsi ya kujieleza katika issue muhimu kama hizi.

mmesahau kuwa pinda anashikilia rekodi ya kulidanganya bunge?

Mpaka leo hoja ya Lema imeshindikana kujadiliwa licha ya Kambi kuhoji mara kadhaa kupitia Tundu Lissu, Chiku Abwao na Kamanda Mkuu

Back
Top Bottom