Maswali kwa CDF Mstaafu, Venance Mabeyo

Nadhani uwepo wa Janabi uliwafanya watu wahisi kuwa alikuwa na kazi maalum, hasa kutokana na kilichotokea baada ya kifo cha JPM. Yaani wale mzee Kinana kurudishwa ghafra kwenye uongozi wa chama na mtoto wa yule mzee mwenzake waliokuwa wakimtukana JPM kurudishiwa uwaziri na mtoto wa JK kuteuliwa uwaziri. (kumbe it was just a coincidence)
Hoja ya kutopelekwa Ulaya nadhani wanadhani kama CDF hakutii hoja ya kuamuru akafie kwao, angeshindwaje kutotii kukataa kutibiwa nje, maana kwa maelezo ya Mabeyo ni kama JPM had no powers to order anything ambacho kwa busara ya Mabeyo kingesound illogical.
Kuhusu kuachwa apiganie uhai wake kama mateka, nadhani wanajiuliza kwa nini hata mke wake hakuruhusiwa awepo kushuhudia kinachotokea kwa baba watoto wake?
Inaonekana JPM died a very lonely and painful death.
Nadhani hakutendewa haki kufariki pasipo kuonana na kuwaaga wapendwa wake. It seems Mrs Magufuli knows nothing kilichokuwa kikiendelea kuhusu last minutes za mume wake (na inatia mashaka - it was designed so)

Nadhani baadhi ya watu ndivyo wanavyodhani
Kama ilikuwa hivyo basi CDF na jopo lake wapewe kongole kwa kumwacha mtesaji wa watu ateseke mpaka afe.Hata paka akitaka kumla panya mara tu anapomkamata humchezea na kumwacha ajifariji kuwa labda ataachiwa huru lakini kumbe ni kinyume chake na mwisho humwua panya yule na kumla.
 
Umenijibu kwa wepesi sana huku ukiwa na hoja ingine mfukoni!
Labda ungenijibu maswali muhimu kuliko haya uliyoamua kuyachagua kidogo ningekuelewa!

Je!
Nchi ilikuwa chini ya uongozi wa nani wakati wote wa ugonjwa hadi kifo cha JPM?
Je!
Katiba inasema nini kuhusu hilo?
Kama Mabeyo anatuambia Makamu wa Rais wala waziri mkuu hawakuwa na taarifa hadi walipopigiwa simu ili kutaarifiwa juu ya kifo!

Ni kina nani walikuwa wakiratibu mambo hayo yote?
Je!
Serikali ilikuwa chini ya amri za jeshi?
Kuhusu Dokta Janabi na uwepo wake muda woote wa Magufuli akiugulia pale.Je ni nani hasa na alikuwa wapi daktari maalumu wa Marehemu Rais Magufuli?
Na ni nini ilikuwa uwajibikaji na uhusika wake kwenye tukio zima?

Msiwe mnakimbilia kutoa majibu mepesi kwenye mambo mazito kama haya bila kwanza kutanguliza tafakuri.

Na ndio maana nimeunganisha tukio la kifo cha kijana pekee wa Mabeyo kwenye ile ajali baada tu ya muda mfupi wa kifo cha JPM kupita na nikasema hiyo ndio Karma!

Magufuli alifariki akiwa peke yake bila hata mke wake kuitwa ili kuja kushuhudia saa za mwisho za mumewe!
Walikuwa wakiitana kina Mabeyo na kamati yao tu!
Khe!
Mkuu kama ulivyosema damu ya mtu haipotei bure ni kweli kabisa, damu ya Lissu, Ben Saa 8, Akwilina hazikupotea bure, zilikwenda na mtu. Huwezi kuona hii inaweza kuwa ni sababu kubwa ya malaika wenu kusepa? Unajua Law of Karma? Usituletee hapa hoja zako za kipumbavu
 
Yeye Ndio CDF Ndio mkuu wa majeshi yote,alipopewa Amri na amirijeshi mkuu ukiyaka afanye Nini zaidi.

Kuhusu kupelekwa nyumbani haikuwezekana sababu akishakua Rais kuna muda hawezi jiamulia kilakitu anaamurishwa na kuwa mali ya uma.
Ndio maana kula kuvaa kwake ni gharama ya nchi.

Swala la kutoambiwa Makamu ni swala la kawaida.

Kama angekua anamchukia Makamu asingepambania kuapishwa kwake.
 
Alimpambania lakini nadhani hakujua kuwa washauri watakuwa wakimpotosha.
Pengine ndiyo message ya lile chozi.
Mama inabidi sasa apunguze kupotoshwa.
 
Maswali yako naona yanajibika, naona umeacha hisia zikutawale kwa kiasi kikubwa ndio tatizo lako.

-Hii tabia ya kuficha ugonjwa wa viongozi wetu niseme ndio tabia ya serikali yetu, walianzia kwa Hayati Magufuli wakaja nayo mpaka kwa VP wa sasa.

- Uwepo wa Dr. Janabi eneo la tukio kwangu nachukulia tofauti, inawezekana aliitwa pale akatoe ushauri wake wa kitabibu juu ya mgonjwa, hili hutokea kwa madaktari wengi, sioni sababu ya kuwa na hofu.

- Kuhusu Hayati JPM kupelekwa Mzena, najua hiyo ndio hospitali yao wazito wa hii nchi, hata Mzee Hayati Mwinyi nae alienda kutibiwa pale last month tukaambiwa mauti yalimkuta pale.

- Hayati JPM kwa ile tabia yake ya kutopenda mambo ya wazungu, sishangai kuona kwanini hakupelekwa huko Ulaya unapopataka ili akatibiwe.

- Unaposema Hayati Magufuli aliachwa akipigania uhai wake kama mateka napo unapokosea, mgonjwa akiwa amelazwa hospitali akiendelea na matibabu hutembelewa na ndugu au jamaa zake, wakati ule hauwezi kusema aliachwa akipigania uhai wake kama mateka, wakina Mabeyo na wengine ndio walikuwa jamaa zake wakati ule, Hayati JPM akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu, na Mabeyo akiwa kama CDF.

emoji830.png
Hili suala la kushirikishwa kwa wengine, mbona inawezekana kabisa ikawa walishirikishwa kwa njia nyingine za kimawasiliano, mimi nijuavyo, hakuna hospitali inayoeleweka itaruhusu lundo la watu bila kujali vyeo vyao wakajazane wodini kwa mgonjwa, huo utakuwa ni usumbufu kwa mgonjwa usiotakiwa.

Kwangu, kama wakati wa kifo cha Hayati JPM pasingekuwepo na ugonjwa wa Corona, hapo ningeweza kuamini hizi rumours za mwendazake kuondolewa na wajanja, lakini kama Corona ilikuwepo, na ikaondoka na baadhi ya wasaidizi wa Hayati JPM, sioni kwanini isingemuondoa na JPM ikiwa yeye hakuwahi kuchukua tahadhari zozote za kisayansi kujikinga dhidi ya ule ugonjwa.
Nimemshangaa sana anavyohoji uwepo wa Prof Janabi kwenye matibabu ya JPM ambaye tuliambiwa alikufa kwa ugonjwa wa moyo. Alitaka nani awepo?
Angejiongeza kifdogo tu hata kwenye google asome cv za huyo tuliyeambiwa ndiye alikuwa daktari binafsi wa JPM akijulikana kama Prof Mabula Mchembe. Kwenye google cv yake inasomeka kama ifuatavyo:
Dr. MABULA DAUD PAUL MASALU MCHEMBE
MD, M.Med(Surgery)(UDSM),FCS(ECSA),Cert.Cardiothoracic Surgery.

Kwa hiyo daktari binafsi wa JPM ni surgeon, bingwa wa upasuaji. Ugonjwa tulioambiwa umemuua ni ugonjwa wa moyo, ambao bingwa wa fani hiyo ni Prof Janabi. Hivyo ilikuwa muhimu na lazima kumshirikisha Janabi katika jopo la kumtibia mkuu JPM.
 
Umenijibu kwa wepesi sana huku ukiwa na hoja ingine mfukoni!
Labda ungenijibu maswali muhimu kuliko haya uliyoamua kuyachagua kidogo ningekuelewa!

Je!
Nchi ilikuwa chini ya uongozi wa nani wakati wote wa ugonjwa hadi kifo cha JPM?
Je!
Katiba inasema nini kuhusu hilo?
Kama Mabeyo anatuambia Makamu wa Rais wala waziri mkuu hawakuwa na taarifa hadi walipopigiwa simu ili kutaarifiwa juu ya kifo!

Ni kina nani walikuwa wakiratibu mambo hayo yote?
Je!
Serikali ilikuwa chini ya amri za jeshi?
Kuhusu Dokta Janabi na uwepo wake muda woote wa Magufuli akiugulia pale.Je ni nani hasa na alikuwa wapi daktari maalumu wa Marehemu Rais Magufuli?
Na ni nini ilikuwa uwajibikaji na uhusika wake kwenye tukio zima?

Msiwe mnakimbilia kutoa majibu mepesi kwenye mambo mazito kama haya bila kwanza kutanguliza tafakuri.

Na ndio maana nimeunganisha tukio la kifo cha kijana pekee wa Mabeyo kwenye ile ajali baada tu ya muda mfupi wa kifo cha JPM kupita na nikasema hiyo ndio Karma!

Magufuli alifariki akiwa peke yake bila hata mke wake kuitwa ili kuja kushuhudia saa za mwisho za mumewe!
Walikuwa wakiitana kina Mabeyo na kamati yao tu!
Khe!
Upon sahihi kuuliza maswali haya, lakini kwa kweli haisaidii sana zaidi ya kuongeza huzuni Kwa familia. JPM alipenda kuzuungwa na viongozi wa ulinzi na usalama na labda yalikuwa maelekezo Yako. By the way maisha yetu yapo ktk mikono ya Mungu.
 
Mi naongezea kuhusu nchi ilikua chini ya nani wakati anaumwa.

Mtoa mada amesahau kua JPM kwenye wakati wake alikua hafuati sheria za nchi na pia aliowaamini walikua ni wale waliokua kwenye cycle yake na ndo walikua na nguvu kuliko hata makamu wa Rais. Ndo maana mara kadhaa wale wapendwa wake waliwavimbia baadhi ya watu ambao wapo juu yao vyeo vyao.

Mtu kama Bashiru yeye alikua na power kubwa kumuwajibisha yeyote nchi hii ukitoa magufuli na kwa hisia zilizokuwepo alikua akiandaliwa kuja kuwa mkuu wa nchi baadae ndo maana alimoa nafasi zile nyeti.

Kuhusu kua wakuu wa vyombo vya ulinzi muda wote kua mbele ya mstari ni kwasababu marehemu yeye alikua na maadui wengi na mara kadha alinukuliwa akisema ametoa uhai wake,pengine jukumu la kumsimamia kuwapa wao aliamini ni watu waaminifu si rahisi kumsaliti.

Kwanini alipodai kurudoshwa nyumbani Mabeyo alimwambia jambo la afya si la CDF, mkuu wa majeshi sio daktari ingekuaje aamuru mgonjwa arudi home na akafia huko si ingeonekana amemuua kwa kukosa matibabu stahiki. Mara kadhaa sisi tumeuguza mgonjwa anadai kurudi nyumbani ila tunamkatilia kwasababu nyumbani sio sehemu salama kwa matibabu hilo liko wazi. Mtoa mada alisema kwanini hawajampeleka Hospital ya maana ,mimi nimesikia CDF alisema walianzia Muhimbili(hiyo national hospital imejengwa na serikali kwa watu wote) ila walipoona hakuna utulivu ndo wakahamia Nzena akiwa na madaktari wake na alimtaja jina na prof janab akiwepo.

NB:kama hayati angekua anafuata sheria walau nusu basi mambo mengi yasingekua hivi, pengine angekua hai.
Kitendo cha Lissu kupigwa risasi, ile damu ilomwagika, na kila mtanzania aliingiwa na simanzi ktk tukio lile, ilikuwa suala la muda tu karma kuchukua nafasi yake.
 
Kama profesa Janabi aliitwa hospitalini kutoa ushauri kwanini daktari maalumu wa rais Mchem

Kama profesa Janabi aliitwa hospitalini kwenda kutoa ushauri kwanini daktari Mchembe ambaye ni daktari maalumu wa rais JPM hakushirikishwa kwenye jopo la matibabu kuanzia mwanzo hadi kikapu kilipodondoka chini na alitengwa?
*Why was Professor Janabi called to the hospital to provide a bit of consultative advice while a specialized doctor Mchembe for president JPM was not involved in the medical team from scratch to the climax of the tragic event and was isolated? The recent response of the retired CDF to the TBC journalist's interview which is currently spiraling viral on the social media platform is just the beginning, as there is more to uncover.

Tiba ya JPM ilihitaji maarifa zaidi ya yale aliyonayo daktari wake (Prof Mchembe) ambaye ni surgeon. Na kwenye mahojiano retired CDF amesema Mchembe alikuwepo. Kiitifaki, kama umewahi kutibiwa hospitali utaelewa kuwa daktari wako anayekutibu ndiye anayefanya consultation kwa wenzake au kuandika rufaa. Kwa mantiki hiyo, Prof Mchembe ndiye aliyeomba msaada wa Prof Janabi katika hiyo case.
 
Nadhani uwepo wa Janabi uliwafanya watu wahisi kuwa alikuwa na kazi maalum, hasa kutokana na kilichotokea baada ya kifo cha JPM. Yaani wale mzee Kinana kurudishwa ghafra kwenye uongozi wa chama na mtoto wa yule mzee mwenzake waliokuwa wakimtukana JPM kurudishiwa uwaziri na mtoto wa JK kuteuliwa uwaziri. (kumbe it was just a coincidence)
Hoja ya kutopelekwa Ulaya nadhani wanadhani kama CDF hakutii hoja ya kuamuru akafie kwao, angeshindwaje kutotii kukataa kutibiwa nje, maana kwa maelezo ya Mabeyo ni kama JPM had no powers to order anything ambacho kwa busara ya Mabeyo kingesound illogical.
Kuhusu kuachwa apiganie uhai wake kama mateka, nadhani wanajiuliza kwa nini hata mke wake hakuruhusiwa awepo kushuhudia kinachotokea kwa baba watoto wake?
Inaonekana JPM died a very lonely and painful death.
Nadhani hakutendewa haki kufariki pasipo kuonana na kuwaaga wapendwa wake. It seems Mrs Magufuli knows nothing kilichokuwa kikiendelea kuhusu last minutes za mume wake (na inatia mashaka - it was designed so)

Nadhani baadhi ya watu ndivyo wanavyodhani
Sababu ya mke wa JPM kushindwa kumuuguza mumewe imeandikwa hapa: Mke wa Rais Magufuli naye mgonjwa? Azuiwa kumwona mumewe hospitalini - Sauti Kubwa
 
Hatimae tumemsikia na kumshuhudia aliekuwa Chief of Defense Forces kupitia media na mtu ambae inaonekana ndie alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa siku zote Marehemu JPM akiwa anapigania uhai wake na hatimae kuondoka Duniani!

Lakini maelezo yake yameongeza sintofahamu zaidi kuliko alivyotarajia. Na kwa wengine hasa mimi binafsi,

Sasa nimeelewa maana ya
Kwa kusahihisha tu Karma lazima ianzie kwa Ben Saanane , Azori Gwanda , Leopold Lwajabe na wengineo wengi waliokumbana na mkono wa chuma wa dikteta.
"karma". Muda mfupi baadae mtoto wa kiume wa Mabeyo aliekuwa Pilot pale Coastal Aviation alianguka na ndege uwanja wa Seronera akiwa yeye na rubani mwanafunzi wa vitendo (trainee) na wote walifariki Dunia.

Hili kwa sasa sintaliongelea sana ila nimeliweka hapa ili kuonyesha ukuu wa Mungu na Malipo yake kwa wale anaotaka kuwapa majibu ya matendo yao wakiwa bado hai.

Na wakati mjadala ukiendelea kuhusu mambo kadhaa ya kisiasa kutoka na hotuba ya Mstaafu Mabeyo!
Sisi wengine tunajiuliza wwali muhimu:
Magufuli ndio alianzisha tabia ya kuficha vitu na uongo ndio aliwapa kina Kabudi ndege wakaenda Madagascar wakaleta juice wakisema rais kule anagawa mwenyewe wakaishia kunywa wao wakapiga mapicha wengine wakaambiwa hawatokunywa hadi iende maabara ya NIMR haijawahi kuletwa majibu ya tafiti za NIMR hatujui hata kama Magufuli mwenyewe aliyetoa ndege alikunywa ile juice au lah!
Ni kwa nini walituficha ugonjwa wa mpendwa Rais wetu JPM?
Tunajiuliza:
Dr Janabi alikuwepo pale JKCI muda tu hatukutokea nje ya nchi siku Magufuli analazwa labda hii ingeleta clue kidogo na senior specialist wa cardiology pale so kuwepo kwake pale sio tatizo .
Dk Janabi alikuwa pale muda wote akifanya nini ilhali yeye hakuwahi kuwa Daktari wa JPM, bali alikuwa ni Daktari wa familia ya Kikwete na pia swahiba ya JK?

Tunajiuliza
Mzena ameenda Mkapa na imekuwepo muda pale , Mkapa kafia pale ,Binti Nyerere , na Magufuli mwenyewe sasa Mwinyi sasa sijui kufichwa huko ni kupi
...ni kwa nini walikwenda kumficha pale Mzena badala ya kumpeleka kwenye hospitali nyingine yenye hadhi ikiwezekana hata nje ya nchi?
Nje ya nchi Magufuli ndio alikuwa akisema hapataki wangempeleka akafia huko si mngepiga kelele za kutosha kuwa "mabeberu " walimuua ila pia Magufuli alizuia vibali vya watumishi wa umma kusafiri nje na akasema anaboresha hospitali watu watatibiwa hapo hapo hakuna sababu ya kwenda nje.
Tunajiuliza. Kama waziri mkuu alituficha. Makamu wa Rais alituficha!
Ni nani au kikundi gani kilikuwa kinaratibu haya mambo?
Madaktari ndio wanaamua mgonjwa aruhusiwe au lah , huko alikotaka kwenda kulikuwa na huduma bobezi za kitabibu ?

ex-CDF angedictate hii na akafia Chato si mngesema Mabeyo amesuka mkakati , pia kwa wimbi lile la UVIKO la pili mtu atatolewaje hospitali arudi nyumbani akiwambukiza wa nyumbani wote hujiulizi kwanini familia yake haikuwepo hospitali ?
Tunajiuliza: Kama Mkuu wa majeshi aliambiwa na JPM awali kwamba wamrudishe nyumbani akafie huko.Ni kwa nini aligoma kutimiza takwa la Marehemu? Na kwa nini hakuwashirikisha wengine ili wachukuwe maamuzi sahihi?
Ukweli usemwe Magufuli alikuwa mgonjwa wa muda mrefu na dalili za kuchoka zilishaanza kuonekana mosi angalia kampeni za "uchafuzi" mkuu 2020 alikuwa anapiga kampeni leo anapumzika siku 8 , kila Magufuli alipokuwa akisimama kulikuwa na "air cooler " nyuma yake hii kwa wachache tuliona sio dalili nzuri hasa kwa open space kama ile na hewa ni ya kutosha air cooler ni ya nini?

Pia baada ya wimbi la kwanza kwa kuwa alikuwa "prone " kuambukizwa UVIKO alifuata ushauri vizuri alichimbia Chato kuanzia March 2020 hadi May mwishoni 2020 , Baada ya Mahiga kufariki hata Mwigulu aliapishwa Chato maana yake ni nini Chato waliifanya kama ngome ya kumficha na kumfanyia 'isolation' maana wimbi lile lingeweza kumfyeka kama asingekuwa makini ila awamu ya pili akapuuza wimbi likiwa limechachamaa February 2021 akatoka kwenda kuzindua soko la Kingalu Morogoro, Kijazi interchange na stendi ya mbezi huko kote alijiingiza kwenye mikusanyiko isiyo na sababu wakati yeye yuko kwenye yale makundi "prone" kupata UVIKO na kupelekea matatizo makubwa kutokana na complications za kupumua.
Je, Magufuli aliugua ugonjwa gani huo ambao madaktari walikaa pembeni wakimshuhudia akipigania uhai wake akiwa kama mateka?
Utawala wa Magufuli chain of command haikuwa sawasawa ndio maana hata Sabaya alisema yeye anampigia Magufuli simu hata saa 8 usiku na anapokea na yeye anaripoti kwa Magufuli moja kwa moja asiulizwe na mtu yoyote je hii ni sawa?

Polepole alikuwa anapigia mawaziri simu kwenye kipindi cha TV na kuwauliza maswali live wakati ofisi zipo na miongozo na muda wa kazi upo , yani mtu yupo kwake kapumzika saa 2 usiku apigiwe simu kisa mwenezi ana kipindi hapo kuna work-life balance kweli?

Magufuli alitengeneza magenge ya watu waaminifu na tiifu kwake aliowaamini bila kufuata chain of command maana tulishuhudia Makonda akimbeza Spika wa bunge live wakati spika wa bunge ni mkuu wa mhimili kabisa .

Pia waliohoji Magufuli yupo wapi walitishiwa , kuambiwa hawaitakii mema Tanzania na wengine kukamatwa haya aliyasema Kasim Majaliwa akiwa msikitini Iringa , March 12 2021
Anasema alipofariki wao wakuu wa vyombo ndio waliwajulisha viongozi kama PM, CS na baadae makamu wa rais, ena wote hawakuwepo eneo la tukio.
Hawa hata wangekuwepo wangefanya nini?

Bashiru Ali aliteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi kinyume na katiba , katiba inasema katibu mkuu kiongozi atatakiwa kuwa mtumishi wa umma je Bashiru Ali alikuwa ni mtumishi wa umma bado baada ya kutoka UDSM?
Hatuoni mahala makamo wa Rais, mwanasheria mkuu, Wala jaji mkuu au spika wakiwa na maamuzi yeyote. Kila kitu kilipangwa na jeshi. Huyu Mabeyo ameongea, iko siku na wengine wataanza kuongea. Damu ya mtu huwa haipotei bure.
Samia alitengwa na kundi la Magufuli ambalo ndio wahuni hao waliotaka kumsimika mtu wao ili waendeleze maslahi yao waliyoyapata Magufuli akiwa madarakani hivyo waliona akishaondoka kuna namna watapwaya na ndio uhalisia leo hii 99% ya wafuasi tiifu wa Magufuli wametulia kama maji mtungini
Kama kuna jambo lilipangwa na kufanywa na kikundi fulani,kinyume na tulivyoamishwa sisi wananchi. Na kwa jinsi siku ya Jana ilivyopita bila hata serikali ya Saa100 kujishughulisha na lolote kuhusu kumbukumbu hii muhimu nchini.
Tukiwa tunaendelea kusubiri shuhuda tunahitaji kupata taarifa za alipo Ben Saanane, Azori Gwanda.

Nani walikuwa nyuma ya tukio la kutekwa kwa Mohamed Dewji ,Roma Mkatoliki na wengineo wengi.

Nani alikuwa nyuma ya shambulizi la risasi kwa Tundu Lissu September 7 ,2017

Tutashuhudia taraatiiibu!

R.I.P Jemedari JPM!

Wameanza kuropoka huku!
 
Maswali yako naona yanajibika, naona umeacha hisia zikutawale kwa kiasi kikubwa ndio tatizo lako.

-Hii tabia ya kuficha ugonjwa wa viongozi wetu niseme ndio tabia ya serikali yetu, walianzia kwa Hayati Magufuli wakaja nayo mpaka kwa VP wa sasa.

- Uwepo wa Dr. Janabi eneo la tukio kwangu nachukulia tofauti, inawezekana aliitwa pale akatoe ushauri wake wa kitabibu juu ya mgonjwa, hili hutokea kwa madaktari wengi, sioni sababu ya kuwa na hofu.

- Kuhusu Hayati JPM kupelekwa Mzena, najua hiyo ndio hospitali yao wazito wa hii nchi, hata Mzee Hayati Mwinyi nae alienda kutibiwa pale last month tukaambiwa mauti yalimkuta pale.

- Hayati JPM kwa ile tabia yake ya kutopenda mambo ya wazungu, sishangai kuona kwanini hakupelekwa huko Ulaya unapopataka ili akatibiwe.

- Unaposema Hayati Magufuli aliachwa akipigania uhai wake kama mateka napo unapokosea, mgonjwa akiwa amelazwa hospitali akiendelea na matibabu hutembelewa na ndugu au jamaa zake, wakati ule hauwezi kusema aliachwa akipigania uhai wake kama mateka, wakina Mabeyo na wengine ndio walikuwa jamaa zake wakati ule, Hayati JPM akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu, na Mabeyo akiwa kama CDF.

Hili suala la kushirikishwa kwa wengine, mbona inawezekana kabisa ikawa walishirikishwa kwa njia nyingine za kimawasiliano, mimi nijuavyo, hakuna hospitali inayoeleweka itaruhusu lundo la watu bila kujali vyeo vyao wakajazane wodini kwa mgonjwa, huo utakuwa ni usumbufu kwa mgonjwa usiotakiwa.

Kwangu, kama wakati wa kifo cha Hayati JPM pasingekuwepo na ugonjwa wa Corona, hapo ningeweza kuamini hizi rumours za mwendazake kuondolewa na wajanja, lakini kama Corona ilikuwepo, na ikaondoka na baadhi ya wasaidizi wa Hayati JPM, sioni kwanini isingemuondoa na JPM ikiwa yeye hakuwahi kuchukua tahadhari zozote za kisayansi kujikinga dhidi ya ule ugonjwa.
Kama hospital ya Mzena ni ya Viongozi kwanini MKAPA na LOWASSA hawakupelekwa?
 
Back
Top Bottom