CDF Mabeyo amepasua masikio yetu, pata madini ya Askofu Bagoza

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,608
93,374
CDF MABEYO AMEPASUA MASIKIO YETU

Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo, amesema maneno yanayopasua ngoma za masikio yetu. Amefanya mahojiano na “kutoa siri” za kilichotokea miaka 3 iliyopita wakati hayati Rais JPM anaaga dunia. Nimesita kumpongeza na nimesita kumlaumu.

Nimewahi kujishauri mwenyewe kuwa Tanzania ingekuwa familia yangu ninayoitawala mwenyewe, ningeondoa zuio (declassify) linalozuia kuchapisha habari za kuugua, kufa, kuhamisha madaraka, mazishi na kuunda serikali mpya pale kiongozi anapokufa akiwa madarakani. Sababu zangu ni hizi:

1. Kifo cha kawaida si mapinduzi ya serikali. Kwa hiyo inawafariji wananchi kujua kiongozi wao alivyoondoka na mwingine akaingia.

2. Inaondoa uwezekano wa watu kujipa madaraka ya kuhodhi habari na kuzitumia kujinufaisha au hata kuumiza wengine.

3. Ni fursa ya kuboresha taratibu zetu za mipito ya madaraka (power transitions). Hata mipito ya madaraka baada ya chaguzi imegubikwa na usiri na mikwala miiingi bila sababu. Wapo wanaonufaika binafsi na usiri huu hata kuifilisi nchi.

4. Uwazi katika tukio kubwa kama hili ni darasa la Sayansi ya Siasa na Historia ya Madaraka (The History and Anatomy of Power). Kizazi cha vijana wanaoishia kuwa machawa badala ya kukalishwa chini na kufundishwa kwa nini CDF awe Mwenyekiti wa wakuu wa vyombo? Kwa nini wakuu wa vyombo wabishane juu ya nani ajulishwe kifo kwanza? Kwa nini Makamu aape kabla ya kuzika? Kwa Spika afikiri yeye awe rais badala ya Makamu? Haya ni maswali muhimu lakini kwa sababu ya usiri (classification) yanageuka kuwa uzushi na uchochezi unaoweza kumfanya mtu kunyea ndoo😭.

5. Mungu wetu hajaacha kuja kuvuna kutoka shamba lake la viongozi. Alikuja, anaweza kuja na ataendelea kuja. Si wakati tutakuwa na CDF wa aina hii (kwa wema na ubaya). Laweza kutokea kosa mkajikuta mna CDF Mpumbafu kama Kalikawe. Itakuwaje? Kufichaficha chakula humnenepesha panya kuliko paka!

6. Tuchukulie CDF kasema kweli. Aje IGP aseme kweli zaidi. Aje DGIS naye aseme asiyoyajua IGP na CDF. Baadate tumsikie daktari wa Mzena naye aje na ya kwake. Mjane achukie aone kwa nini nilifichwa, naye aseme. Padre, Kardinali, dereva, maabara, mwanasheria, ADC, nk. Nionavyo, CDF kafunua chupa na jini limetoka. Tukililazimisha kurudi kwenye chupa, itapasuka. Usiri ni kichaka cha maovu.

7. Hata kwa uchache; body language ya CDF inasema mengi kuliko mdomo wake. Mikono na miguu yake havijatulia na vinajitahidi kuzuia tusichokijua. Naamini alipata ruhusa kusema aliyosema. Kuutumikia ukweli ni kibarua kigumu. Hakuna mshahara utoshao kumlipa mkweli. Nimebaki kujiuliza wapi mbali kutoka DsM: Tanga au Dodoma? Tuseme ilikuwa nia njema lakini haitabakia nia njema wakati wote. Mama amebeba mengi, siachi kumwombea.

8. Naweza kuwa nimeshiba maharage. Nitamke. Wanaosita kuruhusu mchakato wa katiba mpya ukamilike au wanaosita kufanya marekebisho ya katiba kuondoa hodhi ya makundi katika maisha ya kisiasa katika taifa letu, hawalitakii taifa letu mema. Tusitegemee kila wakati Mungu aingilie au mtu mmoja (mwema au kichaa) ateke hatima ya taifa letu. Kuna siku tutalia na haoatakuwa na mtu wa kututuliza.

Leo sifiki 10, ngoja niishie hapa.
 
Kufichaficha chakula humnenepesha panya kuliko paka!

6. Tuchukulie CDF kasema kweli. Aje IGP aseme kweli zaidi. Aje DGIS naye aseme asiyoyajua IGP na CDF. Baadate tumsikie daktari wa Mzena naye aje na ya kwake. Mjane achukie aone kwa nini nilifichwa, naye aseme. Padre, Kardinali, dereva, maabara, mwanasheria, ADC, nk. Nionavyo, CDF kafunua chupa na jini limetoka. Tukililazimisha kurudi kwenye chupa, itapasuka. Usiri ni kichaka cha maovu.
Uandishi na kujenga hoja na ikaeleweka ni kipaji, Kongole kwake #Bagoza.
 
7. Hata kwa uchache; body language ya CDF inasema mengi kuliko mdomo wake. Mikono na miguu yake havijatulia na vinajitahidi kuzuia tusichokijua. Naamini alipata ruhusa kusema aliyosema. Kuutumikia ukweli ni kibarua kigumu. Hakuna mshahara utoshao kumlipa mkweli. Nimebaki kujiuliza wapi mbali kutoka DsM: Tanga au Dodoma? Tuseme ilikuwa nia njema lakini haitabakia nia njema wakati wote. Mama amebeba mengi, siachi kumwombea.
Naam! hoja juu ya hoja.
 
Hivi ni kwanini VP alikuwa ahaminiki?
Lazima kulikuwa na sababu…
Kwenye story za Mabeo amejikuta ana wataja hadi waliokuwa wanampa taarifa Lissu za mgonjwa!
 
Back
Top Bottom