Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 6,573
- 10,661
Nimependa mchanganuo wako pia. Nami naongeza kidogo.Mi naongezea kuhusu nchi ilikua chini ya nani wakati anaumwa.
Mtoa mada amesahau kua JPM kwenye wakati wake alikua hafuati sheria za nchi na pia aliowaamini walikua ni wale waliokua kwenye cycle yake na ndo walikua na nguvu kuliko hata makamu wa Rais. Ndo maana mara kadhaa wale wapendwa wake waliwavimbia baadhi ya watu ambao wapo juu yao vyeo vyao.
Mtu kama Bashiru yeye alikua na power kubwa kumuwajibisha yeyote nchi hii ukitoa magufuli na kwa hisia zilizokuwepo alikua akiandaliwa kuja kuwa mkuu wa nchi baadae ndo maana alimoa nafasi zile nyeti.
Kuhusu kua wakuu wa vyombo vya ulinzi muda wote kua mbele ya mstari ni kwasababu marehemu yeye alikua na maadui wengi na mara kadha alinukuliwa akisema ametoa uhai wake,pengine jukumu la kumsimamia kuwapa wao aliamini ni watu waaminifu si rahisi kumsaliti.
Kwanini alipodai kurudoshwa nyumbani Mabeyo alimwambia jambo la afya si la CDF, mkuu wa majeshi sio daktari ingekuaje aamuru mgonjwa arudi home na akafia huko si ingeonekana amemuua kwa kukosa matibabu stahiki. Mara kadhaa sisi tumeuguza mgonjwa anadai kurudi nyumbani ila tunamkatilia kwasababu nyumbani sio sehemu salama kwa matibabu hilo liko wazi. Mtoa mada alisema kwanini hawajampeleka Hospital ya maana ,mimi nimesikia CDF alisema walianzia Muhimbili(hiyo national hospital imejengwa na serikali kwa watu wote) ila walipoona hakuna utulivu ndo wakahamia Nzena akiwa na madaktari wake na alimtaja jina na prof janab akiwepo.
NB:kama hayati angekua anafuata sheria walau nusu basi mambo mengi yasingekua hivi, pengine angekua hai.
Hao akina Mabeyo, Diwani na Sirro hawakumjulisha Makamu wa Rais kipindi anaumwa kwa kuogopa namna Magufuli atakavyo REACT ikiwa atataoka hospitali akiwa amepona.
Kuhusu kumtaarifu Makamu baada ya Magufuli kufariki nadhani walikuwa kwenye hilo jaribio la kutaka kumpora Samia u-Rais. Na isingekuwa Mabeyo Rais angekuwa ni Job Ndugai au Bashiru Ally.
Big respect kwa Venance Salvatory Mabeyo, Mkatoliki mwenzangu aliyenyooka kuliko hata Cardinal Pengo