Maswali kwa CDF Mstaafu, Venance Mabeyo

Mi naongezea kuhusu nchi ilikua chini ya nani wakati anaumwa.

Mtoa mada amesahau kua JPM kwenye wakati wake alikua hafuati sheria za nchi na pia aliowaamini walikua ni wale waliokua kwenye cycle yake na ndo walikua na nguvu kuliko hata makamu wa Rais. Ndo maana mara kadhaa wale wapendwa wake waliwavimbia baadhi ya watu ambao wapo juu yao vyeo vyao.

Mtu kama Bashiru yeye alikua na power kubwa kumuwajibisha yeyote nchi hii ukitoa magufuli na kwa hisia zilizokuwepo alikua akiandaliwa kuja kuwa mkuu wa nchi baadae ndo maana alimoa nafasi zile nyeti.

Kuhusu kua wakuu wa vyombo vya ulinzi muda wote kua mbele ya mstari ni kwasababu marehemu yeye alikua na maadui wengi na mara kadha alinukuliwa akisema ametoa uhai wake,pengine jukumu la kumsimamia kuwapa wao aliamini ni watu waaminifu si rahisi kumsaliti.

Kwanini alipodai kurudoshwa nyumbani Mabeyo alimwambia jambo la afya si la CDF, mkuu wa majeshi sio daktari ingekuaje aamuru mgonjwa arudi home na akafia huko si ingeonekana amemuua kwa kukosa matibabu stahiki. Mara kadhaa sisi tumeuguza mgonjwa anadai kurudi nyumbani ila tunamkatilia kwasababu nyumbani sio sehemu salama kwa matibabu hilo liko wazi. Mtoa mada alisema kwanini hawajampeleka Hospital ya maana ,mimi nimesikia CDF alisema walianzia Muhimbili(hiyo national hospital imejengwa na serikali kwa watu wote) ila walipoona hakuna utulivu ndo wakahamia Nzena akiwa na madaktari wake na alimtaja jina na prof janab akiwepo.

NB:kama hayati angekua anafuata sheria walau nusu basi mambo mengi yasingekua hivi, pengine angekua hai.
Nimependa mchanganuo wako pia. Nami naongeza kidogo.

Hao akina Mabeyo, Diwani na Sirro hawakumjulisha Makamu wa Rais kipindi anaumwa kwa kuogopa namna Magufuli atakavyo REACT ikiwa atataoka hospitali akiwa amepona.

Kuhusu kumtaarifu Makamu baada ya Magufuli kufariki nadhani walikuwa kwenye hilo jaribio la kutaka kumpora Samia u-Rais. Na isingekuwa Mabeyo Rais angekuwa ni Job Ndugai au Bashiru Ally.

Big respect kwa Venance Salvatory Mabeyo, Mkatoliki mwenzangu aliyenyooka kuliko hata Cardinal Pengo
 
Hata sijachagua maswali ya kukujibu, ngoja niendelee...

- Nchi inakuwa chini ya uongozi wa VP, hili lipo kikatiba.

- Katiba inazungumzia pale Rais anapokuwa nje ya nchi, kwa shughuli za kikazi, ugonjwa au vinginevyo, Makamu wake ndie anashika hatamu. Au ulitaka Katiba iseme kitu kuhusu VP kutopewa taarifa za ugonjwa wa Hayati JPM?!

Nani kati yenu mwenye uhakika kama VP hakuwa anafahamu chochote kuhusu hali ya ugonjwa wa Hayati JPM, narudia tena zipo njia nyingine za mawasiliano kufikisha ujumbe kwa mhusika, wakati ambao Mabeyo hakuwepo, ndio maana nasisitiza mwenye jibu la mwisho kuhusu hili, ni Samia pekee.

Mabeyo kazungumzia aliyoyaona mwenyewe, mengine yaongelewe na wengine. Naamini hata PM nae akiulizwa kuhusu hili jambo atakuja na part yake tofauti ambayo Mabeyo hakuigusa, hivyo hivyo kwa VP na wengine.

- Suala la waratibu, hao mbona wanaonekana wazi, ukianza na Mabeyo mwenyewe kwa cheo chake, PM Majaliwa, waliokuwa eneo la tukio, na viongozi wengine serikalini inawezekana walishirikishwa kwa mbali, wasingeweza wote kujazana kwenye chumba cha mgonjwa.

- Uwepo wa Dr. Janabi eneo la tukio pia nimekwambia inaweza kuwa ni ushauri wake kitaalamu ndio uliohitajika eneo husika, kama hata Dr. binafsi wa Hayati Magufuli humfahamu mpaka unaniuliza ni nani hasa, mimi siwezi kukupa jibu kwasababu hata nami sikuwa namfahamu.

• Hapa nakushangaa, kama hukuwa ukimfahamu daktari wa Hayati Magufuli, kwanini ushangae kutokuwepo kwake?!

• Mtu ambaye hata hukuwa ukimfahamu, unaulizia vipi uwajibikaji wake?!

Hata kuhusu kifo cha kijana wa Mabeyo kwenye ajali { sikumbuki kilitokea wakati gani}, napo sioni cha kushangaza, hakuna karma pale; ni nani kati yetu asiyekufa? au wewe ndie hupanga nani afe lini? mimi sioni uzito wowote wa hoja zako.
Umemjibu vizuri kama akiendelea kujiuliza kwako maswali ya kindezi , basi mgumu kuelewa na mwepesi wa kusahau
 
Umenijibu kwa wepesi sana huku ukiwa na hoja ingine mfukoni!
Labda ungenijibu maswali muhimu kuliko haya uliyoamua kuyachagua kidogo ningekuelewa!

Je!
Nchi ilikuwa chini ya uongozi wa nani wakati wote wa ugonjwa hadi kifo cha JPM?
Je!
Katiba inasema nini kuhusu hilo?
Kama Mabeyo anatuambia Makamu wa Rais wala waziri mkuu hawakuwa na taarifa hadi walipopigiwa simu ili kutaarifiwa juu ya kifo!

Ni kina nani walikuwa wakiratibu mambo hayo yote?
Je!
Serikali ilikuwa chini ya amri za jeshi?
Kuhusu Dokta Janabi na uwepo wake muda woote wa Magufuli akiugulia pale.Je ni nani hasa na alikuwa wapi daktari maalumu wa Marehemu Rais Magufuli?
Na ni nini ilikuwa uwajibikaji na uhusika wake kwenye tukio zima?

Msiwe mnakimbilia kutoa majibu mepesi kwenye mambo mazito kama haya bila kwanza kutanguliza tafakuri.

Na ndio maana nimeunganisha tukio la kifo cha kijana pekee wa Mabeyo kwenye ile ajali baada tu ya muda mfupi wa kifo cha JPM kupita na nikasema hiyo ndio Karma!

Magufuli alifariki akiwa peke yake bila hata mke wake kuitwa ili kuja kushuhudia saa za mwisho za mumewe!
Walikuwa wakiitana kina Mabeyo na kamati yao tu!
Khe!

Wabongo tunaujuaji mwingi Sana
Ukisikiliza Ile interview vizuri utaelewa kila kitu ulichouliza hapo

It's like ulitaka Hali ilivyochange Dr angepiga simu Kwa mke wake au angepiga simu Kwa makamu wa Rais?

Tofautisha Kati yako kifo na hali kubadilika
 
Hata sijachagua maswali ya kukujibu, ngoja niendelee...

- Nchi inakuwa chini ya uongozi wa VP, hili lipo kikatiba.

- Katiba inazungumzia pale Rais anapokuwa nje ya nchi, kwa shughuli za kikazi, ugonjwa au vinginevyo, Makamu wake ndie anashika hatamu. Au ulitaka Katiba iseme kitu kuhusu VP kutopewa taarifa za ugonjwa wa Hayati JPM?!

Nani kati yenu mwenye uhakika kama VP hakuwa anafahamu chochote kuhusu hali ya ugonjwa wa Hayati JPM, narudia tena zipo njia nyingine za mawasiliano kufikisha ujumbe kwa mhusika, wakati ambao Mabeyo hakuwepo, ndio maana nasisitiza mwenye jibu la mwisho kuhusu hili, ni Samia pekee.

Mabeyo kazungumzia aliyoyaona mwenyewe, mengine yaongelewe na wengine. Naamini hata PM nae akiulizwa kuhusu hili jambo atakuja na part yake tofauti ambayo Mabeyo hakuigusa, hivyo hivyo kwa VP na wengine.

- Suala la waratibu, hao mbona wanaonekana wazi, ukianza na Mabeyo mwenyewe kwa cheo chake, PM Majaliwa, waliokuwa eneo la tukio, na viongozi wengine serikalini inawezekana walishirikishwa kwa mbali, wasingeweza wote kujazana kwenye chumba cha mgonjwa.

- Uwepo wa Dr. Janabi eneo la tukio pia nimekwambia inaweza kuwa ni ushauri wake kitaalamu ndio uliohitajika eneo husika, kama hata Dr. binafsi wa Hayati Magufuli humfahamu mpaka unaniuliza ni nani hasa, mimi siwezi kukupa jibu kwasababu hata nami sikuwa namfahamu.

• Hapa nakushangaa, kama hukuwa ukimfahamu daktari wa Hayati Magufuli, kwanini ushangae kutokuwepo kwake?!

• Mtu ambaye hata hukuwa ukimfahamu, unaulizia vipi uwajibikaji wake?!

Hata kuhusu kifo cha kijana wa Mabeyo kwenye ajali { sikumbuki kilitokea wakati gani}, napo sioni cha kushangaza, hakuna karma pale; ni nani kati yetu asiyekufa? au wewe ndie hupanga nani afe lini? mimi sioni uzito wowote wa hoja zako.
Kwanza kabisa ni vigumu sana kumuondoa mobeyo kwenye swala kama hilo kumbuka Mobeyo ndo alikuwa mwenyekiti wa Ulinzi na usalama wa nchi..

Kwahyo DGIS na IGP hawawezi kufanya jambo bila kumshirikisha kwahyo hakuna taarifa yoyote ya Kwenda kwa mtu yyte ingeamriwa bila yeye kuamua
 
Rais anaposhindwa kutimiza majukumu yake Baraza la mawaziri hukaa Na hupekeka hoja kwa Jaji mkuu!
Wapi jaji mkuu Alitajwa, Wapi speaker alitajwa..

Katiba hujui mkuu Ungenyamaza tu usikaririshwe vitu vya kuongea
Hebu lete hicho kifungu cha Katiba hapa twende sawa. Unajua maana ya Rais anaposhindwa kutimiza majukumu yake kikatiba? unajua mpaka ithibitike hivyo huchukua muda gani?

- Jaji mkuu atajwe kama nani?

- Speaker atajwe kama nani?

Ikiwa Makamu wa Rais yupo!. Unaandika vitu usivyovijua ajabu unasema nimekaririshwa, na nani?!
 
Umenijibu kwa wepesi sana huku ukiwa na hoja ingine mfukoni!
Labda ungenijibu maswali muhimu kuliko haya uliyoamua kuyachagua kidogo ningekuelewa!

Je!
Nchi ilikuwa chini ya uongozi wa nani wakati wote wa ugonjwa hadi kifo cha JPM?
Je!
Katiba inasema nini kuhusu hilo?
Kama Mabeyo anatuambia Makamu wa Rais wala waziri mkuu hawakuwa na taarifa hadi walipopigiwa simu ili kutaarifiwa juu ya kifo!

Ni kina nani walikuwa wakiratibu mambo hayo yote?
Je!
Serikali ilikuwa chini ya amri za jeshi?
Kuhusu Dokta Janabi na uwepo wake muda woote wa Magufuli akiugulia pale.Je ni nani hasa na alikuwa wapi daktari maalumu wa Marehemu Rais Magufuli?
Na ni nini ilikuwa uwajibikaji na uhusika wake kwenye tukio zima?

Msiwe mnakimbilia kutoa majibu mepesi kwenye mambo mazito kama haya bila kwanza kutanguliza tafakuri.

Na ndio maana nimeunganisha tukio la kifo cha kijana pekee wa Mabeyo kwenye ile ajali baada tu ya muda mfupi wa kifo cha JPM kupita na nikasema hiyo ndio Karma!

Magufuli alifariki akiwa peke yake bila hata mke wake kuitwa ili kuja kushuhudia saa za mwisho za mumewe!
Walikuwa wakiitana kina Mabeyo na kamati yao tu!
Khe!
Kwahiyo Mungu aliangusha ndege kumlipiza CDf punguza HISIA ndugu.
We tangu lini nchi hii ikafuata katiba 100% mpk ulilie ifuatwe kipindi hiko?
Nchi za kiafrika asilimia 99 ni wasiri kwenye ugonjwa WA kiongozi iwe mdogo au mkubwa... Hata awe na miaka 129 bado watadanganya.
Mbona huulizi MKAPA aliumwa nini na yeye pia nadhani kama sijakosea alifia mzena.
Na huyo dk WA magufuli unayemtaja sana kuwa hakuwepo Jina lake ni NANI?
 
Kwanza kabisa ni vigumu sana kumuondoa mobeyo kwenye swala kama hilo kumbuka Mobeyo ndo alikuwa mwenyekiti wa Ulinzi na usalama wa nchi..

Kwahyo DGIS na IGP hawawezi kufanya jambo bila kumshirikisha kwahyo hakuna taarifa yoyote ya Kwenda kwa mtu yyte ingeamriwa bila yeye kuamua
Hamna popote nilipomuondoa Mabeyo kwenye andiko langu.
 
Hebu lete hicho kifungu cha Katiba hapa twende sawa.

- Jaji mkuu atajwe kama nani?

- Speaker atajwe kama nani?

Ikiwa Makamu wa Rais yupo!. Unaandika vitu usivyovijua ajabu unasema nimekaririshwa, na nani?!
Screenshot_20240318_084908_Adobe Acrobat.jpg

Kuna watu wametajwa hapo Jaji mkuu, Madaktri, na speaker bado una la kusema
 
View attachment 2938011

Kuna watu wametajwa hapo Jaji mkuu, Madaktri, na speaker bado una la kusema
Kumbe hata kutafsiri sheria hujui, unajua kusoma tu kama gazeti ndio maana unaniambia nami nikasome niwe kama wewe!.

Kifungu ulicho "bold" kinasema endapo Baraza la Mawaziri "litaona" kwamba Rais hawezi kutekeleza majukumu yake....

Sasa umewahi kujiuliza ni wakati gani Baraza la Mawaziri hutumia ili "kuona" kama Rais hawezi kutimiza majukumu yake ili limpe taarifa Jaji Mkuu?

Jiulize; kwa muda huo wa kati kabla Baraza la Mawaziri halijakutana baada ya "kuona"... nafasi ya uongozi wa nchi hukaimiwa na nani?

Jiulize tena; ni magonjwa yapi yanayomfanya Rais "aonekane" hawezi kutimiza majukumu yake na Baraza la Mawaziri? Je, ugonjwa wa Magufuli upo miongoni mwa hayo magonjwa tajwa?

Usisome sheria kama gazeti unaokota kifungu kimoja pekee kisha unakuja kunifundisha sheria!, kila kitu kimeainishwa kisheria, chambua na vifungu vingine vya Katiba ili ujue kwa undani jambo husika.
 
Halafu pale mzena Huwa hawachomoki pale!

Sijui Ile sehem ni Bermuda triangle!!?aiseh!!
Ukipelekwa mzena na wewe ninmzito basi andika urithi kabisaa!!
Pale hawapelekwi kupatiwa matibabu wapone. Pale unapelekwa kwenye your last days and they see no option. Na kwa mujibu wa mabeyo anasema pale si kila mtu anaweza kuingia maana yake kwa watanzania wanavyopenda ushilawadu na upaparazi ukifia muhimbili taarifa zitawafikia ndugu zako kupitia manesi na wauguzi wengine hata kabla ya taarifa rasmi kutolewa na wanao takiwa kufanya hivyo.

Wanapelekwa pale pengine wakiwa ni wafu ili kupisha protokali nyinginezo tu za kiserikali na unatangaziwa kuwa alifia mzena. End of story
 
Hatimae tumemsikia na kumshuhudia aliekuwa Chief of Defense Forces kupitia media na mtu ambae inaonekana ndie alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa siku zote Marehemu JPM akiwa anapigania uhai wake na hatimae kuondoka Duniani!

Lakini maelezo yake yameongeza sintofahamu zaidi kuliko alivyotarajia. Na kwa wengine hasa mimi binafsi,
Sasa nimeelewa maana ya "karma". Muda mfupi baadae mtoto wa kiume wa Mabeyo aliekuwa Pilot pale Coastal Aviation alianguka na ndege uwanja wa Seronera akiwa yeye na rubani mwanafunzi wa vitendo (trainee) na wote walifariki Dunia.

Hili kwa sasa sintaliongelea sana ila nimeliweka hapa ili kuonyesha ukuu wa Mungu na Malipo yake kwa wale anaotaka kuwapa majibu ya matendo yao wakiwa bado hai.

Na wakati mjadala ukiendelea kuhusu mambo kadhaa ya kisiasa kutoka na hotuba ya Mstaafu Mabeyo!
Sisi wengine tunajiuliza wwali muhimu: Ni kwa nini walituficha ugonjwa wa mpendwa Rais wetu JPM?
Tunajiuliza: Dk Janabi alikuwa pale muda wote akifanya nini ilhali yeye hakuwahi kuwa Daktari wa JPM, bali alikuwa ni Daktari wa familia ya Kikwete na pia swahiba ya JK?

Tunajiuliza ...ni kwa nini walikwenda kumficha pale Mzena badala ya kumpeleka kwenye hospitali nyingine yenye hadhi ikiwezekana hata nje ya nchi? Tunajiuliza. Kama waziri mkuu alituficha. Makamu wa Rais alituficha!
Ni nani au kikundi gani kilikuwa kinaratibu haya mambo?

Tunajiuliza: Kama Mkuu wa majeshi aliambiwa na JPM awali kwamba wamrudishe nyumbani akafie huko.Ni kwa nini aligoma kutimiza takwa la Marehemu? Na kwa nini hakuwashirikisha wengine ili wachukuwe maamuzi sahihi?

Je, Magufuli aliugua ugonjwa gani huo ambao madaktari walikaa pembeni wakimshuhudia akipigania uhai wake akiwa kama mateka? Anasema alipofariki wao wakuu wa vyombo ndio waliwajulisha viongozi kama PM, CS na baadae makamu wa rais, ena wote hawakuwepo eneo la tukio.

Hatuoni mahala makamo wa Rais, mwanasheria mkuu, Wala jaji mkuu au spika wakiwa na maamuzi yeyote. Kila kitu kilipangwa na jeshi. Huyu Mabeyo ameongea, iko siku na wengine wataanza kuongea. Damu ya mtu huwa haipotei bure.

Kama kuna jambo lilipangwa na kufanywa na kikundi fulani,kinyume na tulivyoamishwa sisi wananchi. Na kwa jinsi siku ya Jana ilivyopita bila hata serikali ya Saa100 kujishughulisha na lolote kuhusu kumbukumbu hii muhimu nchini.

Tutashuhudia taraatiiibu!

R.I.P Jemedari JPM!

Wameanza kuropoka huku!
Hahaaa pale mpuuzi mmoja anapo jiona analyst kumbe mweupee peeee kichwani sababu maswali yako yote ni mepesi kujibika kiwepesi tu
 
FB_IMG_1710724673676.jpg
 
Back
Top Bottom