Maswali 10 yanayoulizwa kwenye Usahili

RuwaIkunda

Senior Member
Nov 2, 2017
156
279
Kwa wale wanaotegemea kufanya usaili wa kazi Leo katika Taasisi na Makampuni mbalimbali, Hakikisha haya maswali una uelewa nayo, haya ndiyo yanakupa asilimia nyingi za kupata kazi;

10 classic questions asked during oral interview;

1. Tell me about yourself?
Hapa sisi hatutaki kujua kuhusu umezaliwa wapi na lini, umesomea nini na kuhusu maisha yako, Hapa waajiri wanataka kujua sifa ulizonazo ukihusianisha na nafasi unayoomba, yaan hapa stick kwenye Skills, Experience, Achievements, Performance na ueleze kwanini unafikiri utaleta mabadiliko.

2. Why do you want to work for us?
Hapa hawataki kujua kuhusu ubora wa kampuni/taasisi yao kwani wao wanaujua, hapa wanataka uoneshe ni jinsi gani unafikiri taaluma, na sifa ulizoeleza kwenye moja hapo juu zitaisaidia kampuni yao, ila pia uoneshe kwa nini unafikiri hayo utayoleta yatakunufaisha wewe pia

3. What are your strengths and weakness?
Hili ni swali la kinyume, kweye strengths zungumzia mengi uliyofanya na yakaleta mabadliko huko unakotoka, na weakness ueleze labda kwa nini ulifanya maamuzi magumu ya binafsi ambayo wengi hawakuelewa mpaka matokeo chanya na wakajifunza. Usielezee udhaifu ambao ni negative.

4. Give an example of where you were able to use leadership skills?
Hapa wanataka kusikia kwa nini na wapi unaweza kuchukua maamuzi magumu katika mazingira yasio rafiki kuongoza watu ambao hata kama hukuwa kiongozi ulikuwa unashika wengine mkono. Talk of not being a boss and not a leader, ukielezea matukio kadhaa ya viongozi mfano: nilisaidia kubadilisha mfumo wa malipo unaiopa hasara kampuni na tukaokoa...., Au niliongoza wenzangu kufanya kazi kwa wakati, kuokoa muda ja kuzuia overtimes zisizo lazima kwa kampuni, nilishiriki kuandaa mpango kazi uliopongezwa sana na kiongozi wangu kuhusu....

5. Where do you see yourself in five years?
Kwenye ajira miaka mitano ni mid term plan, hapa lazima uwaoneshe namna unavyoweza kushawishi viongozi wa taasisi hiyo hiyo ili uwe kwenye key decision makers ndani ya muda huo, hapa elezea utafanya nini in terms of strategies ukiunga na skills zako za kazi husika ili kuonesha management ikuamini kwa majukumu makubwa zaidi, hapa usioneshe kuwa unataka ukuze experience na kuwakimbia.

Ukiwa smart Kuna muda unaweza kubadilishiwa role hapo hapo kwenye interview kwa kupewa nafasi kubwa zaidi.

6. What is your greatest achievement?
Hapa wanataka kusikia zile tu zinazoshabihiana na kazi unayoomba, uwe makini sana waeleze uliwahi kufanya nini na usiishie tu hapo waeleze kuwa kwa haya nimeangalia structure/kazi ninayoomba itakuwa zinaleta impact ya moja kwa moja bila kupoteza muda.

7. Why should we hire you?
Hapa elezea mambo yanayohusiana na kazi unayoenda kufanya, onyesha unafikiri wapi kutakuwa na gap la kiutendaji na jinsi wewe unaweza kuziba hiyo gap? Usijifie kuwa wewe ni bora or so hapa wanataka kuona kama unajua taasisi yao angalau kdg, hivyo katika hili soma sana kuihusu hiyo taasisi kabla hujaenda kwenye usaili.

8. Are you a good team player?
Hapa wanajua jibu ni Yes, ila wanataka kusikia how it is Yes, waeleze zile skills zako na kama kuna ushahidi wa huko nyuma tumia We badala ya I, yaana elezea mlifanya nini na kwa niji unafikiri hata ukiikuta team iliyokatika itasaidia kuiunganisha kupitia skills zako za mawasiliano, coaching, listening more, bealiver of open door policy, collective efforts etc.

9. What are your salary expectations?
Swali la mtego, hapa lazima uoneshe kwanza unajua mshahara wao, ila pia ujue mshahara wa soko kwa kazi unayoomba na kisha usiende mbali sana au chini ya mshahara wao, yote yana madhara, ila ukiwa na sifa nzuri wao wanakuwa flexible kwa negotiation.

Katika hili jitahidi sana kusema kwa nini unafikiri mshahara sio kigezo kikubwa cha wewe kufanya nao kazi ila pia onesha majukumu yako kwanini yanafaa kulipwa vizuri, wakisema figure basi weka figure ambayo itawalazimisha kukuajiri na sio kukuacha, yaani iwe kwenye ile ambayo utakaa ukijilaumu keshokutwa.

Ila pia itegemee na kazi kuna kazi hazina negotiations

10. Do you have any question?
Usiende bila swali, na maswali yawe ya msingi hapa ujiandae kuijua kampuni na kisha uwe unauliza maswali yanayoihusu taasisi mfano:.

Nimeona performance yenu mwaka jana mlipata.... Hii ni chini ya soko ambalo lilikuwa na wastani wa.... Je kuna mipango yoyote ya kulinda au kufanya bora zaidi? Je, what are long term plans za taasisi na mnafikiri wapi naweza kusaidia kama sehemu yangu ya kujiandaa kua nanyi? Na maswali ya hivi yaana yale yanaonesha kuwa wewe unaelewa unachofanya na sio unaenda pale kupoteza muda na kulipwa mshahara.


HITIMISHO:
The list above and response are not exhaustive unaweza kuongeza au kupunguza chochote, ila ukifuatilia hata haya machahe yatakusaidia siku yoyote huko mbeleni.
 
Sema hapo kwa utumishi wanatoaga hilo la kwanza tu
Wewe unakumbuka hata mengine ambayo utumishi washakuulizaga kwenye oral interview ? Kama unayakumbuka yataje hapa mkuu pamoja na post uliyofanyiwa interview
 
Kuna usaili mwezi uliopita nilihudhuria sijakuta hata swali moja kati ya hayo ni mwendo wa mkando tu mpaka nikahis hawa jamaa hawataki watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom