Masikini alichomfanyia mkewe kilinifadhaisha

Jacaranda

Member
Oct 23, 2011
45
20
Watu husema unaweza kumfanya mwanamke kuwa malkia wa uingereza lakini kama hakupendi atakunyea tu bila kujali,hii yaweza kuwa kweli.Lakini niyoyashuhudia juzi yameniaminisha pia ukiwa na fedha unaweza kumnyea mwanamke na badala ya kuchukia akafurahi.Siku hiyo ilikuwa hivi

Mziki ulikuwa unapigwa kwa sauti ya taratibu ,watu waliendelea kuingia ukumbini.Nilipoingia ukumbini nilikaa nyuma ya wanandoa wenye umri wa makamo ambao kwa mtazamo wa nje tu ulionyesha kuwa wana fedha za kutupa.Wakati wakiwa wamekazia macho kwenye jukwaa ghafla akapita msichana moja mrembo sana ambaye alimtambua mwanandoa wa kiume akasimama na kusalimiana naye na kisha wakapiga stor mbili tatu kabla ya kuwaacha wanandoa hao.

Alipoondoka mke wa jamaa kwa sauti ya ukali akamuuliza “Huyo ni nani” Mume wake bila hata ya kumuangalia akajibu “ni nyumba ndogo yangu” Mkewe kusikia hivyo akakunja ndita kisha akamkunja shati mumewe na kumwambia kwa ukali”naomba taraka yangu sasa hivi” mumewe akatafakari kwa muda na kisha kwa sauti isiyo na hisia hata chembe akamjibu “Mke wangu naomba ufikirie vizuri.Si unajua maana ya taraka? Nikikupa taraka inamaanisha hutaendesha tena range,wala benzi,safari za Dubai,China na ulaya hautazipata tena na ina maana hautaishi tena kwenye nyumba za kifahari wala kufanya shoping Woolworth au ufaransa” Akaendelea “na kwa umbo lako hilo sidhani kama tena utapata mwanaume hata wa kukusimamisha ,tumia busara mke wangu” mkewe kwa kugundua ukweli akaliachia shati la mumewe akageuz uso wake stejini akaendelea kutazama show.

Baada ya muda akapita msichana mwingine mrembo pia akasimama na kumsalimia jamaa na kisha akaendelea na hamsini zake.Mkewe akamuuliza tena jamaa “na huyo ni nani?” Jamaa akamjibu kwa pozi lilelie “hiyo ni nyumba ndogo ya rafiki yangu Fred” mkewe akamjibu kwa heshima kubwa ambayo ilinishtua mimi “,’Mhhh huyu wala siyo mzuri kama nyumba ndogo yetu’ ”
 
anajua upande gani wa mkate una siagi

Watu husema unaweza
kumfanya mwanamke kuwa malkia wa uingereza lakini kama hakupendi
atakunyea tu bila kujali,hii yaweza kuwa kweli.Lakini niyoyashuhudia
juzi yameniaminisha pia ukiwa na fedha unaweza kumnyea mwanamke na
badala ya kuchukia akafurahi.Siku hiyo ilikuwa hivi

Mziki ulikuwa unapigwa kwa sauti ya taratibu ,watu waliendelea kuingia
ukumbini.Nilipoingia ukumbini nilikaa nyuma ya wanandoa wenye umri wa
makamo ambao kwa mtazamo wa nje tu ulionyesha kuwa wana fedha za
kutupa.Wakati wakiwa wamekazia macho kwenye jukwaa ghafla akapita
msichana moja mrembo sana ambaye alimtambua mwanandoa wa kiume akasimama
na kusalimiana naye na kisha wakapiga stor mbili tatu kabla ya kuwaacha
wanandoa hao.

Alipoondoka mke wa jamaa kwa sauti ya ukali akamuuliza “Huyo ni nani”
Mume wake bila hata ya kumuangalia akajibu “ni nyumba ndogo yangu” Mkewe
kusikia hivyo akakunja ndita kisha akamkunja shati mumewe na kumwambia
kwa ukali”naomba taraka yangu sasa hivi” mumewe akatafakari kwa muda na
kisha kwa sauti isiyo na hisia hata chembe akamjibu “Mke wangu naomba
ufikirie vizuri.Si unajua maana ya taraka? Nikikupa taraka inamaanisha
hutaendesha tena range,wala benzi,safari za Dubai,China na ulaya
hautazipata tena na ina maana hautaishi tena kwenye nyumba za kifahari
wala kufanya shoping Woolworth au ufaransa” Akaendelea “na kwa umbo lako
hilo sidhani kama tena utapata mwanaume hata wa kukusimamisha ,tumia
busara mke wangu” mkewe kwa kugundua ukweli akaliachia shati la mumewe
akageuz uso wake stejini akaendelea kutazama show.

Baada ya muda akapita msichana mwingine mrembo pia akasimama na
kumsalimia jamaa na kisha akaendelea na hamsini zake.Mkewe akamuuliza
tena jamaa “na huyo ni nani?” Jamaa akamjibu kwa pozi lilelie “hiyo ni
nyumba ndogo ya rafiki yangu Fred” mkewe akamjibu kwa heshima kubwa
ambayo ilinishtua mimi “,’Mhhh huyu wala siyo mzuri kama nyumba ndogo
yetu’ ”
 
unajua sanyingine dawa la jamaa kicheche ni kujitoa ufaham kama alivyomjibu bibie alipoonyeshwa nyumba ndogo ya shemej tho athari ni kubwa..wanaume wenye hela ni utumwa sana..hiyo inaonyesha bibie shida zake zitamfanya avumilie.kwakuwa amekubaliana na hilo akaendelee kupangwa tu..Na pia nimempenda sana huyo mume kwa kuwa mkweli,ningekuwa mimi ningemsaidia kumnunulia mabox ya kondom tu.
 
Umeniboa hujui kuandika kiswahili.......... Otherwise hadithi yako ni nzuri. Amekusimulia nani hadithi hii?
 
kwanini unakuwa muongo? Lini ulienda harusin ukakaa nyuma ya hao wanandoa? Hii ni stor ya ku2ngwa mara ya kwanza nlisimuliwa 2007 wakat nko form six then nkaisikia tena 2009 nko 2nd year..ACHA IZO PELEKA KWENYE GOSSIP..OVYOO.
 
Back
Top Bottom