Masharti ya kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM)

Ukitaka kujiunga na CCM, njia rahisi ni kufika katika ofisi zao. Kama hujui ziliko nenda hata kwa kiongozi wa nyumba kumi (balozi) Au hudhuria mikutano yao kwani siku hizi huwa wanatembea na kadi zao.Kwa elimu uliyo nayo naamini hayo ulitakiwa uwe unayajua. Kwani yale matatizo ya elimu ya msingi na sekondari yameingia na vyuoni mara hii?

Faida:

1. Utafaidi sana but just for now, kwani kile ni chama cha wala rushwa na mafisadi, you just need to know what buttons to press. You do it right,umeula. Ila nikutahadharishe kuwa kila utakachokula ni mali ya wananchi wengine waliodhulumiwa sehemu, aidha kwa mafungu ya huduma za jamii yaliyopigishwa chenga, kwa ushuru na kodi zilizokwepwa, au kwa maliasili kama Madini na meno ya tembo. Pia if hazijaibiwa huenda zikatoka kwenye miradi haramu kama ya madawa ya kulevya.

Angalizo: Wakati unaanza kula kaa ukijua kuwa mwisho wa CCM unakaribia, na baada ya wananchi kujichukulia nchi yao tutapenda wote walioshiriki hujuma washughulikiwe. Itakuwa mbaya kuwa utafaidi kwa muda mfupi tu kuliko wenzio waliokutangulia.


Hasara:

Hasara pekee ni kupoteza uhuru, kwani kwa sasa wananchi wote wanaungana pamoja kutafuta jinsi ya kumtoa nyoka huyo (CCM) nchini. Kwa hiyo kwa sasa hata kama utatokea kupata pa kulia (ingawa kwa ulivyoshindwa hata namna ya kujiunga, pamoja na elimu yako, ni wazi hutaona myanya ya kula) bado hutakaa kwa amani.

Pia in fase two (baada ya uhuru) kutafuata kipindi cha kuwajibishana na kushughlikiana. Sasa hapo utajikuta unakabiliana na sheria na sidhani kama (kwa ulivyoshindwa mambo madogo madogo) utaweza hata kujificha! Wenzio walioanza mapema tayari walishaiba vya kutosha, na wameshajilimbikizia mali na fedha walizoficha Uswisi na kwenye mabenki mengine ya nje! Wakati ukifika,wao watatoroka na kuomba hifadhi za kisiasa. Wewe mpaka wakati huo sidhani kama utakuwa na nauli hata ya kusafiria. Kwa hiyo itabidi usubiri kushughulikiwa tu. What I am saying here ni kuwa, umeamua kujiunga na CCM in a wrong time.

Ushauri: Kwa nionavyo mimi kujiunga kwako na CCM kwa wakati huu, kuna hasara kubwa zaidi kuliko faida. Kwa hiyo nashauri uchague wisely. Unless you have a death wish, you can't consider joining CCM, at least not at these times. And I am sorry that I can't tell you where to go. If you consider not joining CCM you gonna have to do your homework better.

Sijui kama hii itakuwa imekusaidia.

Ushauri nimeupokea. Asante. Ushauri umekaa kitaluma kidogo.
 
Kama nilivyosema,nataka kujiunga na CCM, mimi nina elimu ya shahada na cheti cha taaluma. Sasa kabla sijajiunga naomba wana CCM mniambie
1. Je kuna faida gani ya kua mwanachama wa CCM.
2. Kadi naipata wapi ya uanachama.

Naomba mtu asijaribu kuhoji uamuzi wangu, Tuheshimiane.

Umesema una elimu ya shahada na cheti cha taaluma sio? kule wamejaa maprofesa e.g Prof. Maji Marefu.
 
picha p/size utazikuta hukohuko kwa mjumbe we nenda tu na ela sh.300.unachagua psize unayotaka ,ukitaka ya mzee wa gombe au mzee wa presha inapanda presha inashuka,zote utazikuta huko

We jamaa umenifurahisha sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa......
 
Kama nilivyosema,nataka kujiunga na CCM, mimi nina elimu ya shahada na cheti cha taaluma. Sasa kabla sijajiunga naomba wana CCM mniambie
1. Je kuna faida gani ya kua mwanachama wa CCM.
2. Kadi naipata wapi ya uanachama.

Naomba mtu asijaribu kuhoji uamuzi wangu, Tuheshimiane.

UPDATES

Toka juzi nilipoomba ushauri humu kuhusu nia yangu ya kujiunga CCM, wadau mmetoa michango yenu mingi na ushauri wenu. Elly B na wengine wote mlionishauri kutokujiunga na ccm nimepokea ushauri wenu mzuri, nimetafakari na kuamua kuachana na nia hiyo ovu iliyokua inanisukuma. Asanteni sana. Mungu awabariki wote.

Ushauri: Elly B elimu hiyo muwe mnaitoa hata huko kwa wananchi wengine isiwe humu jf tu. Waelimisheni ndugu na jamaa zetu ambao hawako humu,sambazeni elimu hiyo kwa wananchi.
The Unknown,

Nafurahi kusikia umepokea ushauri. Nashukuru pia kwa ushauri wako. Binafsi nafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuwashauri na kuwaelekeza wote. Na kwa sasa natia nguvu zaidi kwenye elimu kuhusu umuhimu wa kila mtu kujisajili kwenye daftari la kudumu, na kupiga kura. Nimekuwa nikikutana na watu waliokata tamaa kwa madai kuwa haina haja kupiga kura kwa sababu zitaibiwa, na wanayemtaka wao ndiyo atakuwa.

Ni vema wote wakaelewa kuwa kila kura katika mabadiliko ina maana. Kura moja inaweza kuweka tofauti ya nani anakuwa na nani hawi kiongozi. Na kama zoezi la usajili litasimamiwa vizuri, basi ni wazi hata myanya ya kuiba itakuwa imepunguzwa sana kwani itawalazimu wanaoiba waibe idadi ambayo ni chini ya idadi halali. Kwa msingi huo inapotokea kura zilizopigwa ni nyingi kuliko waliojiandikisha, kutakuwa na kila sababu ya kurudia kupiga kura. Now imagine kama watu wote waliojiandikisha watapiga!

Naomba mnisaidie kufanya kazi hii. Najua ni kazi kama ya hasara kwani haina malipo, na ukiangalia sana ni kama wanaofaidika ni wanaochaguliwa. Lakini ni wazi kuwa wanapochaguliwa viongozi wabovu kwa sababu tu hatukupiga kura na tukawapa nafasi ya kujaza kura za kuiba, tunaoumia ni wote, isipokuwa viongozi. Kwa hiyo hii ni kazi ambayo ni lazima tuifanye na tusipoifanya hakuna wa kuja kuifanya. Naamini mtaniunga mkono kwa hilo, wewe, wengine wanaosoma hapa na wengine mtakaowakuta mitaani. Waambieni kuwa wale wazee wasiojiweza na watoto wadogo na wagonjwa, na wenye ulemavu wanawategemea wao. Na siyo lazima kuweka majukwaa ya mikutano. Ukimwelekeza mmoja au wawili na hao unaowaelimisha ukiwaambia wafanye hivyo hivyo inatosha.

Asante.
 
Back
Top Bottom