Riwa
Platinum Member
- Oct 11, 2007
- 2,607
- 3,068
Hili jambo ni gumu kweli kwa pande zote. Upande mmoja matakwa ya mgonjwa yanastahili kuheshimiwa sababu imani yake haikubali kuongezwa damu. Upande mwingine daktari anawekwa katika muelekeo mgumu pale anapoona mgonjwa wake ambaye pengine hana fahamu yupo taabani sababu ya upungifu wa damu !!
Labda uongozi wa hospitali ungejaribu kuwaita na kuongea na kasisi na familia kujaribu kumshawishi mama kama inawezekana. Mwisho kama yote hayawezekani nadhani matakwa ya mgonjwa yaheshimiwe.
Percival...hapo penye red ndio sahau kabisa, Kasisi hawezi ruhusu hiyo hata kwa nini. Kanisa la Sabato limeingia gharama kutengeneza ID ambazo wasabato wanatembea nazo kwenye pochi na wallet zao zikiwa na sentensi 'USINIWEKEE DAMU'. Sasa Kasisi atahalalishaje muumini awekewe wakati huo ni msimamo wa kanisa! Kinachonishangaza ni wapi chimbuko la msimamo huo...Biblia? Mstari gani? Mbona kila jumapili tunakula mkate na divai kama kiwakilishi cha mwili na damu ya Yesu alipokufa kwa ajili yetu?!