Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
Mashahidi wa yehova(jehova's witnesses) ni kundi la kiimani kama yalivyo makundi mengine mfano waislamu, wakatoliki na waprotestanti.kundi hili ni maarufu katika suala la uongezwaji damu.kwa shahidi wa yehova,kuongezewa damu ni dhambi na hairuhusiwi(blood transfusion is prohibited among jehova witness members)
Hii ni imani kama zilivyo imani nyingine na kwa maoni yangu yafaa iheshimiwe. Hivi majuzi nilikuwa katika kituo kimoja cha afya(health facility) ambacho sitakitaja jina na kushuhudia mzozo mkali kati ya wahudumu wa afya daktari, nesi na mtoa dawa ya nusu kaputi wote hawa wakijaribu kumshawishi mama mjamzito kwamba kwa hali aliyonayo na kwa usalama wa maisha yake angehitajika kuongezewa damu wakati au mara baada ya operesheni ya kutoa mtoto. Mama huyu alikuwa shahidi wa yehova na alikataa kabisa na hatimaye alisaini maelezo nanukuu "ikitokea hali yoyote hata kama napoteza maisha nisiongezewe damu" hatimaye mama huyu aliingizwa kwenye chumba cha upasuaji na kufanikiwa kupata mtoto na yeye kutoka mzima ingawa hali yake ilikuwa si ya kuridhisha.
Hili jambo laweza kuonekana rahisi kuelezea lakini ni gumu kiutendaji kwani mama mjamzito anapofariki maelezo ya kifo chake lazima yafike wizara husika pia kwa namna moja au nyingine mhudumu wa afya huwajibishwa. Kwa upande mwingine mhudumu wa afya anaweza kushtakiwa iwapo ataenda kinyume na matakwa ya mteja(mgonjwa).
Kazi kwenu wanaJF mnaionaje imani hii haswa kwa mazingira yetu ya Tanzania? Nini kifanyike kuokoa maisha ya watu hawa?
Nawasilisha...