MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,224
- 22,305
Kwa mamlaka niliyojipa ninapiga marufuku tabia zifuatazo kwa mwaka 2024;
1. Kufungua threads za kuwasimanga single mothers.
2. Kukopa ovyo bila mpangilio na mwisho wa siku kujikuta kwenye matatizo yasiyo ya lazima. Waalimu wengi mzingatie sana hili.
3. Wanawake kuwapa kipaumbele viongozi wenu wa kiroho kuliko waume zenu. Huu upumbavu sitaki kuuona wala kusikia kwa 2024. Kama una baba wa kiroho acha mara moja.
4. Kwenda kula vinono migahawani huku nyumbani kwako wakishindia dagaa. Wanao na mke pia wanapenda zile chapati mbili na supu ya mbuzi. Hakikisha na wao wanakula unachokula wewe. Pumbav sana.
5. Kuishi kistaa mijini huku kijijini kwenu wazazi wakiwa wanaishi kifukara kwenye mbavu za mbwa. Unajisikiaje kuishi pazuri ukisukuma ndinga kali town huku familia yako ikiishi kifukara? Huu upumbavu mwishi ilikuwa 2023.
6. Kuendekeza mambo yasiyokuongezea thamani kwa mwaka mzima kama vile kufuatilia sana mechi za mpira. Fuatilia mambo ya burudani ila jiongezee thamani. Kama mhasibu huna CPA fanya uitafute mwaka huu. Wale wa IT kuna zile professional certifications pambaneni mzipate.
7. Wale mnaouza utu na kutojali maadili kisa pesa muache mara moja. Kibaya zaidi akijitokeza mtu kukemea na kukosoa upuuzi mnadhihaki kwa kumwambia "Acha makasiriko tafuta hela"... acheni kuabudu pesa kwa mwaka 2024.
Ongeza tabia nyingine unayoona haifai kuwepo kwa mwaka huu.