MARLAW mzee wa kiduku aachia website ya ukweli sana

Kwa kweli web yake si mbaya ila katika wasanii mi naona T.I.D ndio alikua na web kali sana ila sina hakika km mpaka leo iko hewani
 
I Love this guy
Is He Single mmmhh????

The website is awesome
.....:first::second::third:
 
AD pole mwaya,
Yaani kijana kaoa juzi juzi tu jaman

Hahahhaha labda mpango wa kando kama tayari.

Jamani umeniumiza moyo sana..
acha nikajifungie chumbani nilie

Hongera yake lakini kwa kumpata kimwana
Keep up man... I think you are brilliant...
Number one fan ....
 
ameitahidi ila kwa style yake ya kula vya haramu waziwazi itakuja kumharibia hata kama anafanyia njaa atafute namna maana ajue washabiki wake ni watanzania walalahoi........
 
Kunatofauti gani maraw kukodiwa na ccm kama sehemu ya kazi yake na marando kutetea mafisadi kama kazi yake?,
we hv long way to go kupambanua haya
 
Mimi pia aliniudhi kubadili wimbo wa pi pi kuingiza maneno ya CCM. Hata kama amekodiwa ule wimbo ulishapendwa na wapenzi ambao wengine si CCM wala CHADEMA alinihudhi kwa kweli. Na si peke yake kuna na yule kaka kidumu nae wimbo wake bomba kaweka maneno ya siasa. Si wangetunga nyimbo mpya! Next time wajifunze kutotumia nyimbo zilizowapa chart kisiasa.
 
jamni mbona mnaleta mambo ya siasa na muziki, hebu tumpongezeni kijana wetu mtanzania Marlaw kwa hatua anazopiga deily, watanzania ni watu wenye wivu sana especially pale mtu anapofanikiwa.

zaidi hubaki kuponda tu, wenzetu wazungu mtu anapofanya kitu kizuri hutuzwa na kusifiwa na pia watu wengi huongezeka kumpa sapot ili hiyo kitu alichokifanya kizidi kuwa juu zaidi.

hapa ilikuwa inaongelewa juu ya marlaw kuachia website nzuri na inayovutia sana ambayo imetengeneza na watanzania, mimi niliona ni muhimu sana kulisifia hili swala la kuwa na website.

faida za website ni kama sasa watu toka duniani kote wasiomjua marlaw sasa wanaweza mfahamu na kusikilaza muziki wake hii itapelekea jamaa kupata show za kimataifa hivyo kuja kuwa mwanamziki maarufu duniani.

faida nyingine ni kama watu walioko mikoani, kama mimi, ni vigumu sana kupata nyimbo, habari n.k kutoka kwa wasaniii mfano nimesikia wimbo mpaya wa marlaw kwenye redio inakuwa ngumu mimi kuupata mpaka nisubiri albamu itoke au nisubiri upigwe redioni.

sasa kijana marlaw ameturahisishia sisi watu wa mikoani kupata nyimbo zake tena bure na kuangalia video hata kwenye simu,

jamani hamuoni kama ni maendeleo hayo?? pia kupitia website yake tunaweza kuwasiliana nae, na jamaa kweli hujibu messege zote tunazomtumia iwe kwa email, facebook au kupitia form ya mawasiliano kwenye website yake.

swala la siasa ile ni biashara jamani kama wanavyofanya wasanii wengine, mfano kwenye uchaguzi wa marekani 50cent alimpigia kampeni mpinzani wa obama.

hata hapa bongo hao ccm walikuwa ni wateja wa marlaw katika biashara yake ya muziki,
Narudia tena, mfano wewe ni mfanya biashara wa sukari na vitu vya dukani, je akija mtu aliyevaa jezi za kijani na njano ambaye ni mwana ccm piwa na anaipenda toka moyoni na wewe hukipendi hicho chama je utaacha kumuuzia bidhaa??

hebu tuamke watanzania wenzangu, tusiendekeze siasa kwenye mambo ya maendeleo kama haya, japokuwa siipendi ccm ila kwenye ukweli tuwe wakweli,

mimi mwenyewe ni chadema damu damu, na ninaupenda sana muziki wa marlaw, kwasabu napenda maendeleo marlaw alipowaimbia ccm haikuniuma bcoz niliamini alikuwa anafanya bishara tu,

hata chadema au cuf wangemuwahi na kuongea nae kibishara basi naamini marlaw angewaimbia tu.


sasa tuache kuingiza siasa, wanasiasa wa ki africa hawana uzalendo na nchi bali miili yao na familia zao tu.

website ya marlaw ni www.marlawmusic.com

hongera sana marlaw hope wasanii wengine watafuta nyayo zako.
 
Dogo is talented, super skilled na sauti yake na kama anaweza basi apige mzigo zaidi na zaidi, ushauri wangu ni kwamba nchi yetu sasa inapita mpito mbaya sana, si kama marekani au UK, ni Tanzania, awe mwangalifu si kila mteja utamuuzia bunduki!!! Aliuza bunduki wka jambazi, jambazi anaitumia sasa, ACHAGUE WATEJA!!! HATA MALAYA WA OHIO WANACHAGUA WATEJA!!!!!

Namtakia kila la kheri na maisha ya ndoa na kazi zijazo, ila namuonya awe makini sana kuchagua associates na pia asifanye biashara inaweza kumtenganisha na vijana wa leo wa tanzania (siasa), vijana ndio wateja wake wakuu na si chama cha siasa, kwani kampeni ni mara moja katika kila miaka mitano wakati disco ni kila siku kasoro jumatatu

All the best Marlaw
 
mimi mwenyewe ni chadema damu damu, na ninaupenda sana muziki wa marlaw, kwasabu napenda maendeleo marlaw alipowaimbia ccm haikuniuma bcoz niliamini alikuwa anafanya bishara tu,

hata chadema au cuf wangemuwahi na kuongea nae kibishara basi naamini marlaw angewaimbia tu.

sasa tuache kuingiza siasa, wanasiasa wa ki africa hawana uzalendo na nchi bali miili yao na familia zao tu.
hakuwa na haja ya kuimbia chadema, kafu wala ccm, yeye ndiye aliyeleta siasa........... WEREVU WALING'AMUA!!!
 
Jamani umeniumiza moyo sana..
acha nikajifungie chumbani nilie

Hongera yake lakini kwa kumpata kimwana
Keep up man... I think you are brilliant...
Number one fan ....

Hebu tuwekee nyimbo zake za hivi karibuni please.
 
Mimi pia aliniudhi kubadili wimbo wa pi pi kuingiza maneno ya CCM. Hata kama amekodiwa ule wimbo ulishapendwa na wapenzi ambao wengine si CCM wala CHADEMA alinihudhi kwa kweli. Na si peke yake kuna na yule kaka kidumu nae wimbo wake bomba kaweka maneno ya siasa. Si wangetunga nyimbo mpya! Next time wajifunze kutotumia nyimbo zilizowapa chart kisiasa.

Usishangae mwaka huu wa uchaguzi,nitampata wapi na kitorondo ya diamond ikaja na version ya ccm
 
Back
Top Bottom