Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,551
- 11,607
Mpaka jana (tarehe 23 Oktoba) raisi Joe Biden wa Marekani ameendelea na msimamo wake kwamba hataki mashambulizi ya Israel yasimamishwe huku madhambulizi hayo yakizidi kuongezeka na kuzidi kuuwa watu.
======
Upande wa jeshi la Israel kumeonekana kuwepo kwa msuguano mkubwa baina ya waziri mkuu,Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi uliopelekea hapo jana kujitokeza kwa pamoja kukanusha habari hizo.Waziri wa ulinzi,Gallant amehimiza jeshi liingie Gaza kwa haraka kwani vijana wameanza kuchoka kusubiri na hamasa zao zimeanza kupomoroka.Waziri mkuu kwa mbinu zake za kivita anasema kuingia Gaza kutafungua lango jengine la mapigano upande wa kaskazini kutoka kwa Hizbulah.
======
'Then we can talk': Biden says no ceasefire in Israel-Hamas war until hostages released
Kwa upande wao nchi za kiarabu kwa sauti moja zimesema hakuna kuhama kwa wapalestina kutoka ardhi zao.Wamekumbusha kuwa tayari kuna maazimio ya kuundwa kwa taifa la wapalestina.Hilo taifa litaundwa na nani na wapi kama wapalestina watahamishwa kutoka ardhi zao.Arab states say Palestinians must stay on their land as war escalates
Hayo yakitokea wapalestina waliowahi kutiii agizo la kuhama maeneo ya kaskazini ya Gaza ili kwenda kusini wameamua kurudi walikotoka wakitoa matamko kuwa ni bora kufa kuliko dhiki wanazozipata huko walikokwenda.Mashambulizi yamewafuata huko huko na wamejikuta wameishiwa na mahitaji yote.Kwa hali hiyo wameona warudi walikotoka ili kufukua visima vya maji japo yenye chumvi wanavyovikumbuka .Upande wa jeshi la Israel kumeonekana kuwepo kwa msuguano mkubwa baina ya waziri mkuu,Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi uliopelekea hapo jana kujitokeza kwa pamoja kukanusha habari hizo.Waziri wa ulinzi,Gallant amehimiza jeshi liingie Gaza kwa haraka kwani vijana wameanza kuchoka kusubiri na hamasa zao zimeanza kupomoroka.Waziri mkuu kwa mbinu zake za kivita anasema kuingia Gaza kutafungua lango jengine la mapigano upande wa kaskazini kutoka kwa Hizbulah.