Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Viongozi wawili wakubwa wa Hamas wamezipuuza jjuhudi za Marekani kuhusu Gaza kama ni diplomasia ya askirimu.
Basem Naim akiwa nchini Uturuki ameyapuuza matamshi ya raisi Biden aliyotoa juzi wakati akila askirimu aliposema makubaliano baina ya Hamas na Israel yanatarajiwa kufikiwa ifikapo Jumatatu ijayo.
Kiongozi huyo alisema Marekani haina nia safi na wapalestina kwani wakati wakisema hayo ndio wao wanaopiga kura ya veto Umoja wa mataifa kupinga kusitishwa kwa vita.
Wakiyasema hayo wao pia ndio walioidhinisha dola bilioni 14 kama msaada kwa Israel na hawajasita kupeleka shehena za misaada ya silaha kwa Israel.
Kwa upande wake Ismail Haniyeh amezungumza akiwa Beirut nchini Lebanon,kuwa ni jukumu la nchi za kiarabu kuzuia vifo vya wapalestina kwa njaa kutokana na kuzuiwa kwa makusudi kufikishwa chakula kwenye maeneo ya Gaza.
Haniyeh akaongeza kwa kusema kuwa japo watu wake wanapenda suluhu ili vita viishe lakini kama madai yao ya msingi yasiposikilizwa basi bado wana uwezo wa kuendelea kupigana na Israel.
Miongoni mwa madai yao ambayo hayawezi kubadilika katika makubaliano yoyote yale na Israel ni pamoja na kusitishwa kwa vita na kuondoshwa vikosi vya Israel kutoka Gaza moja kwa moja.