Marekani kupewa Kigamboni

[QUOTE=Dar Es Salaam;Loliondo iko wapi? Uarabuni? wamepewa kivipi? au wamewekeza na wanalipia kodi zote zinazohusu uwekezaji? hebu fafanuwa.

Hakuna uwekezaji hapo kuna uwezekaji. Hao Arabs wanatumia ardhi ya vijiji bila kua na makubaliano (kwa njia ya mikataba) na serikali za vijiji. Kuna uwekezaji hapo au dhuluma? Sasa watalipiaje kodi ilhali hawana mikataba na vijiji husika?! Serikali kuu ndo inahusika katika uporaji wa ardhi ya Loliondo kwani imeingilia ardhi ya vijiji kwa mabavu na kuwapa waarabu!
 
Hivi mnafikili Mmarekani hana akili kuwekeza huko? Au je viongozi wetu ndio hamnazo? Wote wanaakili sana.

Kwa nini Clinton alikwenda kutembelea kusini mwa Tz akafungua na hospitali kule? Kwa nini Busha alikuja Bongo enh. Hivi hamjui kuwa Tz ina Uranium tena nyingi kuizidi Marekani? Marekani wanatoa tani 165 kwa mwaka sisi ile sehemu ndogo tu tuliyoifanyia utafiti tutatoa tani 168 kwa mwaka, na bado ziko sehemu nyinyine zinazofanana na hiyo ikiwemo pembezoni tu na hapo itakapoanza kuchimbwa hiyo. Hivi nyie hamjui hayo au?

Kalaghabaho na ubwezi wako!!
 
Marekani hana msaada wowote ktk africa!maradhi ya ukimwi kaleta yeye,vita zote duniani yumo!bora angepewa japan anatusaidia sana miradi mbalimbali ya maendeleo
 
QUOTE=BONGOLALA;Marekani hana msaada wowote ktk africa!maradhi ya ukimwi kaleta yeye,vita zote duniani yumo!bora angepewa japan anatusaidia sana miradi mbalimbali ya maendeleo

Kweli Bongolala. Na utaendelea kubongolala mpaka unakufa. Yani unaona heri uendelee kupewa misaada tu!? Badala ya kujitafutia mbinu za kujisaidia wewe unataka misaada tu. Huna tofauti na mkwere anaeenda kuhemea huko anakokuita kwa WAKUBWA!
 
Hivi ni kweli Wamarekani wamezawadiwa eneo la kigamboni in exchange na ujenzi wa Daraja?
Swali langu: Hivi iwapo watajenga hilo daraja, litakuwa ni kwa faida ya waTanzania au wa Marekani watakaokuwa ndio wakazi? Je, iwapo hao waMarekani watajenga, je wakazi waTanzania wataendelea kuvumiliwa nao kwenye majengo yao hafifu au watahamishwa?
Nawakilisha

Taarifa hizi inaelekea ni za kweli ingawa haijawekwa wazi na serikali yetu.Inasemekana ujio wa Bush junior wakati ule hiyo ndiyo iliyokuwa agenda yake kubwa kabisa.Wamarekani wanataka kuweka kituo kikubwa kabisa cha kijeshi(Africom-African command) Kigamboni.Waliomba kukiweka Africa ya Magharibu lakini taarifa zilizopo ni kwamba huko wamekataliwa.
 
Too Bad.Daraja tunalitaka lakini Americans usually come with alot of demands. sasa wanaanza vita na Wachina via proxy-tanzania. itakuwa kama enzi za cold war na urusi,
tanzania ikaamua kuingia ktk nchi zisifungamana na upande wowote(wakubwa wa umri watakumbuka hili)kulikuwa na utitiri wa scholarships to russia,ukrain,chekslovakia na bulgaria plus cuba.
sasa Jay Kei ameamua kukumbatia Marekani wakati wachina wanatoa misaada ya elimu plus afya etc undumikuwili usijetutokea puani
 
Hivi ni kweli Wamarekani wamezawadiwa eneo la kigamboni in exchange na ujenzi wa Daraja?
Swali langu: Hivi iwapo watajenga hilo daraja, litakuwa ni kwa faida ya waTanzania au wa Marekani watakaokuwa ndio wakazi? Je, iwapo hao waMarekani watajenga, je wakazi waTanzania wataendelea kuvumiliwa nao kwenye majengo yao hafifu au watahamishwa?
Nawakilisha

Tembelea tovuti ya wizara ya ardhi utapata ukweli kuhusu suala hilo. Si Kama unavyoeleza au kuelezwa. Sometimes it is a good idea to do some homework before starting a topic or contributing to one! Wataaluma husema NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK, Nadhani msemo hue unatufaa wengi JF!!. THANKS ANYWAY FOR THE POST!!
 
Kama ni mkataba wa uendelezaji (development) utakuwa na walakini kwani sheria ya nchi ya "public private partnership (PPP)" haijapitishwa na bunge. Mwisho wake wengi tunauelewa ni kwenda mahakama ya kimataifa ya usuluhishi ambapo serikali inabambikizwa mabilioni ya fidia. Tatizo la nchi letu ni kwamba mfumo (system) na muundo (Structure) wa utawala umeshindwa. Kwa bahati mbaya, wengi (80%) hawako tayari kuufumua na kuuunda upya.
 
Uwekezaji gani anafanya yule mwana mfalme kule Loliondo? Kuchukua wanyama wetu na kuwapeleka Uarabuni kunaitwa kuwekeza?
Kuwapiga marufuku Wamasai wetu katika maeneo waliyokuwa wanatumia ulishaji mifugo ni uwekezaji?

Waarabu wa Loliondo wamewekeza kama walivyowekeza wazungu na hata zaidi yao hapo Loliondo. Kuna makampuni mengi yenye vitalu vya kuwinda Tanzania ambayo hata maji wameshindwa kuwapatia wananchi wanaozunguka vitalu vyao. Waarabu wamechimba visima vya bure kwa wananchi, wamejenga shule, wamejenga hospitali za bure mpaka madaktari na dawa wanatoa bure. Nioneshe mwingine mwenye vitalu sio kitalu kama hawa waarabu, aliwekeza namna hiyo kwa wananchi.

Wanyama hawajachukuliwa kama usemavyo! Wamenunuliwa kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa. Na si hawa Waarabu tu wenye kununuwa wanyama hai kutoka Tanzania.
Ikiwa waliokuwa jamii za waliokuwa wakiishi hapo kabla loliondo haijafanywa kitalu cha kuwindia, bado wapo, walioamuwa kuondoka walilipwa. Wenye asili na waliokutwa wamesajiliwa, wameajiriwa, wamejengewa na wanaendelea kufaidika kwa kupewa huduma zote za bure. Hao waliofurushwa ni wavamizi wa kutaka kujiweka sehemu si yao na ni wenyeji wenyewe wa pale ndio waliowafukuza. Kampuni ya waarabu inayo endesha shughuli za uwindaji pale haihusiki na wanaovamia maeneo na wanaowafukuza.

Jee unajuwa Tanzania ina kampuni ngapi za nje zinazomiliki vitalu vya kuwindia zaidi ya hawa waarabu wenye kitalu hiki kimoja tu?

Wacha ubaguzi wa kikabila na kidini. Ukiongelea wenye vitalu vya kuwinda ongelea wote na usi pin point kwa hawa waarabu tu.
 
na wale Wamasai waliochomewa nyumba zao walikuwa wavamizi kutoka wapi? Haya ya kuchimbiwa visima si ndiyo hiyo hiyo mentality ya kudumisha dependency kuwa Watanzania hatuwezi lakini wageni. ie Waarabu na Wazungu ndio wanaoweza. Shule hatuna uwezo wa kujenga? Huu ni uwekezaji ninaoupinga na haihusiani kabisa na ukabila au udini. Sikubaliani na mwekezaji wa Grumeti, Tudor, ambaye amefukuza ndugu zangu waliokuwa wanawinda na kulinda mifugo yao huko. Sikubaliani na sera yetu kuhusu vitalu kupewa wageni wawe wazungu, wachina, au waarabu. And this has nothing to do with ukabila na udini. Tanzania hatuhitaji this kind of uwekezaji. Ni unyonyaji.
 
Kunawatu wanasema wape japan bila ya kujua dunia inavyoenda.

1. Hiyo project ni ya development kama ilivyo mlimani city tu ingawa yenyewe kubwa hivyo marekani hajapewa chochote bali ni investors kama wengine.
2. Marekani ni powerful kwa mambo mengi lakini jambo mojawapo ni kwamba wana control Japan, S. Korea na German. Hivyo hao wanaosema Marekani haipo Tanzania hawajui kwani Japan na marekani ni kitu kimoja!!. Kambi zote za kijeshi za Japan, S.Korea na German ni za Marekani! S.Korean peke yake kuna wanajeshi wa kimarekani 50,000!!! Japan na German kuna wanajeshi kibao je wanafanya nini sehemu zote hizo!. Kitu kikubwa ni kwamba sehemu zote hizo zina maendeleo makubwa sana.
 
Jamani hebu kama kuna wenye taarifa zaidi kuhusu hii atusaidie. Waswahili walisema LISEMWALO LIPO KAMA HALIPO LAJA.
 
Back
Top Bottom