Mara: Kijana aliyejeruhiwa kwa mishale katika mgogoro wa ardhi Bunda afariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
UPDATE: Aliyefariki ni Isore Mtegetu Marwa (28) Mkazi wa Mekomariro Wilaya ya #Bunda alijeruhiwa wakati wa vurugu zilizohusisha baadhi ya Wakazi wa Mekomariro dhidi ya Wananchi wa Kijiji cha Ryaming’orori Wilayani Serengeti ambapo pia watu wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salum Morcase akizungumza na JamiiForums amesema “Kweli amefariki katika Hospitali ya Bugando (Mwanza) alipokuwa amelazwa, uchunguzi wa daktari unafanyika kisha ndugu watakabidhiwa mwili, baada ya hapo Jeshi la Polisi linaendelea na ukamataji, kwa sasa hali ni shwari eneo la tukio na Polisi wanaendelea kuimarisha ulinzi.”

Awali, akielezea kuhusu mgogoro huo, Kamanda amesema ni wa muda mrefu, pia kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Isoreni kuwa marehemu ameacha mke na Watoto wawili

===

Habari ya vurugu hii hapa: Wakazi wa Wilaya ya Bunda na Wilaya ya Serengeti wadaiwa kuchomana mishale katika mgogoro wa ardhi
 
Back
Top Bottom