Wakazi wa Wilaya ya Bunda na Wilaya ya Serengeti wadaiwa kuchomana mishale katika mgogoro wa ardhi

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Mimi ni Mkazi wa Kijiji cha Mekomariro Wilaya ya Bunda, naomba jamii ijue kuwa kuna ugomvi wa ardhi kati Wananchi wa Kijiji chetu na Wananchi wa Kijiji cha Wilaya ya Serengeti, mpaka sasa kuna ugomvi mkubwa, watu wamechomana mishale.

Huu mgogoro hauwezi kumalizika kwa kuwa kuna viongozi au viongozi wapo nyuma ya kinachoendelea na wamekuwa wakifanya mambo kwa maslahi yao.

TAMKO LA POLISI
RPC Mara Salum Morcase amesema “Kinachoendelea ni amani, vurugu zimedhibitiwa, upande wa Mekomariro wamejeruhiwa watu watano, mmoja yupo hospitali, wengine wamepata majeraha madogo na walienda zahanati wakapata dawa wakarejea nyumbani, upande wa pili Kijiji cha Ryaming’orori aliyejeruhiwa ni mmoja tu naye alipata majeraha machache akarejea nyumbani.

“Vurugu zilitokea jana mchana (Septemba 17, 2013), mgogoro huo ni wa muda mrefu, kuna timu imeenda eneo la tukio kufuatilia na baadaye nitapata ripoti kamili.”
 
Mimi ni Mkazi wa Kijiji cha Mekomariro Wilaya ya Bunda, naomba jamii ijue kuwa kuna ugomvi wa ardhi kati Wananchi wa Kijiji chetu na Wananchi wa Kijiji cha Wilaya ya Serengeti, mpaka sasa kuna ugomvi mkubwa, watu wamechomana mishale.
Duuuh polisi watafika nadhani wanaona
 
Mimi ni Mkazi wa Kijiji cha Mekomariro Wilaya ya Bunda, naomba jamii ijue kuwa kuna ugomvi wa ardhi kati Wananchi wa Kijiji chetu na Wananchi wa Kijiji cha Wilaya ya Serengeti, mpaka sasa kuna ugomvi mkubwa, watu wamechomana mishale.
Kimeumana tayari
 
Mkuu kuna memba humu anasemaga yeye ni mwanakijiji wa kijiji kimojawapo wilaya ya Bunda mshirikishe huyu apaaze sauti yake aandike makala kuhusu kinacho endelea Bunda.

Anaitwa GENTAMYCINE
 
Huu mgogoro umedumu Kwa mda mrefu saana. Chanzo ni Mbunge wa msoma Vijijini Mathayo kajimilikisha zaidi ya hekari 2000. Na jamaa mmoja anaitwa Magambo Afsa TRA DAR. kajimilikisha eneo zaidi ya hekari 3000 za kijiji. Wanamtandao na viongozi wa selikali. Kila mwaka watu wanagombana na kuumizana mkuu wa mkoa anasema anaunda tume. Mwaka huu mwezi wa 6 mkuu wa wilaya alimaliza huu mgogoro kw kuweka vigingi kutenganisha mipaka nakutoa agizo Kila kijiji kiheshimu mipaka ya mwenzie. Ila baado wanaichi wa kutoka kijiji Cha Ryming'orori wakavuka mipaka na kuvamia mashamba ya wenzao.
 
Pole sana ndugu yangu, ugomvi kama huu uliwahi kusumbua sana kipindi hicho ndani ya wilaya ya Tarime, hasa Tarime vijijini kati ya Nyamongo na Nyakunguru, Nyamongo (Matongo) na Mwara, Kebweye na Kyoruba/Bukira, Mrito (Nyamongo) na Gibaso/Bwirege na upande wa Rorya huku.
Huu ugomvi huanza kwa chuki za ardhi ila baadae huhamia kwenye wizi wa ng'ombe ambao husababisha umasikini kwa jamii husika na mara nyingi huchochewa na viongozi wa wilaya ambao hushindwa wasimame wapi ili kulinda soko lao la kura kipindi cha uchaguzi
 
Back
Top Bottom