Mapishi ya mtori...

Mi sijui utafanyaje ila nataka nione uji uji pale... Halafu tangu nimekua mkubwa siyatumii tena nilinenepa shingo kama kenge yani .. ukitaka nenepa ghafla cheza nayo hayo
Na issue zetu zile ukakubaliaje kunenepeana? 🤣🤣 hii chai tajiri, sijainywa…

Mezani utapatana na mtori wa Kaskazini.. sio hiyo mitari wanablend watoto wa Dar wavivu wavivu..
 
Watu wanarahisisha mpaka visivyorahisishika… heri hata utumie chopper ya mkono, kuliko kublend kisamvu/ mtori 😂😂 vinatoka viko rojoooo bayaa
Vinakaa kama uji wa mtori au uji wa kisamvu,, hizi pipo ni vivu sijawahi ona nakwambia
 
Ladha ipo? Mie naona fresh tu labda walizidisha supu/maji....

Mtori wa kupekecha huo je usafi umezingatiwa?

Mwanzoni hata juice ya chungwa ilikuwa ni ya kukamua.. sahiv kuna simplified tools za kuchuja juice.. same as kwa juice ya carrots.

Naprefer mtori wa blender. Hata nyama inasagika vzr.
 
Na issue zetu zile ukakubaliaje kunenepeana? 🤣🤣 hii chai tajiri, sijainywa…

Mezani utapatana na mtori wa Kaskazini.. sio hiyo mitari wanablend watoto wa Dar wavivu wavivu..
Mmmh sasa si kabla ya.. eti umesema ni chai? Tumbo ni lako ila utaona mzigoo.. umekua wa kaskazini sasa kuwananga shemej wa daslama.
Ni chai bwana ghaiiii ..
Kama sio chai tutatesti kama week hivi tuone shingo ya kenge inavyokaa 😂😂🏃🏃

Karibu sana Northzone..
 
The boss usikariri maisha..
kwani mwanao akianza kula mtori ambao ndizi zipo blended akiwa mkubwa akaja kula mtori wa asili kabisa atasema ule wa asili hawajui kupika ndizi hazijasagwa vizuri..

nyakati na mazingira yanatubadilishia utamaduni wetu kila siku..
Hujui wanachopinga. Ni hivi: ukitumia blender hauwi mzuri. Hivyo basi, hata mtu aliyezoea kunywa ilitengenezwa kwa blender mpaka akiwa mkubwa. halafu akaja kunywa uliotumia njia ya asili, ataukubali ule uliotumia njia ya asili.
 
Kuna restaurant nimeingia nikaona wameandika kuna mtori ...dah...Ile kuagiza mtori si ndo nikagundua wana saga na blender ndizi zilizochemshwa wanachanganya na nyama ndo wanasema mtori ... nikashangaa Sana....mtori nilio Zoea ndizi zinachemshwa na nyama Hadi zinasagika zenyewe na haziwezi kuwa uji kabisa kama WA kusaga na blender....nahisi mtori Una makabila yake ...sio kila mtu anaweza pika mtori...

Wachaga na wahaya ndo wanajua kupika mtori...

Hebu wajuzi waweke tips hapa za upikqji mtori..
Kwanza kabisa ni kosa kubwa kusema wahaya wanajua kupika mtori. Ukirudia kusema tena hivyo unaweza kushtakiwa na kufungwa kifungo cha miaka 30. Mtori ni chakula cha asili ya wachaga. Ni chakula maalumu kwa wanawake waliojifungua mtoto, ile miezi mitatu ya kwanza. Kidogo kidogo umaarufu wake ukaanza kusambaa na sehemu nyingi Tanzania ukapata umaarufu. Mapishi yake: Kuna ndizi maalum za kupika mtori japo siku hizi watu wanatumia ndizi zisizo maalum. Unamenya ndizi, unazipasua vipande vidogo vidogo, kama chips halafu unazichemsha baada ya kuziosha. Unatia chumvi kiasi. (zamani walikuwa wanatumia vyungu kuchemsha ili ndizi ziive vizuri na kuwa na ladha nzuri). Kwenye sufuria nyingine, unachukuwa nyama nzuri (siyo kila nyama inafaa kupika mtori,) unaichemsha mpaka inaiva. Ikisha iva, unakata vipande vidogo vidogo, na kuweka pembeni. Ndizi zikishaiva, unaepua na kuanza ''kuzisonga'' kwa kutumia mwiko. Zikishapondeka, unaweka supu ya moto kutoka kwenye ile nyama, pamoja na vile vipande vya nyama huku ukipekecha na kipekecho maalum. Unatakiwa uwe fundi, usiweke supu nyingi sana wala usipunguze sana.
 
Iwe kutengenezwa kwa kusaga ndizi kwa blender, kipekecho, kinu au potato masher zote ni njia sawa tu...

Tulipokuwa shule tulifundishwa kuhusu mashine/nyenzo kwamba kuna simple machine na complex machine...

Kazi ya mashine ni kuifanya kazi iwe rahisi, kupunguza muda wa utendaji na kuongeza ufanisi, kwa habari ya kusaga chakula teknolojia imeleta nyenzo kama blender, choppers n.k...

Wapo wanaoponda mawe kwa nyundo (simple machine) kupata kokoto, na wapo wanaoponda mawe kwa crushers (complex machine) kupata kokoto...

Hivyo hata kwenye uandaji wa mtori ambapo moja ya process ni kusaga/kuponda ndizi, nyama au viazi si kitu cha ajabu kurahisisha hiyo kazi kwa kutumia mashine ambayo inaongeza ufanisi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom