Mapenzi yananitesa, naombeni ushauri

ukipanda mbegu tegemea kuona mbegu hiyo itaota so usishangae, pole sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.......................
 
halafu mariam katabia ka kupenda palipo pendwa ukiamini kuwa u may be a gud sample to replace and cover the religion gape btn two always kanakuaga just for short run because if huyo jamaa alikua na huyo binti by the time being it mins dat the man was still flirt to the gal na wewe ulikua unatumika kama kilaka tuu though u cmc to be more commited in luving em
 
MAPENZI YANANITESA NIPENI USHAURI

Nimefikiria kwa muda mrefu naona nazidi kupoteza muelekeo. Naombeni ushauri wenu wa mawazo naweza kufarijika kwani nipo njia panda. Ninampenzi ambaye kwa kiasi kikubwa ninampenda , mwanzao wa mapenzi yetu alinieleza kuwa anampenzi lakini hawawezi kuwa pamoja kwasababu ya imani ya dini zao hivyo uwezekano wakuishi pamoja hautaendelea kuwepo. Mimi nilikubali kwani nilikuwa tayari nimeshampenza sana.

Hivi sasa mimi nina mimba, na yeye ananiambia na yule aliyekuwa mpenzi wake pia ana mimba sikujali. Tatizo lilokuwepo kila siku ananilazimisha nikatoe mimba mimi nimemwambia sipo tayari kufanya hivyo kwani mimi nina kazi yangu nimemwambia sitamsumbua lakini haelewi anatafuta mpaka watu waje wanishauri nikatoe. Pia ananiambia hataweza kuwa na mm bora aendelee na mpenzi wake wa mwanzo. Naombeni ushauri nifanyaje kwani bado nampenda sana.

Miriam
Huyu bwana wala usijisumbue utapata kiharusi bure, hakutaki period. Kuhusu mimba ina muda gani? ningekuwa mimi kama iko chini ya miezi mitatu ningetoa na kuangalia maisha yangu. Ila kama we mwenyewe unataka kuzaa poa endelea.... nakuambia hivi kwani naamini hata kutoa mimba ni aina ya upangaji uzazi na asilimia kubwa ya wanawake wamefanya hivyo si chini ya mara mbili. Naona watu wanajidai, ooo zaaa shauri yako kulea si mchezo.. especially mtoto ambaye baba yake kamkataa. Huu ni ushauri wangu , changanya na zakwako!
 
MAPENZI YANANITESA NIPENI USHAURI

Nimefikiria kwa muda mrefu naona nazidi kupoteza muelekeo. Naombeni ushauri wenu wa mawazo naweza kufarijika kwani nipo njia panda. Ninampenzi ambaye kwa kiasi kikubwa ninampenda , mwanzao wa mapenzi yetu alinieleza kuwa anampenzi lakini hawawezi kuwa pamoja kwasababu ya imani ya dini zao hivyo uwezekano wakuishi pamoja hautaendelea kuwepo. Mimi nilikubali kwani nilikuwa tayari nimeshampenza sana.

Hivi sasa mimi nina mimba, na yeye ananiambia na yule aliyekuwa mpenzi wake pia ana mimba sikujali. Tatizo lilokuwepo kila siku ananilazimisha nikatoe mimba mimi nimemwambia sipo tayari kufanya hivyo kwani mimi nina kazi yangu nimemwambia sitamsumbua lakini haelewi anatafuta mpaka watu waje wanishauri nikatoe. Pia ananiambia hataweza kuwa na mm bora aendelee na mpenzi wake wa mwanzo. Naombeni ushauri nifanyaje kwani bado nampenda sana.

Unajua ana mpenzi na wewe ukamkubalia! Hukujiuliza kuwa kama anaye na ananitaka mimi si anaweza kuongeza na wa tatu kama sio bibi wa nne! Tena ukaamua kutembea naye kavukavu na wewe unajua anakula makombo ama unamlisha mwenzako makombo! Ona sasa ulimtenda mwenzio yanakurudia.
Pole sana ingawa zilikuwa tamaa zako!

Ushauri
Achana naye kama unakiri kuwa una uwezo wa kulea huyo mtoto mwenyewe
Usijaribu kukanyaga tena kwake maana hana hata chembe ya huruma kwako! Amini anatamani hata sasa hivi uiache dunia ili awe huru!
Ni kosa kubwa kufikiria kuitoa mimba hii. Kosa sio la kiumbe kilichopo tumboni kwako bali kosa ni lako! kuna viongozi na watu wenye maisha yao humu duniani ambao mimba zao zilikataliwa na wazazi wao wa kiume! Tena utafikiri huwa wanagawiwa kipaji maalumu.
Kuna jamaa mmoja alitembea na binti wa shule miaka hiyo! Alipomfata mhusika akamwambia asimzoee! Ikabidi awaeleze wazazi wake, nao wakamkabili jamaa, akawatimulia mbali! Wakati baba yake huyu binti anatoka akamwambia hatolala juu ya mwanamke mwingine tena! Jamaa alidharau! Huku nyuma jamaa jogoo akawa hawiki tena! Akaanza kumtafuta yule binti! Alikua kupata taarifa kuwa yule binti alirudi kijijini na baba yake kitambo na yuko kule anakotoka huyu waziri mkuu wetu wa sasa! akafunga safari. Siku anafika pale kijijini akakuta turubali linafunguliwa. Baba wa yule binti aliaga dunia na alimwachia laana binti yake asijerudiana na yule baradhuli! Jamaa alirudi jijini kichwa chini. Jamaa amekufa hivi karibuni hakuwahi kuwa na mke na wala hakubahatika hata kumjua mtoto wake maana binti naye alitowekea kusikojulikana.
So mimi nataka kusema kuwa unapopata bahati ya kupata ujauzito hata kama umepata maudhi gani ACHA wazo la kukitoa hicho kiumbe tumboni mwako! Inawezekana its the only child you could have!
sali sana na umwombe Mungu akuongoze kwa kila kitu.
 
Kwa uzoefu wangu...huyo mwanaume hajawahi kukupenda hata kidogo...........ni tamaa tu ndio zilimfanya akudanganye na wewe ukaingia line na akamaliza shida zake na kukuachia mzigo. La kufanya......achana nae kwa amani, muombe Mungu akusamehe na kukupa nguvu na afya ili uweze kumtunza mtoto wako, maisha yaendelee.
 
usithubutu kutoa mimba hata kidgo
wapo kina dada wanaouta sasa kwa kutoa mimba na sasa wanalilia watoto
Mtunze huyo kiumbe wa Mungu.
mwepuke huyo kijana kama ukoma na epuka kunywa au kula chochote kutoka kwake
anaweza kukuchanganyia dawa za kuharibu hiyo miba
stay away from hiiiiiiiiiiiiiiiiimmmmmmmmmmmmmmmmm
 
Najiona mwenye furaha tena, kwani ushauri wenu unipa moyo na kunitia nguvu mbalikiwe sana. Msichoke kuniapa ushauri zaidi Mungu awatanguliie.
 
ulikubali ujinga toka mwanzo

achana nae, leo mwanao

mwisho, mapenzi husa hayatesi mtu, sisi binadamu tunakimbilia mateso wenyewe
 
Pole mdada, kuhusu suala la kutoa au kutokutoa hiyo mimba mi nakushauri uusikilize moyo wako, cjui kwa sasa unamchukuliaje huyo mwanaume aliyekudanganya akafunua na kufunikia hicho kiumbe halafu hakihitaji.

Iwapo utakuwa unamchukia inawezekana huyo mtoto akaja kuwa anakukumbusha machungu na hata kukukosesha furaha, lakini km unachukulia poa basi usitoe.

Kwa mabinti hebu jifunzeni basi mwanaume anapokuambia amegombana na mpenzie au hana sifa, km unampenda mpokee lakini mweke katika kipindi cha mpito ukifuatia yale aliyoyasema kabla ya kuingia ktk uhusiano wa ndani zaidi.
Kwa asili mapenzi huwa hayafi hivyo hata km watu wamegombana muda huweza kuponya machungu na kujikuta wanarudiana sasa ww uliyedandia unajikuta unaachwa solemba.
 
Miriam usitoe hiyo mimba yako, itunze vizuri tu. Ila pia uendelee kumwambia huyo mtu kuwa huo ni mzigo wake wa halali na ni damu yake ambayo anataka kuisaliti
 
aisee nachoweza kukwambia ni kwamba afya yako ni muhimu kuliko mapenzi..
 
dada yangu huyo ndugu ahkupendi,na inaonekana alikutamani ili kukamilisha baadhi ya mambo yake,sawla la ujauzito kwake anaona ni kama hatari itakayomuaribia kwa huyo mpnz wake mwngne.kaa mbali na huyo ndugu bse hakuna future yoyote hapo zaid atazidi kukupotezea muda wako.jipange upya na usikubali kuua kiumbe kisicho na hatia kwa ajili ya dhambi mliyofanya ninyi,itakuwa laana kwako na uzao wako wote.
 
Huyo ni muuaji dada. Endelea na maisha yako, hata kama unampenda sana unatakiwa na wewe ujipende na ujionee huruma.
 
Achana nae, kaa na mimba yako. Kumbuka God will be there for you,
na mwanao utakae mzaa will always be there for you too.
Huyo mwanaume amesha sema hakutaki, anamtaka yule mpenzi wake wa zamani,
why let him influence your decision? mtoe kabisa katika mipango yako,
just be happy to have a kid of your own! Be happy!
 
wote watatu wamekutana. kipofu na kiziwi hakuna wa kumuongoza mwenzie, ndio maana wote wana mimba wakati mmoja wakati condom is only 100 shs. unless kama unataka zile zisizo na fungus ndio kuanzia 2000 which is still very cheap kwa afya yako. mie sina cha kukushauri zaidi ya kukupa big pole, na pia usitoe mimba yakop kama unaweza kumlea mtoto wewe mwenyewe.

Huyu mpenzi wako hakupendi bali alikuwa anakutumia
Ila aniacha hoi ina maana hajali afya yake yaani anado na kila mmoja bila kutumia protection
kweli kuna watu wamejitoa fahamu hapa duniani
Cha msingi usitoe mimba zaa,na tunza mwanao ila huyo mpenzi wako hana mapenzi ya kweli kwako
Jipange upya Miriam
 
Asante kwa ushari.

Nnitakuwa sina fadhila kama sita washukuru wote waliochangia kunitia moyo na kunipa mawazo mapya mada yangu Mungu awabariki wote. Hakika nimefarijika na nimejifunza mengi "Nitaangalia nilipo angukia sitageuka kuangalia nilipo jikwaa". ASANTENI SANA
 
MAPENZI YANANITESA NIPENI USHAURI

Nimefikiria kwa muda mrefu naona nazidi kupoteza muelekeo. Naombeni ushauri wenu wa mawazo naweza kufarijika kwani nipo njia panda. Ninampenzi ambaye kwa kiasi kikubwa ninampenda , mwanzao wa mapenzi yetu alinieleza kuwa anampenzi lakini hawawezi kuwa pamoja kwasababu ya imani ya dini zao hivyo uwezekano wakuishi pamoja hautaendelea kuwepo. Mimi nilikubali kwani nilikuwa tayari nimeshampenza sana.

Hivi sasa mimi nina mimba, na yeye ananiambia na yule aliyekuwa mpenzi wake pia ana mimba sikujali. Tatizo lilokuwepo kila siku ananilazimisha nikatoe mimba mimi nimemwambia sipo tayari kufanya hivyo kwani mimi nina kazi yangu nimemwambia sitamsumbua lakini haelewi anatafuta mpaka watu waje wanishauri nikatoe. Pia ananiambia hataweza kuwa na mm bora aendelee na mpenzi wake wa mwanzo. Naombeni ushauri nifanyaje kwani bado nampenda sana.

Soma wewe achana na mambo ya wanaume....Elimu ni ufunguo wa maisha na PENZI ndi KITOVU CHA UZEMBE......shauri zako endekeza mapenzi tu kitu kikiisha oil seal moshi tupu utaruki home unakaa kibarazani unaanza kuuza vitumbua
 
dada
pole huyo mtu hana mpango na wewe ucitoe hichoo kiumbe Mungu anamakusudi nacho pole Mungu akujalie uvumilivu na hekima katika kufanya maamuzi yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom