Mapenzi: Eti nikiolewa na maskini atanisumbua sana?

Logo

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
588
48
Yani mimi napenda sana niolewe na maskini ili nimtunze mimi! Ukweli hakuna anachoweza kukosa kwangu na uzuri vyote ni haki na vya kupewa na Bwana. Sasa eti nimejaribu sana kutafuta maskini ila awe na sifa za kujiheshimu, mcha Mungu lakini sipati! Mama ameniambia eti watanitesa sana. Nisaidieni eti kweli watanitesa?
 
sifikirii kama masikini atakutesa.mapenzi hayajali umasikini,au utajiri.ni maelewano tu ya nyinyi wawili.mkiwa na maelewano mazuri,mnakuwa na furaha na anaweza akawa hana kitu,ila akawa na akili ya kujiendeleza au wewe mwenyewe ukamuendeleza.
 
Maskini kwa maana ipi labda?
Kilema hawezi kufanya kazi?
Na kipimo cha huo umaskini unaoutaka ni upi?
Dah, Maskini anayetafutwa hivi anaweza kuwa humu eeh!!!!!
 
Maskini kwa maana ipi labda?
Kilema hawezi kufanya kazi?
Na kipimo cha huo umaskini unaoutaka ni upi?
Dah, Maskini anayetafutwa hivi anaweza kuwa humu eeh!!!!!

Huenda ana majibu...hapa jamvini wote ni matajiri ila wametofautiana.
 
ukitafuta masikini uwe tayari kuvumilia na kumpa ushauri nasaha kila siku juu ya kujiamini. wanaume hawapendi kutunzwa. atakuwa anajisikia kutokuwa huru na wewe na pia hatakuwa na raha akitumia mali zako. isitoshe watakaomcheka kuwa kaolewa watamkatisha tamaa zaidi. ndugu zako nao wakiona shemeji ni hohehahe wapo watakaomsimanga. ndugu zake watamsusa kwa kumuona kajilengesha kwa sugar mami nknk.

utakuwa mlolongo wa matatizo ya kisaikolojia. ila kama mtazungumza vizuri na mkaelewana na wewe ukamtrain vizuri, ukajiepusha kumynyanyapaa kwa vijisenti vyako au mali zako na mkajiamini kiasi cha kupuuza maneno ya third parties, you can make a happy family. pia itapendeza kama mtashirikiana mtafute kitu ama shughuli ya kumuweka busy kama hatakuwa na kazi kabisa.

mkishindwa, uwe tayari kujkuta unaishi na mtu asiye na furaha na hata kuwa na mpenzi mwingine masikini wa nje is very probable na hela za matumizi utakaokuwa unampa ndio atakuwa akiwahongea hao wasichana wa pembeni. lengo ni kiridhisha nafsi yake kwani wewe atakuwa anafanya na wewe mapenzi kama kutimiza wajibu tu kwa mtu anayempa kula yake hapa duniani

hayo mambo ni too psychological na siyo ya kukurupuka nakutakia tafakari njema

Glory to God
 
Both ur mom and Judy are right, utapata shida unless umkabidhi mali yako aimiliki yeye. Ingawa u can be prone to other dissappointment kama unfaifullnesd, depends on his motive of being with u.
 
mapenzi hayaangali masikini wala tajiri.
kuhusu matatizo ya ndoa ,that inategemeana na mtu na mtu ,by thaway huyo maskini ukimpata na akigundua ulimtafuta kwasababu ya umaskini wake hakutakuwa na uelewano hapo tena.
hlf unaonekana ni mtu wa kupenda kumiliki miliki wewe.
 
Mi bado sijajua huyo maskini mnayemuongelea ni maskini wa namna gani.
Kiwete, tahira, mjinga au..........
AU kwakuwa kipato changu ni sh 500 cha kwako 1000 basi mi maskini.
Ni maskini wa aina gani huyu mnaemuongelea hapa????
 
kuna case ya jaffarai na shyrose,ukiachwa bi dada utatukanwa weeeee.....tafuta mtu mnayeendana naye kitabia,kifedha nk...hii itakupa security na yeye pia atajiamini kama mwanaume ndani ya nyumba hivyo kuepusha migogoro/mifarakano inayotokana na insecurities/
 
kuna case ya jaffarai na shyrose,ukiachwa bi dada utatukanwa weeeee.....tafuta mtu mnayeendana naye kitabia,kifedha nk...hii itakupa security na yeye pia atajiamini kama mwanaume ndani ya nyumba hivyo kuepusha migogoro/mifarakano inayotokana na insecurities/

Leo kweli umeamua
 
Tafuta tu mchumba mungu aliyekupangia na si mchumba masikini, kama mungu hajakupangia mchumba masikini je?
 
Yani mimi napenda sana niolewe na maskini ili nimtunze mimi! Ukweli hakuna anachoweza kukosa kwangu na uzuri vyote ni haki na vya kupewa na Bwana. Sasa eti nimejaribu sana kutafuta maskini ila awe na sifa za kujiheshimu, mcha Mungu lakini sipati! Mama ameniambia eti watanitesa sana. Nisaidieni eti kweli watanitesa?

Una maanisha masikini wa mali au kiroho? Fafanua tafadhali.
Ila pia chunga sana kuna wanaotafuta (siaajabu hapo kanisani kwako) kuharibu mipango ya watu kama wewe. Kumgundua unajikuta tayari hata mimba ulisha bebeshwa. now it becomes an insult to an injury! Mara wiki ya kwanza tu ya unyumba ana disorganize hiyo reception yako.
Sehemu nzuri za kupata wachumba ni college, working environment yako and other places where you spend some of your time at leisure. Ila maombi kwa mungu wako tanguliza.
 
Acha kutumia akili yako tu , mshirikishe Mungu... Kumbuka upo ktk kipindi cha kufanya makosa, One mistake will cost you the rest of your life
 
Unaweza olewa na maskini ukitaka awe maskini milele badae anakuja kuwa tajiri wa kutupwa kwa bidii yake, sasa ikiwa hivi utamwacha? omba tu upate wa kufanana na wewe tabia hobbies na vinginevyo.
 
Ngoja niungane na wadau hapo juu kujua tafsiri ya "Masikini" kwa mujibu wa mtoa mada. Huenda nikawa na vigezo!
 
Nafikiri kuna tofauti kubwa ya masikini na fukara,sasa unayemtafuta wewe ni fukara.
 
duuu pole
definition
- yangu ya masikini ni mtu ambaye hana miguu na mikono
au amekosa kiungo fulani cha mwili Je we ndo unamtafuta mtu wa namana hiyo ?
??
 
Da!!! Hakika JF pana utajiri wa majibu, utapata majibu ya ukweli, ya kufurahisha, ya kutia moyo, yenye kuhitaji ufafanuzi, yenye kukatisha tamaa,yenye kuliwaza,ya kitaalam zaid,ya kutumia uzoefu.....ukiwa uwanja wa JF no stress at all.......ASANTE WADAU WA JF.
 
Back
Top Bottom