Napenda kuanza na nukuu ya mwanafalsafa simkumbuki jina aliyesema " Elimu humfanya mwerevu kuwa mwerevu zaidi na mpumbavu kuwa mpumbavu zaidi"
Kuna kitu hatujakigundua katika suala zima la elimu.Tuna watu wenye ma PhD na ma degree wengi zaidi ya asilimia 99.9 tumewaamini kama "think tanks" wa nchi kumbe hawawezi kufikiri kabisa.
Kipimo cha wao kupata hizo shahada ni uwezo wa kukumbuka vitu na sio uwezo wa kuchakata.Kukumbuka vitu ni kipaji kama alicho nacho ndege kasuku.Kipaji cha kukumbuka vitu hakiwezi kuwa kipimo cha akili.Bahati mbaya maprofesa wengi, na wasomi wengi walipatikana kwa kipimo hicho cha uwezo wa kukumbuka.Hawa ndio wanaitwa watu wenye akili sana.
Nasikitika kusema kuwa nchi yetu kama siyo nchi zetu za kiafrika,tutaendelea kuwa maskini wakubwa hadi pale tutakapochoma misingi ya elimu tuliyorithishwa na mzungu.Siamini kama wachina wanasoma upumbavu unaotupotezea muda shuleni na vyuoni.
Anatakiwa kiongozi anayeweza kuliona hili.
Kufuta vyeti vyote ambavyo havileti suluhisho kwa changamoto tulizo nazo.
Inatakiwa uthubutu mkubwa.
Binafsi ninaumia sana kwa hii hali kuendelea.Tutakuwa wateja wa simu ,teknolojia,silaha,sawa hadi toothpick na cotton buds?!!
Tutasoma kwa mtindo huu huu tuliodanganywa eti 7:4:2:3?!!Ni nani alifanya utafiti kuwa huu mfumo ndio unafaa?
Niko tayari kupokea matusi lakini siamini katika wasomi wetu ambao wengi wameifanya elimu kama nyenzo ya kuibia serikalini na kwa watu,cheti kama kitu cha kutambia mtaani na ikibidi kutukania watu wasio nacho,kama nyenzo ya kutunga sheria kandamizi ili ziwalinde mkiiba kwa kushirikiana na watu weupe.