Maoni yatolewayo na wanasiasa wajulikanao hapa JF yalindwe vipi?

Mwl Kichuguu,

Nakubalina na wewe kuwa distortion ni kitu kibaya sana.......nilipoisoma habari uliyoiweka nikamsikitikia Mh Zitto......."pengine" alikuwa so genuine akimjibu Lingson............nimesema pengine nikiwa na maana......no body is sure kwamba he meant what he said...........na kutokana na hilo watu tofauti huja na perceptions na analysis mbali mbali........hili hatuwezi kulizuia......wengine wamekuwa victims to some circumstances kwa the so claimed "tafsiri mbovu mbovu" kama za mwandishi wa Absalom.........na nilivyomuelewa Mkuu Absalom ni kwamba yeye anaruhusu open analysis.....which may be termed distortion in this case...............

....sasa how do we deal with such situations..........tulalalmike kuwa tumenukuliwa vibaya na kwa nia mbaya kwa kuwa una wapinzani?......I usually call this as "a baby cry"........habari yako inapokuwa distorted..........kuna ubaya gani/unaonaje uki-clarify.......na kama mtu umekuwa offended with obvious distortion.........si kuna taratibu zake......au?

watu wanaposema siasa ni mchezo mchafu.....THEY REALLY MEANT IT!

Omega......ameandika hapa kuna njia nyingi za kufikisha ujumbe.........mambo mengi tu hapa JF yameandikwa na yamenukuliwa (kutoka kwa wanaJF wenye nick names mpaka wenye majina yao halisi)...........either kwa ubaya.....na mengine mazuri tu na yamefanyiwa kazi.........ushahidi upo........

Kumbuka issue ya "Air Uchumi wa Lowassa"

Forum aliyokuwepo Lowassa mpaka kuzungumzia uchumi wetu unapaa........haikuwazuia wana JF wakiongozwa na Mwanakijiji kumshukia Lowassa.......despite kuendelea kutetea hoja yake kwa facts....and ofcourse alipingwa vikali kwa facts..........lakini a plausible action ya Lowassa alisimama bold kujibu....kuna waliomuona "amejibu" na kuna sie tulioendelea kumuona "kachemka"...........

besides........alicho-suggest Mh Zitto kwa Lingson is not the end of the world.........it was a suggestion kama alivyoombwa atoe mfano........kuwa-crush akina Absolom kwa waliyoaandika its very easy........au anaweza kuja sema otherwise or ku-emphasize alichomaanisha...............

Swali la msingi ulilouliza ni kuwa tuwa-protect vipi hapa JF watu wanaotumia majina yao halisi e.g Mh Zitto......

Aina ya protection itategemea sana na level ya exposion ya ideas za mtu mwenyewe.........something very difficult ku-control kutokana na level of freedom tuliyonayo hapa...........watu wako huru kusema chochote ili mradi hawaendi kinyume na conditions za JF........

pili JF ni chombo rasmi na distortion ikafanyika kuichafua JF na wana JF then hatua/taratibu zipo dhidi ya "distorters".........nafikiri pia mhusika inabidi aongee na Admin wa JF kuelezea the whole distortion.............

tatu.....watu tuwe makini na tunachokiandika
 
Swali langu, je hapa JF tuna utaratibu gani wa kulinda michango original ya wanachama wetu (hasa wale wanaojulikana kwa majina yao halisi) isipotoshwe kwenye print media au kwa njia nyingine yoyote?
Mkuu wangu Kichuguu, nimekuwa nikimfuatilia sana Zitto akiandika kwenye Google Groups na anakuwa mis-quoted. Ambacho hajajua hapa ni kuwa hizi zinatuma emails kwenda kwa watu zaidi ya hao ambao anawaona kwenye circulation list inayoenda kwake. Kwake anaona watu kama 6 so anaandika sensitive issues sometimes akijaribu kuwa muwazi (kitu ambacho si kibaya) sema watu wanautumia mwanya huo kumwaribia.

Haya yalitumika kipindi cha Zitto vs Freeman, yakaja kipindi cha Zitto vs Kafulila issue ila ngumu kwangu kuingilia the CHADEMA issue. Kwa mwanasiasa ambaye anajua tofauti ya Google au Yahoo Groups zinafanyaje kazi na Public Forums zinafanyaje kazi basi anaweza ku-opt kwenda kwenye Public Forums kuliko kwenda kwenye Google au Yahoo Groups ambako kuna hidden readers (huwaoni, wanakusoma bila wewe kujua na wanaweza kukutafsiri vinginevyo).

Kuhusiana na JF:

Ni ngumu kwa mwandishi kuupotosha ukweli kuhusiana na alichoongea mwanasiasa hapa JF, JF si blog kusema haitachukua hatua dhidi ya mtu aliyeupotosha ukweli wa habari flani iliyoandikwa humu endapo itatokea imefanywa hivyo kwa makusudi. Ikitokea mwanasiasa ambaye amejiandikisha hapa kwa jina lake ameandika hapa kitu sensitive na akanukuliwa vibaya na vyombo vya habari na akataka JF tumsaidie kuchukua hatua tunachukua hatua kweli, maana habari yenyewe inakuwa bado ipo hapa na iko public na gazeti linalokuwa limeinukuu vinginevyo itabidi limwombe msamaha mhusika!

Hatuzuii mtu kutumia contents zilizo JF, ila kuzitumia kinyume ya zilivyowekwa ni kosa kubwa.

Kumradhi, sikusoma michango ya wengine kwasababu ya haraka nilizokuwa nazo, nimejibu kwa harakaharaka...
 
Kichuguu:

Itakuwa ni kukosa maadili na kuminya uhuru wa vyombo vya habari kusema kwamba waandishi wa habari wasiwanukuu yale ambayo wanasiasa wanayoyasema na kuyaandika katika forum hadi wapate kibali. Hiyo itakuwa sawa na kuwaambia wasiandike habari za yale wanayoyasema wanasiasa kwenye mikutano ya hadhara, hadi wawe wamepewa ruhusa na wanasemaji. Hiyo itakuwa haijakaa sawa. Kinachotakiwa:

i) wanasiasa wawe makini na kuyasimamia yale wanayoyasema popote pale, iwe ni kwenye mikutano ya hadhara, kwenye press conference, kwenye dinner party, hapa JF, huko kwa wanabidii, etc

ii) waandishi wa habari kuwa na maadili, nidhamu, kuwa wa kweli na kuacha kutumiwa.

Sasa katika habari ya Tanzania Daima, ni wazi kwamba hawa bwana hawakuwa wa kweli, walikuwa waongo, hawakuwa na nidhamu, na kushinda yote, kuna dalili kwamba mwandishi na gazeti walikuwa na malicious intent katika kuandika ile habari. Kwa kifupi hawa sio tu wamekosa maadili katika uandishi wao, lakini pia wanapoteza sifa ya kuwa gazeti. Kibaya zaidi, Kibanda ambaye ndiye mhariri mkuu, badala ya kukiri udhaifu na kuomba msamaha kwa uozo wa habari waliyoandika, anajaribu kuhalalisha yasiyohalalishika. It's terribly disgusting.

So, kwa maoni, katika hili, tatizo sio aliyetoa maoni yake kwenye wanabidii, tatizo ni hilo gazeti ambalo linajaribu kujenga taswira mbaya ya wananchi dhidi ya Zitto kwa habari ya kupika! Kwa lengo gani? Time will tell what these guys are up to!
 
Ogah:

That is the mistake Kibanda is making, Ile haikuwa analysis. Ile ilikuwa ni habari; haikuwa makala ya mwandishi. Kama alikuwa hajamwalewa Zitto angeiweka habari yenyewe kwenye question mark. Ukisoma kichwa cha habari unapata picha moja kwa moja kwamba Zitto alikuwa anapendekeza Kikwete aongezewe muda wa kuongoza, maoni ambayo yamekaa kiLamwai kiLamwai enzi za Mkapa ambayo ndiyo ilikuwa silaha ya mwisho dhidi ya uanasiasa wake.

Kwa hiyo tusichanganye, ile haikuwa makala ya analysis-mwandishi alikuwa anaripoti habari ambayo haikuwepo-what else can you say other than a malicious intent or at least a personal vendetta?
 
Tabia hii ya waandishi/wahariri ku-quote out of context ni ya kawaida sana kwenye magazeti yetu[na kwa bahati mbaya wengi huamini hivyo na kuchukulia kuwa ni kweli]. Hali hii inawafanya wengi kuogopa kuchangia na pengine ndiyo maana hujificha kwenye majina yasiyo halisi.
 
Dr. Kitila,

Naungana na wewe hasa ikizingatiwa kama kweli Kibanda ni kiongozi anajua kabisa habari zinavyosambaa. Kuanzia saa 12 unusu karibu kila mtu anafungulia RFA kujua nini kilichopo. Mimi ni msikilizaji mzuri, i heard it and i thought was Mtanzania.

Wengi wanategemea heading pasipo kwenda kuchambua ndani kuna nini. Sijui Mhariri mtendaji kazi yake ni but hali ya hewa iliopo hakupaswa kurusha ile heading.

Only heading ndo imeharibu mambo.
 
Kichuguu:

Itakuwa ni kukosa maadili na kuminya uhuru wa vyombo vya habari kusema kwamba waandishi wa habari wasiwanukuu yale ambayo wanasiasa wanayoyasema na kuyaandika katika forum hadi wapate kibali. Hiyo itakuwa sawa na kuwaambia wasiandike habari za yale wanayoyasema wanasiasa kwenye mikutano ya hadhara, hadi wawe wamepewa ruhusa na wanasemaji. Hiyo itakuwa haijakaa sawa. Kinachotakiwa:

i) wanasiasa wawe makini na kuyasimamia yale wanayoyasema popote pale, iwe ni kwenye mikutano ya hadhara, kwenye press conference, kwenye dinner party, hapa JF, huko kwa wanabidii, etc

ii) waandishi wa habari kuwa na maadili, nidhamu, kuwa wa kweli na kuacha kutumiwa.

Sasa katika habari ya Tanzania Daima, ni wazi kwamba hawa bwana hawakuwa wa kweli, walikuwa waongo, hawakuwa na nidhamu, na kushinda yote, kuna dalili kwamba mwandishi na gazeti walikuwa na malicious intent katika kuandika ile habari. Kwa kifupi hawa sio tu wamekosa maadili katika uandishi wao, lakini pia wanapoteza sifa ya kuwa gazeti. Kibaya zaidi, Kibanda ambaye ndiye mhariri mkuu, badala ya kukiri udhaifu na kuomba msamaha kwa uozo wa habari waliyoandika, anajaribu kuhalalisha yasiyohalalishika. It's terribly disgusting.

So, kwa maoni, katika hili, tatizo sio aliyetoa maoni yake kwenye wanabidii, tatizo ni hilo gazeti ambalo linajaribu kujenga taswira mbaya ya wananchi dhidi ya Zitto kwa habari ya kupika! Kwa lengo gani? Time will tell what these guys are up to!

- Dr. Kitila, huwa ninasema hivi watu kama wewe ndio mmemalizia zile PhD kama za wazazi wetu, maana siku hizi kuna PhD mpya za kusikitisha sana unayoyasema nimeyasema sana hapa kwamba kama tuna wanasiasa wanaoweza kuja hapa na kusema wasiyoyaamini kwa vile ni forums hatuwahitaji kwenye taifa, ahsante sana kwa maneno yako mazito sana.

Respect.

FMEs!
 
Strongly I do support Dr Kitila Mkumbo and FMEs;there is no room for any preferential treatment in our discussion forum!

JF ikazanie kuwalinda wachangiaji wake kama alivyobainisha mkuu Invisible na izidi kutoa nafasi sawa kwa kila mchangiaji anayekuja hapa;hiyo ya kuwalinda baadhi ya wachangiaji hapa haipo na isiwepo!

Kama una hisi ulinukuliwa vibaya ni jukumu lako kutoa ufafanuzi iikuwaje na uamuru rasmi uombwe msamaha kwa yale waliyoyapotoshana ,na wewe uliyeombwa msamaha sasa ni juu yako ama kukubali na kuendelee kuchangia au kukataa na kuacha kuchangia!

JF;for great thinkers!
 
....... watu tofauti huja na perceptions na analysis mbali mbali........hili hatuwezi kulizuia......wengine wamekuwa victims to some circumstances kwa the so claimed "tafsiri mbovu mbovu" kama za mwandishi wa Absalom.........na nilivyomuelewa Mkuu Absalom ni kwamba yeye anaruhusu open analysis.....which may be termed distortion in this case...............

....sasa how do we deal with such situations..........tulalalmike kuwa tumenukuliwa vibaya na kwa nia mbaya kwa kuwa una wapinzani?......I usually call this as "a baby cry"........habari yako inapokuwa distorted..........kuna ubaya gani/unaonaje uki-clarify.......na kama mtu umekuwa offended with obvious distortion.........si kuna taratibu zake......au?

........kuwa-crush akina Absolom kwa waliyoaandika its very easy........au (i.e. Zitto) anaweza kuja sema otherwise or ku-emphasize alichomaanisha...............

Ogah:

That is the mistake Kibanda is making, Ile haikuwa analysis. Ile ilikuwa ni habari; haikuwa makala ya mwandishi. Kama alikuwa hajamwalewa Zitto angeiweka habari yenyewe kwenye question mark. Ukisoma kichwa cha habari unapata picha moja kwa moja kwamba Zitto alikuwa anapendekeza Kikwete aongezewe muda wa kuongoza, ...........

Ni kweli kabisa Mkuu Kitila..........

.........sikutaka kusema moja kwa moja kuwa mwandishi yule alifanya poor analysis (kwani hili tatizo mojawapo la kuruhusu open analysis)..........tuna matatizo sometimes ya kutokujielewa na kutokubali ujinga wetu........

..........ndio maana nikasema....it is very easy ku-crush mtu kama Absolom na mwandishi wake kutokana na ile analysis (maana Absolom mwenyewe amedai ile ilikuwa analysis)........analysis zina level mbali mbali kulingana na aina ya watu (uwezo), nyakati na mazingira........

otherwise tuko pamoja Mkuu

Na katika kuwalinda watu kama akina nyie nilisema hivi

Swali la msingi ulilouliza (i.e. Kichuguu) ni kuwa tuwa-protect vipi hapa JF watu wanaotumia majina yao halisi e.g Mh Zitto......

Aina ya protection itategemea sana na level ya exposion ya ideas za mtu mwenyewe.........something very difficult ku-control kutokana na level of freedom tuliyonayo hapa...........watu wako huru kusema chochote ili mradi hawaendi kinyume na conditions za JF........

pili JF ni chombo rasmi na distortion ikafanyika kuichafua JF na wana JF then hatua/taratibu zipo dhidi ya "distorters".........nafikiri pia mhusika inabidi aongee na Admin wa JF kuelezea the whole distortion.............

tatu.....watu tuwe makini na tunachokiandika
 
Naona kuwa swali langu halijaeleweka kwa watu wengi sana hapa, including kwa Dr. Kitila; ngoja niliruide tena:

Swali langu, je hapa JF tuna utaratibu gani wa kulinda michango original ya wanachama wetu (hasa wale wanaojulikana kwa majina yao halisi) isipotoshwe kwenye print media au kwa njia nyingine yoyote?

Nimebold na kuandaline point kubwa ninayoongelea ya KUPOTOSHWA. In fact swali hili halilengi wanasiasa wanaoujulika tu, ni kuhusu members wote ila nimewataget wanasiasa kwa vile ndio wako vulnerable zaidi kwenye swala hili. Sina maana ya kuzuia waandishi wasiwaquote wanasiasa; ndiyo maana huko nyuma nimemwambia FMEs kuwa matumizi yangu ya term "forum siyo press conference" huenda yalikuwa yanakwenda zaidi ya lengo langu hivyo nikai-withdraw statement hiyo hivi:
Kwa kurekebisha tu, nitakubaliana nawe kwa kufuta neno langu la "press conference," lakini hoja yangu kubwa inabaki pale pale kuwa wasichuke post moja na kuifanya habari kamili bila kuiunganisha na premises zake zote na vile vile kupata uthibitisho kutoka kwa mchangiaji. Inawezekana mchangiaji akawa anatoa vipande vipande kabla ya kuungnsiha, wewe mwenyewe FMES umewahi kutuwekea post za namna hiyo na kuacha kuwa tunakufuatilia kwa siku kadhaa hadi unapomaliza mada yako.

Nimerudia tena hapa kama ifuatavyo:

Nimeanza kuona ugumu wetu katika matumizi ya maneno. Wakati ni kweli kuwa kila mtu analoongea kwenye mtandao lazima litoke moyoni mwake na awe tayari kulisimamia, ndugu yangu unalokosea ni kuchukulia kuwa tunatetea maneno yaliyosemwa na Zito, hapana, tunachoongelea ni ule upindishaji wa yale yaliyosema na ZIto, na kuyachukulia nje kabisa ya mada. Nimekopi hapo ujuu posts zote zilizoandikwa na Zito kwenye forum ile: zilikuwa mbili tu. Hakuna hata moja iinayoonyesha kuwa Zito alisema JK aongezewe muda.

Inapotokea gazeti likaandika kuwa eti Zito alipokuwa kule JF alisema kuwa JK aongezewe muda, ni distrotion ambayo siyo tu inachafua jina la Zito bali pia credibility ya JF yenyewe. Maoni yangu ni kutaka posts za hapa JF zisiwe distorted kwenye media; wakiamua kuzitumia basi wazitumie kama zilivyotolewa na mchangiaji bila kuziwekea chumvi au pilipili yoyote. Sababu ya kuwataka wawasiliane na mchangiaji ni huko kutaka kuhakikisha kuwa wanajua fika kuwa wanalioandika linaendana na nia ya mchangiaji huyo siyo nia yao wenyewe. Ni posts chache sana kwenye forum ambazo ni standalone kwa nyingi hutolewa vikiwa ni vpande vipande vinavyoendana na mtililiko wa mjadala wenyewe, hivyo wakichukua vipande vichache tu inabidi wao ndio wawe waangalifuy siyo mchangiaji.

Nadhani point yangu imeelezeka vya kutosha ila naona wengi wetu hatujaipokea vizuri tu huenda kwa vile inaonekana kama vile inamtetea mwanasiasa mmoja wa chama fulani badala ya kuichukulia kwa mapana yake yote. Maoni ya baadhi ya wachangiaji kuwataka wanasiasa wote wawe makini na wawe wanaandika posts zilizo kamili badala ya kuandika posts vipande vipande ni jambo zuri kwa maana pana zaidi lakini ninana kama halina uhusiano wowote na wao kuwa misquoted na waandishi wa habari. Ninapigia kelele jambo hili kwa sababu nimeanza kuwa na imani kuna waandishi wa habari ndani yetu wanatumia mwanya huu kwa makusudi kabisa kudistort yaliyoandikwa na wanasiasa kwa sababu za kisiasa tu.

Madhara ya kumisquote wanasiasa kwenye vyombo vya habari ni mapana kuliko haya ya ninayoongea hapa ya kuchafuana majina na kudiscredit fora zinazotumiwa na wanasiasa hao. Kuna madhara makubwa zaidi mabayo ni ya kutoa huduma hafifu za habari kwa wananchi na hivyo kuendelea kujenga uninformed society, jambo ambalo ni baya zaidi.
 
............Madhara ya kumisquote wanasiasa kwenye vyombo vya habari ni mapana kuliko haya ya ninayoongea hapa ya kuchafuana majina na kudiscredit fora zinazotumiwa na wanasiasa hao. Kuna madhara makubwa zaidi mabayo ni ya kutoa huduma hafifu za habari kwa wananchi na hivyo kuendelea kujenga uninformed society, jamabo ambalo ni baya zaidi.

Mkuu uko sahihi kabisa.........

Starting point should be kwa mtu aliyeathirika/distorted/misquoted ku-point out kwa JF Admin....nina imani JF watalishughulikia ipasavyo.......

Pili, hata JF Admin wakiona au sisi memba hapa JF tukiona jambo hilo basi tuwataarifu JF Admin...........

hayo ni maoni yangu kwa sasa
 
Mimi sio mwandishi wa habari lakini kulingana na swali la kwenye mada hii, inabidi kila mwandishi wote wale makini na wale uchwara anaeandika habari yoyote ile inaohusiana na jamiiforums ni lazima aeleze nukuu kutoka jamiiforums.com.

Vyombo vingi vya habari duniani yakiwemo magazeti wanapoandika habari yoyote ile ambayo haikutokana na juhudi za mwandishi bali kutoka katika chanzo chochote huwa wanaweka wazi wapi wamepata "source" ya habari hio.

Kwa upande wa wanasiasa wenyewe wa aina ya mheshimiwa Zitto ni wazi kwamba inabidi wawe makini na waangalifu katika kutoa maoni iwe hapa jamiiforums au kwenye mkusanyiko wa watu au hata kwenye ukumbi wa starehe.

Ni lazima wajue kuwa wao ni kioo cha jamii ambayo siku zote huwa inatafuta "reference" au marejeo na kama "reference" hio ni mbaya ndio utakuta wanasiasa wanapata taabu kidogo.

Kwa hio kulindwa kwa maoni yao hapa JF ni kwa wale waandishi kuonesha kwamba habari wanayoiandika imepambwa na marejeo kutoka JF.
 
Hapa hakuna suala la kukosa umakini kwa upande wa muandishi/waandishi wa habari pamoja na wahariri wake iwe ni jukumu la Kibanda ama Ansbert Ngurumo.

Ni wazi kabisa alieandika hii habari alikuwa anajua anachokifanya na wala siamini kama ni kazi ya muandishi mmoja bila ya ushirikiano wa waandishi watendaji wa gazeti hili ambao ni wataalamu wa upotoshaji wa makusudi - SPINING.

Ukiangalia ni wazi habari hii iliandikwa ikiwalenga watanzania walio wengi wasio na upeo wa kuchambua habari hizi kwa mapana yake, na ambao hawajui siasa za ndani za vyombo vyetu vya habari na ambao kutokana na uwezo wao kifedha ama utamaduni uliojengeka huishia kusoma vichwa vya habari tu vya magazeti na kufikia conclusions ambazo mwandishi ama waandishi wa habari ndizo wangependa wafikie.

Kinachouma zaidi ni kuwa gazeti hili sio just another newspaper when it comes to Zitto and the ongoing politics in CHADEMA.

Yawezekana kabisa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe hajahusika kabisa na habari hii lakini kuna historia ambayo wote tunapaswa kuiangalia kwa umakini. Wakati gazeti hili ambalo Freeman ni mmiliki wake ambalo liko chini ya kampuni ya FreeMedia kwa kutumia jina la mwanafamilia wake, limekuwa likiandika habari na makala lukuki zenye kulenga kujenga hali ya kutokumuamini na hata chuki dhidi ya Zitto tangia siku aliporudisha fomu ya kugombea UENYEKITI akishindana na Freeman Mbowe.

Mtu wa mwanzo kabisa kuandika aina hiyo ya makala ni ABSALOM KIBANDA ambaye hapa anajaribu kulazimisha kuwa uandishi huu wa Mobini Sarya ulikma ni uzembe tu na sio wenye nia mbaya.

Kibanda ni rafiki mkubwa wa Zitto na pia ni rafiki yangu lakini ukweli katika hili siwezi kabisa kufunika chungu maana ni wazi wameamua kuweka wazi vita yao dhidi ya Zitto kwa manufa yao binafsi na ya wale wanaodhani kuwa CHADEMA ni miliki yao na Zitto ni mzamiaji ambaye wangependa kumona wanammaliza kama wasemavyo.

Ni ajabu sana kuona sumu kama hii inatoka katika gazeti lenye uhusiano na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye siku moja tu kabla gazeti hilohilo lilimkariri Freeman akidai kuwa yeye hana ugomvi na "mdogo" wake Zitto.

Na kwa wale wanaodhani kuwa eti SIASA NI MCHEZO MCHAFU hivyo tuyaache haya yakiendelea kama vile ndivyo inavyopaswa kuwa, ujumbe wangu ni kuwa hata kama wengi waliopo katika siasa wanaona hivyo lakini sisi wengine tunaoamini katika mabadiliko makini tuna jukumu la kusiamama kidete kuhakisha kuwa tunajenga utamaduni wa SIASA SAFI.

Bila ya kusimama kidete kupigania SIASA SAFi kwa kukemea na kutojihusiaha na siasa chafu kamwe hatutakuwa na uhalali wa kujidai kuwa tunapigania mabadiliko chanya kwa nchi yetu. Tutaendelea kuwa watumwa wa siasa za ujanjaujanja na longolongo zinazotugharimu sasa...
 
Zito aache kulialia, mbona ni hao hao kina Absolom KIbanda ndio pekee walimuunga mkono wakati wa sakata la Dowans , mara nyingi walikopi na kupaste baadhi ya mambo aliyo ya sema humu JF bila ridhaa yake katika kuhalalisha upuuzi ule, hatukumsikia kulalama wala nini, leo kakubwa na balaa za critisism kule kwenye forum ya google basi wapambe wake wameibeba na kuileta humu JF kulialia,
anapaswa kutambua thamani ya yeye kua mwanasiasa na gharama ya yeye kua mwanasiasa, akisifiwa anavimba kichqwa akikosolewa anapayuka.
Jambo la mwisho aache kudekadeka na kulialia, kuwa mwanasiasa lazima kuwa na kichwa kigumu na kuvumila mengi. nakumbuka alipingwapingwa kidogo humu JF akajidai kususaa kuwa hatachangia tena na zaidi ya yote atabaki kua mtizamaji na mfatiliaji wa moai yetu, mimi naamini Zito ni mjivuni na mpenda ujiko asiependa kukosolewa kwa namna ambayo yeye hufanya dhidi ya wenzake.
 
Jamani hii kitu ukiingalia kwa umakini unaweza kupasua kichwa na jibu lisipatiknae. Two quick things from my idea
one, huku kwenye forums kila mtu kaficha jina na tunatumia majina feki (ispokuwa wanasiasa, so far) lakini tunajadili mambo halisi. my query is kwanini wao wameamua kutumia majina halisi? partly ni sababu ya nafasi zao. this gives brings me to a second query,

two, kama mwanasiasa wewe ni public figure! be responsible to what you say in public, wewe ni model. unafaida ya kupata forum cheap for communicating your idea, philosophy etc, thats is a plus.

therefore sion kwanini forums zinafikiria kulinda maoni yao ambayo waliyasema wakijua is an open forum people think differently. lets go ahead,
 
Well said Mkuu

Kulinda maoni "inapobidi" ni muhimu Mkuu.....kwa afya ya jamvi letu au hata mtu/mwanachama mwenyewe ikibidi unajitetea.........ndio maana tunamshauri Mh Zitto alinde maoni yake na aache "baby cry"..........kule alikotoa maoni kama hawana sera ya kulinda wanachama wake..........ni bahati mbaya.........na kuna option ya kutoe ufafanuzi yeye mwenyewe......

Hivi jamani shida iko wapi huyu Mh Zitto/mwanachama wa JF kutoa ufafanuzi pale maneno yake yanapotafsiriwa visivyo?........hii tabia ya kuzila zila/kulalalmika sijui itatufikisha wapi?.........
 
Kubwa ni kule kupotoshwa kwa maneno yao; akisema "anataka ua", basi wao wasiandike kuwa alisema "anataka kuua."

Well said Mkuu

Kulinda maoni "inapobidi" ni muhimu Mkuu.....kwa afya ya jamvi letu au hata mtu/mwanachama mwenyewe ikibidi unajitetea.........ndio maana tunamshauri Mh Zitto alinde maoni yake na aache "baby cry"..........kule alikotoa maoni kama hawana sera ya kulinda wanachama wake..........ni bahati mbaya.........na kuna option ya kutoe ufafanuzi yeye mwenyewe......

Hivi jamani shida iko wapi huyu Mh Zitto/mwanachama wa JF kutoa ufafanuzi pale maneno yake yanapotafsiriwa visivyo?........hii tabia ya kuzila zila/kulalalmika sijui itatufikisha wapi?.........

It is unfortunate kuwa mada hii imegeuka kuwa ya Zito; sikutaka tujadili maneno ya Zito. Nadhani wamekwisha yajadili sana huko alikoyatolea, na kama ningeta kuyajadili wala nisingeyaleta hapa kwa vile ningeweza kuyajadili huko huko.

Nilipoanziosha mada hii nilitaka tuangalie kama kuna possibilities za kuzuia watu wasiwe wanachukua discussion zetu hapa na kuzipotosha kwenye print media zao. Wakichukua post ya Kichuguu na kuwatangazia watanzania kuwa kichuguu kasema blablabla huku wamepindisha, huenda hakutakuwa hakuna tatizo kubwa kwa vile wananchi hawmajui Kichuguu; lakini wakichukua mada ya mwanasiasa anayetumia jina lake halisi na kuipindisha, kuna uwezekano mkubwa sana yule mwanasiasa akajitoa kabisa hapa ili kulinda jina lake.

Nina imani kuwa michango ya wanasiasa wanotumia majina yao moja kwa moja huwa ina nafasi fulani kwenye forum hii. Kwa mfano, juzijuzi tu kuna mtu alituambia hapa kuwa Nape kasema hili na lile na binafsi nilimuamini. Lakini baada ya Nape mwenyewe pamoja na mwenzie Mnyika kuja wakitumia majina yao halisi, mtazamo wangu ukabadilika kabisa; naona kuwa dynamics za namna hiyo kwenye forum ni nzuri sana. Mwaka 2006, tulikuwa na Freeman Mbowe amejiunga tu, lakini tulimkaribisha kwa makombora yaliyomfanya ashindwe kuvumilia na akajiondoa. Inawezekana bado yupo hapa anatumia jina la bandia e.g. "Kichuguu II," ila kwa vyovyote kungekuwa na utamu sana katika discussion anazochangia kama angekuwa anatumia jina lake halisi. Angalia jinsi posts za Slaa zinavyopokelewa na wanachama wengi hapa, hata wale wasokubaliana naye kiitikadi.

Hiyo ndiyo sababu nikafikiria iwapo tunaweza kuwa na rules zinazolinda posts zao zisipotoshwe kiasi cha kuwafanya watukimbie. Ilikuwa ni idea ambayo ilikuwa open for discussion lakini unfortunately imegeuka kuwa ya Zito.
 
Mimi nadhani pseudonames tunazotumia ni utaratibu tosha! Na tena utaratibu wa kukataza 'name calling' (i.e. hata kama umegundua true identity ya mtu ni marufuku kuiweka hadharani!) kwa maoni yangu unakidhi. Endapo mtu anaamua kuweka identity yake wazi na kwa ridhaa yake mwenye then awe makini zaidi na michango yake.

Lastly, I sympathise with Hon. Zitto for what happened. Namshauri badala ya kuacha kuchangia, atumie jina bandia kama wengine tunavyofanya!
 
Naona Modereta kasafisha kidogo thread hii..:D Kweli nilishangaa sana kuona upana wa tofauti za watu katika uelewa contents za maandishi.

Ndugu SMU, unalosema ni sahihi kabisa na ndiyo njia inayotumiwa na wengi wetu, ila kama nilivyoonyesha huko nyuma, posts za politicians wanaojulikana waziwazi huwa zina utamu fulani kwa wasomaji wote: wanaomsapoti na wasiomsapoti. In fact politician anapokuwa anatumia jina lake halisi, mara zote huwa wanakuwa makini katika posts zao zaidi ya sisi tunaotumia majina ya bandia kwa sababu politicians wanataka wapate supporters wengi. Ni rahisi kuvumilia iwapo posts zao zimetumika magazetini bila kupindishwa kwa sababu publicity ndicho kitu wanachotaka pia, lakini inaumiza sana iwapo posts hizo zimepindishwa na kuharibu malengo yake.

Jambo kubwa lililokuwa kichwani mwangu wakati ninaanzisha thread ilikuwa ni kuona kama website hii copyright protection. Na kama haina, tujadiliane nini cha kufanya ili kuwe na kitu cha namna hiyo kwa sababu nimeshaona websites nyingi zilizo copyright protection kuzuia matumizi holela ya contents zake bila kibali. Kukiwa na utaratibu huo wa copyright protection, basi itakuwa ni vigumu kwa waandishi wa habari kupotosha posts za hapa kwa vile watatakiwa waonyeshe jinsi wanavyotumia posts hizo kwenye magazeti yao kabla hawajapewa kibali cha kuzitoa magazetini.

The fact kuwa internet content iko easily accessible siyo warrant ya content hiyo kuwa abused kwa namna yoyote. Kumbuka kuwa mwandishi wa habari anapokopi contents za website freely bila ridhaa ya mwenye website hiyo na kuziweka kwenye gazeti lake ambalo anauza kwa faida yake binafsi kipesa, hiyo ni sawa kabisa na mwandishi huyo kuuza kitu alichopata kwa njia ya wizi.
 
Kichuguu,

..waandishi wanaofanya mchezo mchafu wanajua wanachokifanya.

..vilevile hawajali kama watapelekwa kwenye mkono wa sheria na kulipa gharama za makosa yao.

..kuna waandishi wengi sana ambao hawajiheshimu wao wenyewe, na wako ktk taaluma hiyo kutengeneza pesa za haraka-haraka.

..mtindo wa wanasiasa kutumia magazeti kuchafuana umeanzishwa na kundi la wana MTANDAO.

..Jamii Forums inaweza kuwa copyright protected lakini kama tutaendelea kuwa na wanasiasa aina ya MTANDAO ambao ndiyo washirika wa hawa waandishi wasiozingatia maadili basi tatizo hili haliwezi kumalizika.

..kwa kweli taifa linapitia ktk wakati mgumu sana.

NB:

..kwa upande wa Zitto nadhani ingekuwa vema kama angeitisha press conference na kufafanua kilichotokea.

..vilevile ingefaa kama angewashitaki waandishi waliomchafua kule kwenye baraza la habari.
 
Back
Top Bottom