Naona Modereta kasafisha kidogo thread hii.. Kweli nilishangaa sana kuona upana wa tofauti za watu katika uelewa contents za maandishi.
...... Ni rahisi kuvumilia iwapo posts zao zimetumika magazetini bila kupindishwa kwa sababu publicity ndicho kitu wanachotaka pia, lakini inaumiza sana iwapo posts hizo zimepindishwa na kuharibu malengo yake.
Jambo kubwa lililokuwa kichwani mwangu wakati ninaanzisha thread ilikuwa ni kuona kama website hii copyright protection. Na kama haina, tujadiliane nini cha kufanya ili kuwe na kitu cha namna hiyo kwa sababu nimeshaona websites nyingi zilizo copyright protection kuzuia matumizi holela ya contents zake bila kibali. Kukiwa na utaratibu huo wa copyright protection, basi itakuwa ni vigumu kwa waandishi wa habari kupotosha posts za hapa kwa vile watatakiwa waonyeshe jinsi wanavyotumia posts hizo kwenye magazeti yao kabla hawajapewa kibali cha kuzitoa magazetini.
The fact kuwa internet content iko easily accessible siyo warrant ya content hiyo kuwa abused kwa namna yoyote. Kumbuka kuwa mwandishi wa habari anapokopi contents za website freely bila ridhaa ya mwenye website hiyo na kuziweka kwenye gazeti lake ambalo anauza kwa faida yake binafsi kipesa, hiyo ni sawa kabisa na mwandishi huyo kuuza kitu alichopata kwa njia ya wizi.
Kuna sehemu kwenye hii mada Mkuu Invisible alieleza yafuatayo
Kuhusiana na JF:
Ni ngumu kwa mwandishi kuupotosha ukweli kuhusiana na alichoongea mwanasiasa hapa JF, JF si blog kusema haitachukua hatua dhidi ya mtu aliyeupotosha ukweli wa habari flani iliyoandikwa humu endapo itatokea imefanywa hivyo kwa makusudi. Ikitokea mwanasiasa ambaye amejiandikisha hapa kwa jina lake ameandika hapa kitu sensitive na akanukuliwa vibaya na vyombo vya habari na akataka JF tumsaidie kuchukua hatua tunachukua hatua kweli, maana habari yenyewe inakuwa bado ipo hapa na iko public na gazeti linalokuwa limeinukuu vinginevyo itabidi limwombe msamaha mhusika!
Hatuzuii mtu kutumia contents zilizo JF, ila kuzitumia kinyume ya zilivyowekwa ni kosa kubwa..........
Mkuu Invisible......je tunaweza kusema in short maandishi ya hapa JF yako "Copyright Protected?"....au unachozungumza hapo juu ni tofauti?