Maoni yangu dhidi ya "Baadhi ya wananchi wahuni" wa Arusha kujaribu kuzuia wanahabari wa TBC

Umepatia kidogo, ni kweli niliwahi kuwa kiongozi wa CCM, na mzee wangu alikuwa mfurukutwa wa CCM na Mama yangu pamoja na ndugu zangu wote.

Ulichokosea: Tido hakufukuzwa ila mkataba wake uliisha na Serikali ikaamua kutoendelea na mkataba wake. Jingine ni kuwa awepo Tido asiwepo kwangu hanipunguzii tija nafanya kazi kulingana na mkataba wangu wa kazi unavyonielekeza sasa kuwepo au kutokuwepo kwake kunahusiana vipi na mimi?

Mwisho: Usijipendekeze kwa kujifanya unanijua sana, CV yangu iko wazi na kazi zangu zinajieleza uwezo wangu sihitaji wahuni kama nyie kunizungumzia. BTW - CCM ni chama cha siasa kama kilivyo chama kingine huna uwezo wa kuniamualia kwasababu sijawahi kuja kukuomba msaada. So yes i support CCM and CHADEMA pale napoona wanafanya vizuri, wakikosea na likinigusa nitalisema vilevile bila kuogopa vitisho au matusi....that's how politics should be not that of few hooligans.

njoo arusha 'wahuni' wakufunze adabu.
 
Kimsingi mimi sitaki kuingilia mawazo yako lakini kwanza kabisa mimi ni mmoja ya hao wahuni unao wazungumzia tulio wazuiya TBC kufanya kazi yao,na tulikuwa na sababu za msingi za kuwa zuiya, kwanza wajuwe tumewashtukia kuwa wanafanya kazi zao kwa kuwafurahisha baadhi ya watu lakini pili wajuwe hatuwahitaji wala kuwetegemea kwa maana sisi faida yao hatuoni, na hii ni mesege kwa ccm na serikali yake tumechoka vyombo vyetu vya umma kufanya kazi kwa maslahi ya kundi fulani wenye uwezo kipesa ona sasa sisi umetuita wahuni kwa kua sisi ni masikini lakini huoni uhuni unaofanywa na ccm na serikali yake kwakuo wao wameshika mpini sisi ndo tumeshika makeli

Wewe umechangia kiungwana sana, watu kama nyinyi ndo nilihitaji maoni yenu maana hoja lazima ijibiwe kwa hoja. Huwezi kulipuka kisa umetukanwa. Nimekuelewa mkubwa ila kwa upande wangu sikuona kama kuwazuia waandishi ni njia nzuri maana kama habari inawalakini basi vyombo vya sheria viko wazi, kuna Media Council, Jukwaa la Wahariri, Mahakama na sehemu zingine. Hatuwezi kujichukulia sheria mkononi. Siamini kama Mbowe au Dk Slaa anaunga mkono jambo hili pia.
 
likinigusa nitalisema vilevile bila kuogopa vitisho au matusi....
Acha kujidai kuisemea serikali au kuujua mkataba wa TIDo kuliko yeye...una weza kutuambia mkataba wake ulipaswa kuisha lini? Alipaswa kujulishwa lininkuwa TBC hawataendelea na TIDO....je una unaogovyi na CDM kwasababu hawaja kugusa na CCM inaonyesha wana kugusa sana je hayo ndiyo maadili ya uandishi wa habari......!?
 
Pamoja na changamoto zinazoikabili tasnia ya habari nchini bado watanzania wanapaswa kuheshimu na kuthamini huduma ambayo wote tunajua mazingira yalivyo si tu Tanzania lakini bara zima la Afrika linapokuja suala la Uhuru wa vyombo vya habari. Kitendo kilichoripotiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa, baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha ambao kwangu nawaona ni "wakazi wahuni" kujaribu kuwazuia waandishi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kufanya kazi yao kwa kigezo kuwa wanatoa taarifa za kupotosha hazina msingi na walipaswa kutafuta njia nyingine ya kuonyesha kwao kutoridhishwa na utendaji wa shirika hilo. Nachelewa kusema kuwa tabia iliyoanzishwa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA kuwaona kila wasio waunga mkono ni wasaliti haifai na wala haileti picha ya uvumilivu wa kisiasi ambao tungetarajia kuuona ukihubiriwa kwa vitendo na yoyote anajipambanisha na chama au jumuiya makini.

NB: Huu ni mtazamo wangu binafsi kama mwanahabari, wala hakuna mahusiano na itikadi au maslahi ya shirika lolote.

Kaka wafanyie tu kazi hao TBC1 then ufurahie huo ujira wao, jiulize kwanza kwa nini watu wa Arusha awajalalamikia Chanel Ten au ITV? Wewe unafahamika vyema umekwisha wahi kuwa kiongozi wa UVCCM wilaya Ilala, kama unabisha sema, bilashaka kwa uelewa wangu ni miongoni mwa wafanyakazi wa TBC1 waliofurahishwa na kuvunjwa mkataba wa former CEO THido Mhando kwasababu eti ya mchakato majiboni. Uwazi na ukweli ungekuwepo TBC bilashaka usingepost hiyo thread na usingesikia hayo malalamiko kutoka kwa watu wa Arusha. No research no right to speak. please Dotto dwell on research why that for .TBC and not for other TV station.
Pia dotto hizi si zama za chama kimoja na chombo cha habari kimoja bali ni kizazi cha digital, unaweza ukaficha ktk TV lakini watu waka digitalised na ukweli ukaonekana ua kusikika.Post yako imekaa ki politics politics hiv , vp unagombea nini next party election?
 
kama habari inawalakini basi vyombo vya sheria viko wazi, kuna Media Council, Jukwaa la Wahariri, Mahakama na sehemu zingine. Hatuwezi kujichukulia sheria mkononi. Siamini kama Mbowe au Dk Slaa anaunga mkono jambo hili pia.
Vyombo vipi vya sheria vilivyoko chini ya Kikwete haahahahaha...Mwandishi CCM, anafanya kazi TBC iliyoko chini ya CCM, unapelka kesi mahakamani una mkuta jaji CCM, ameteuliwa na CCM haafu unataka haki itendeke zidi ya kada mwenzake alie fanyakazi kwa maelekezo ya boss wa hakimu na mshitakiwa....acha kudanganya umma...
 
Acha kujidai kuisemea serikali au kuujua mkataba wa TIDo kuliko yeye...una weza kutuambia mkataba wake ulipaswa kuisha lini? Alipaswa kujulishwa lininkuwa TBC hawataendelea na TIDO....je una unaogovyi na CDM kwasababu hawaja kugusa na CCM inaonyesha wana kugusa sana je hayo ndiyo maadili ya uandishi wa habari......!?

Ni wazi unataka nikupe faida, mi siisemei serikali uoga wako ndo unakutuma kuwaza haya uliyo nayo. Kwanza kwanini tutishane wakati hapa tunachangia hoja? Are we daring to speak openly? Kuwa mvumilivu kama umeshindwa kutoa majibu kaa chonjo vitisho kwa mtu kama mimi havina nafasi. Unajisikiaje kujadiliana na mtu unaemfahamu badala ya kujificha nyuma ya pazia? Hiyo ni message tosha kuwa vitisho hapa havina nafasi. Jifunze ustaarabu, maana hata mkichukua nchi msidhani mtakuwa na uwezo wa kufanya mnachotaka. Tuambieni kama sera yenu inaendana na hayo makombati ya mgambo.
 
Pamoja na changamoto zinazoikabili tasnia ya habari nchini bado watanzania wanapaswa kuheshimu na kuthamini huduma ambayo wote tunajua mazingira yalivyo si tu Tanzania lakini bara zima la Afrika linapokuja suala la Uhuru wa vyombo vya habari. Kitendo kilichoripotiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa, baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha ambao kwangu nawaona ni "wakazi wahuni" kujaribu kuwazuia waandishi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kufanya kazi yao kwa kigezo kuwa wanatoa taarifa za kupotosha hazina msingi na walipaswa kutafuta njia nyingine ya kuonyesha kwao kutoridhishwa na utendaji wa shirika hilo. Nachelewa kusema kuwa tabia iliyoanzishwa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA kuwaona kila wasio waunga mkono ni wasaliti haifai na wala haileti picha ya uvumilivu wa kisiasi ambao tungetarajia kuuona ukihubiriwa kwa vitendo na yoyote anajipambanisha na chama au jumuiya makini.

NB: Huu ni mtazamo wangu binafsi kama mwanahabari, wala hakuna mahusiano na itikadi au maslahi ya shirika lolote.

Mkuu kama wananchi waliwazuia TBC kufanya kazi ni ujumbe tosha kabisa kwa TBC, sioni haja ya kuwalaumu hao vijana. Unaposema wale wanaoona hawawaungi una maana gani hasa?. Hivi kazi ya chombo cha habari ni kuunga mkono chama cha siasa au kutoa habari na taarifa zilizo sahihi bila ya ubaguzi?. Hii ni ishara kuwa watanzania uvumilivu unaanza kuwashinda hasa kuhusu TBC.

Ni kwamba TBC imekosa credibility kama TV ya Taifa na hivyo kuonekana imejikita katika propaganda za CCM zaidi na hii ni mbaya. Kama wananchi wanashindwa kutofautisha kati ya TBC na Redio uhuru basi ni dhahiri kuna tatizo TBC. Wajiangalie, ama wasitangaze kabisa habari za siasa za chama chochote ama watangaze habari zote bila ya upendeleo.

Hao unaowaita wewe ni wahuni mimi nawaona ni wazalendo maana wamekataa kukaa kimya wakiona kodi zao zinakuwa abused na chombo kisichokuwa na sura ya kitaifa.
 
Mada haizungumzii shirika la TBC hapa pitia upya, mi natoa maoni yangu kama Mtanzania huru kuhusu kitendo cha "BAADHI YA WAHUNI" kuwazuia wanahabari kufanya kazi yao. Usifananishe jina langu na mtazamo wangu kama Raia mwema. Hata ukienda vitani mwandishi haruhusiwi kuguswa hata kama anaripoti upande wa adui yako...hilo la utendaji wa TBC la kwenu na sina mamlaka kulitetea maana ni feedback hivyo linapokelewa kama lilivyo na kufikishwa kwa wahusika wa uboreshaji wa vipindi na habari.

lakini wewe kama raia mwema, kwanini uwa tuhumu we zako kama wahuuni wakati wao pia walikuwa wana wasilisha ujumbe, kwa kukataa kuchukuliwa habari zao na tbc. na hili halijatokea kwa TBC peke yake kumbuka pia waziri mkuu aliwakataa mwanahalisi, wasiingie kwenye mkutano wake alipo kuwa anaongea na waandishi wa habari, je waziri mkuu naye ni muhuni.
 
kwa mara ya kwanza najitokeza hadharani kuchangia katika ukurasa huu wa jamii forum. ukweli ni kwamba naumia mno ninaposikia TBC inaendeshwa kwa kodi za wqananchi kama television ya taifa. sijawahi kuona chombo cha habari kilichojaa unafiki kama TBC. achilia mbali kuwa wachakachuaji wa habari lakini hata wakialika watu wa vyama tofauti na chama tawala wanataka wawaongoze kusema wanayotaka wao, yote kwa yote angalia uchambuzi wa magazeti wanachagua magazeti ya kuchambua, mbaya kuliko yote kuna habari ambazo wanaruka hawazichambui hata kama zimeandikwa kwa herufi za kukoleza, lakini wakiona habari ya kuzodoa chama fulani nje na chama tawala au habari ya kipropaganda ataisoma kwa nguvu kama vile maiki ni mbovu. Cha msingi jirekebisheni, kwani haitaishia kuzuiwa tu, ila itafika kipindi mtapigwa mawe.
 
Mkuu kama wananchi waliwazuia TBC kufanya kazi ni ujumbe tosha kabisa kwa TBC, sioni haja ya kuwalaumu hao vijana. Unaposema wale wanaoona hawawaungi una maana gani hasa?. Hivi kazi ya chombo cha habari ni kuunga mkono chama cha siasa au kutoa habari na taarifa zilizo sahihi bila ya ubaguzi?. Hii ni ishara kuwa watanzania uvumilivu unaanza kuwashinda hasa kuhusu TBC.

Ni kwamba TBC imekosa credibility kama TV ya Taifa na hivyo kuonekana imejikita katika propaganda za CCM zaidi na hii ni mbaya. Kama wananchi wanashindwa kutofautisha kati ya TBC na Redio uhuru basi ni dhahiri kuna tatizo TBC. Wajiangalie, ama wasitangaze kabisa habari za siasa za chama chochote ama watangaze habari zote bila ya upendeleo.

Hao unaowaita wewe ni wahuni mimi nawaona ni wazalendo maana wamekataa kukaa kimya wakiona kodi zao zinakuwa abused na chombo kisichokuwa na sura ya kitaifa.

Nataka kuamini huu ni mtazamo wako na wala siupingi. Je unahisi sikupaswa kuwa na mtazamo wangu pia? Binafsi nitaendelea kuwaona na kuwaita wahuni wote walioshiriki kuwazuia na watakao shiriki huko mbele kuwazuia waandishi wa chombo chochote kufanya kazi zao kwa kigezo cha kutoridhishwa na utendaji wao. Hii haipo duniani popote pale. Mnihukumu kwa kuwaita wahuni niko radhi kupokea matusi kwa malipo ya kauli hii ila sitakaa kimya kuona watu wanapindisha mtazamo wangu kisa nafanya kazi TBC. HAIPO hiyo na kwangu haikubaliki.
 
kwa mara ya kwanza najitokeza hadharani kuchangia katika ukurasa huu wa jamii forum. ukweli ni kwamba naumia mno ninaposikia TBC inaendeshwa kwa kodi za wq
nanchi kama television ya taifa. sijawahi kuona chombo cha habari kilichojaa unafiki kama TBC. achilia mbali kuwa wachakachuaji wa habari lakini hata wakialika watu wa vyama tofauti na chama tawala wanataka wawaongoze kusema wanayotaka wao, yote kwa yote angalia uchambuzi wa magazeti wanachagua magazeti ya kuchambua, mbaya kuliko yote kuna habari ambazo wanaruka hawazichambui hata kama zimeandikwa kwa herufi za kukoleza, lakini wakiona habari ya kuzodoa chama fulani nje na chama tawala au habari ya kipropaganda ataisoma kwa nguvu kama vile maiki ni mbovu. Cha msingi jirekebisheni, kwani haitaishia kuzuiwa tu, ila itafika kipindi mtapigwa mawe.

mwisho kabisa naona mtoa hoja kama hana logic. nimesoma mtiririko mzima wa maoni ya wengine na majibu yake, nimeelewa ana uelewa mdogo mno, akili zilizofungwa, na inawezekena uchache wa madaraka unamsumbua.

ELEWA: Arusha watu hawataki uswahili mwiiiiiingi, wanapenda kuishi in reality. note, uswahili wa tabia na sio uswahili kwa uhalisia.
 
kwa mara ya kwanza najitokeza hadharani kuchangia katika ukurasa huu wa jamii forum. ukweli ni kwamba naumia mno ninaposikia TBC inaendeshwa kwa kodi za wananchi kama television ya taifa. sijawahi kuona chombo cha habari kilichojaa unafiki kama TBC. achilia mbali kuwa wachakachuaji wa habari lakini hata wakialika watu wa vyama tofauti na chama tawala wanataka wawaongoze kusema wanayotaka wao, yote kwa yote angalia uchambuzi wa magazeti wanachagua magazeti ya kuchambua, mbaya kuliko yote kuna habari ambazo wanaruka hawazichambui hata kama zimeandikwa kwa herufi za kukoleza, lakini wakiona habari ya kuzodoa chama fulani nje na chama tawala au habari ya kipropaganda ataisoma kwa nguvu kama vile maiki ni mbovu. Cha msingi jirekebisheni, kwani haitaishia kuzuiwa tu, ila itafika kipindi mtapigwa mawe.

mwisho kabisa naona mtoa hoja kama hana logic. nimesoma mtiririko mzima wa maoni ya wengine na majibu yake, nimeelewa ana uelewa mdogo mno, akili zilizofungwa, na inawezekena uchache wa madaraka unamsumbua.

ELEWA: Arusha watu hawataki uswahili mwiiiiiingi, wanapenda kuishi in reality. note, uswahili wa tabia na sio uswahili kwa uhalisia.
 
kwa mara ya kwanza najitokeza hadharani kuchangia katika ukurasa huu wa jamii forum. ukweli ni kwamba naumia mno ninaposikia TBC inaendeshwa kwa kodi za wq
nanchi kama television ya taifa. sijawahi kuona chombo cha habari kilichojaa unafiki kama TBC. achilia mbali kuwa wachakachuaji wa habari lakini hata wakialika watu wa vyama tofauti na chama tawala wanataka wawaongoze kusema wanayotaka wao, yote kwa yote angalia uchambuzi wa magazeti wanachagua magazeti ya kuchambua, mbaya kuliko yote kuna habari ambazo wanaruka hawazichambui hata kama zimeandikwa kwa herufi za kukoleza, lakini wakiona habari ya kuzodoa chama fulani nje na chama tawala au habari ya kipropaganda ataisoma kwa nguvu kama vile maiki ni mbovu. Cha msingi jirekebisheni, kwani haitaishia kuzuiwa tu, ila itafika kipindi mtapigwa mawe.

mwisho kabisa naona mtoa hoja kama hana logic. nimesoma mtiririko mzima wa maoni ya wengine na majibu yake, nimeelewa ana uelewa mdogo mno, akili zilizofungwa, na inawezekena uchache wa madaraka unamsumbua.

ELEWA: Arusha watu hawataki uswahili mwiiiiiingi, wanapenda kuishi in reality. note, uswahili wa tabia na sio uswahili kwa uhalisia.

Ni furaha yangu kukufanya utoe maoni yako kwa mara ya kwanza, hii ndo sifa ya mwandishi, kuwachokonoa watu waseme yanayowasibu. Jitahidi utumie lugha ya kistaarabu ili usiangukie kwenye mikono ya matusi yangu maana sitakuacha upite bure bure:heh:
 
kwenda zako kule, mara ya mwisho umelipa kodi lini? Kuna watu humu ni mzigo tu, kodi hawalipi, kura hawapigi kazi kunyodoka...tatizo unaongozwa na Bange hii ndo taswira nayoipata kutoka kwako:A S-fire1:

Du kweli unaupeo mdogo wa kuelewa mkuu,watanzania wote wanalipa kodi,kwani wewe unapoenda kununua bidhaa mahali unakua umeshalipia kodi kabisa,sio lazima uchukue hela na kupeleka TRA.
 
Vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa dola.TBC ni chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi za walala hoi wa kitanzania nawe ukiwemo, TBC inatakiwa kuwa watchdog kwa serikali yake na kuionesha serikali nini imekosea, nini ilitakiwa kufanya na nini inatakiwa kufanya kutokana na matakwa ya umma wa tanzania lakini imekuwa kinyume chake. lakini chombo hiki kimetumika na kutumiwa na viongozi wetu kufanikisha ajenda zao kama udhalimu, upotoshaji wa dhahiri kwa umma n.k. mfano Issue ya AFANDE SELE 'Moro'jana.
 
Umepatia kidogo, ni kweli niliwahi kuwa kiongozi wa CCM, na mzee wangu alikuwa mfurukutwa wa CCM na Mama yangu pamoja na ndugu zangu wote.

Ulichokosea: Tido hakufukuzwa ila mkataba wake uliisha na Serikali ikaamua kutoendelea na mkataba wake. Jingine ni kuwa awepo Tido asiwepo kwangu hanipunguzii tija nafanya kazi kulingana na mkataba wangu wa kazi unavyonielekeza sasa kuwepo au kutokuwepo kwake kunahusiana vipi na mimi?

Mwisho: Usijipendekeze kwa kujifanya unanijua sana, CV yangu iko wazi na kazi zangu zinajieleza uwezo wangu sihitaji wahuni kama nyie kunizungumzia. BTW - CCM ni chama cha siasa kama kilivyo chama kingine huna uwezo wa kuniamualia kwasababu sijawahi kuja kukuomba msaada. So yes i support CCM and CHADEMA pale napoona wanafanya vizuri, wakikosea na likinigusa nitalisema vilevile bila kuogopa vitisho au matusi....that's how politics should be not that of few hooligans.

Bilashaka mtu mzima una jazba, sijakuamulia, hujaniomba msaada na pia na sikujui sana kama unavyodhani ila nimesema records zinaonyesha umekwisha wahi kuwa kiongozi uvccm ilala.
Pole sana kiongozi ndio ukubwa huo.
 
Back
Top Bottom