Dotto, ulikuwa wapi muda wote huu? Nimefurahishwa sana na hitimisho lako ama kweli wewe ni think tank, kama kuna mtu atashindwa kukubali kwa hiyo post ya mwisho basi huyo ni mahututi wa mawazo. Nakushauri ujiunge na chadema wewe ni asset muhimu sana pale bungeni. Good to go utafika mbali sana ukiendelea kuwa visionary wa sina hii.
Soma vizuri maelezo acha kupindisha maelezo yangu.
Pamoja na changamoto zinazoikabili tasnia ya habari nchini bado watanzania wanapaswa kuheshimu na kuthamini huduma ambayo wote tunajua mazingira yalivyo si tu Tanzania lakini bara zima la Afrika linapokuja suala la Uhuru wa vyombo vya habari. Kitendo kilichoripotiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa, baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha ambao kwangu nawaona ni "wakazi wahuni" kujaribu kuwazuia waandishi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kufanya kazi yao kwa kigezo kuwa wanatoa taarifa za kupotosha hazina msingi na walipaswa kutafuta njia nyingine ya kuonyesha kwao kutoridhishwa na utendaji wa shirika hilo. Nachelewa kusema kuwa tabia iliyoanzishwa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA kuwaona kila wasio waunga mkono ni wasaliti haifai na wala haileti picha ya uvumilivu wa kisiasi ambao tungetarajia kuuona ukihubiriwa kwa vitendo na yoyote anajipambanisha na chama au jumuiya makini.
NB: Huu ni mtazamo wangu binafsi kama mwanahabari, wala hakuna mahusiano na itikadi au maslahi ya shirika lolote.
Kwako wewe busara ni kutoa habari za kuipendelea ccm???Nakubaliana na wewe ila kwa mtazamo wangu sikuona kama ni jambo la busara.
Mkuu mi sipo hapa kujadili habari zinazoletwa na TBC, na wala siko hapa kulitetea shirika hilo maana hiyo si kazi yangu na wala sihusiki. Inawezekana nimetumia kauli iliyowaudhi wengi lakini hii hainifanyi niwe mdogo na kukubali matusi yanayoletwa kishabiki. Mimi ni binadamu, nina hisia na pia sio malaika hivyo kama mtu akinilitea maneno ya Kunya na mimi nayajua. This is where we dare to speak openly, nimeyapokea matusi yote bila jazba na wenzangu nao wayapokee ya kwangu kwa mikono miwili.

Huyu jamaa anawaita wakazi wa arusha wahuni kisa wanaiunga mkono cdm,hizi njaa za wanahabari sijui ztaisha lini?