Maoni ya watu wa Kyela na Mbeya kwa ujumla kuhusu afya ya Dr Mwakyembe

Wakati mwingine wabongo tumezidi mno kulalamika, tufike hatua tuwe kama wenzetu wa nchi za Kiafrika like Senegal, rais anataka kugombea muhula 3 wana nchi wameingia mtaani na nina hakika kitaeleweka tu, sisi kila siku maneno tu na kulalamika, Mwakyembe pamoja na kutoa taarifa Polisi kuwa wanataka kumuua, polisi walikaa kimya na sisi tukaa kimya, wamemuwekea sumu sasa, polisi wanadanganya na tunaendelea kukaa kimya, huenda hata ana weza kufa (Mungu apishilie mbali) still tutakaa kimya, kweli nchi hi ni ya mabwege na ndo maana ccm wanaendelea kutalawala, sipati picha kama ccm ndio kinge kuwa chama tawala Kenya, Zambia au Senegal ni nini kingetokea.
 
Kwanza kabisa namuombea kwa Mungu apone haraka. Ukweli Mwakyembe ni mmoja kati ya wabunge niliokuwa nawakubali na alikuwa anawakilisha hasa matakwa ya watanzania na ninaamini amefanya mabo mengi mazuri kwa nchi hii. Sasa ni wakati wake kuwaomba radhi wa Tz kwa dhambi aliyoifanya yeye na Sitta kuwaficha ukweli wa Tz kuhusu richmond kwa heshima ya kulinda CCm na serikali yake. Mshahara wa dhambi ni mauti afanye toba ya kweli na mwenzake sitta kuueleza umma wa wa Tz nini hasa walichoficha, vinginevyo tutaendeklea kumuombea heri apone lakini hiyo dhambi itaendelea kumtafuna
 
Jamani tuchangie hoja vizuri,Mm huyu ni mbunge wangu,sioni sababu ya kuhusisha ugonjwa wa mbunge wangu Dr H Mwakyembe na CCM, yeye mwenyewe na wapiganaji wa Ufisadi wakina Sita hawajawahi kutuambia na kulitangazia taifa kuwa CCM ndiyo imemdhuru Dr H Mwakyembe waliomdhuru ni kikundi cha watu wachache ambao wao wanawaita mafisadi na wala si CCM jamani kama huna cha kuchangia kaa kimya usitake kupotosha watu kwa utashi wako wa kisiasa kyela ni jimbo la CCM damu damu kama wapinzani hamuamini njoeni tutawathibitishia kwa vitendo sisi huku huwa hatutaki mtu mwenye porojo!

huwezi kutenganisha ugonjwa wa mwakyembe na chama mfu cha ccm...unaposema kikundi cha watu sita unamanisha nini? Ccm bila hao watu unaowasema haipo...kwanza kyela ipi unayosema na ccm damudamu? Wewe either huelewi au ni mvivu wa kufikiri...katika uchaguzi wa 2010 slaa aliongoza jimbo la kyela katika nafasi ya urais...kwanza nahisi wewe sio mtu wa kyela bali umetumwa na hao mafisadi na hakika waambie hujatukuta...mara ngapi mwakyembe amelaumu jeshi la polisi kwa kutofuatilia njama zake...wewe unadhani hawa polisi nani anayewazuia wasizifuatilie njama za kuuawa kwa mwakyembe kama hiyo serikali iliyo chini ya ccm....CCM IMEKUFA KYELA...wana kyela tumeamka...mim niko huku ipinda katika kijiji cha lupaso na diwani wetu ni wa chadema sasa utasemaje ccm damudamu huku
...ccm inahusika 100% na ugonjwa wa mwakyembe...kiama chao ni 2015...APONE HARAKA MBUNGE WETU MWAKYEMBE
 
Namuombea apone aje aendelee kutimiza ahadi jimboni, kubwa likiwa ni barabara ya Kikusya hadi Matema beach
 
hauna lolote wewe,na sizani kama wewe ni mwana kyela,chuki na wivu zimekutawala.acha roho mbaya ndugu.
Wewe mi ni mwanakijiji cha ikolo. Nimesoma ngamanga na ikolo. Tumechoka kunywa maji na vyura. Omberike apo nkamau gwango
 
Taratibu dogo, naona una chuki binafsi na Mwakyembe, tena chki kubwa kama aliyonayo Manumba. Hapa kinachojadiliwa ni maradhi yanayomkabili mbunge wa Kyela, ambao kila mtu anamsikitikia. Yaweza kumkuta yeyote anayeonyesha uzalendo wa nchi yake. Rudia kujikumbusha ripoti aliyotoa kuhusu Richmond.

Vinginevyo utakuwa hutendi haki si tu kwa Mwakyembe peke yake ila kwa wa tanzania woote ambao hafaidi matunda ya rasilimali zao. Wewe ni Fred EL nini?
Mi ni mkulima wa mpunga saiz nipo napandikiza huku nsesi, ongeni ukweli khs huyu mwakyembe. Napenda apone haraka labda atakuja tubu dhambi zake alizoifanyia tz na wanakyela. Mungu mbariki mwakyembe jirani yangu
 
Wana Kyela waseme kama kweli bado wana imani na ccm inayotaka kumwua mbunge wao,watangaze rasmi kuachana na hayo majambazi wajiunge na wazalendo wenzao kukomboa taifa letu!

Kumbe ww mchicha mwiba, aaaaaaaaaaaaaaaaaaah !

 
Jamani, nimeguswa sana na hali aliyo nayo Mbunge wetu wa Kyela, Mh. Mwakyembe. Kusikitishwa huku hasa kunatokana na mazingira mazima yanayozunguka hali aliyonayo mbunge wetu huyu, ambaye zaidi ya ubunge bali ni mtanzania mzalendo ambaye siku zote ametetea si tu maslahi ya wana kyela bali maslahi ya uma kwa ujumla dhidi ya waporaji wakuu wa mali za nchi hii.

Nimeanzisha uzi huu, ili wana kyela, tutoe mtazamo wetu wa ugonjwa wa mbunge wetu na jinsi serikali inavyolishughulikia suala hili. Na kisha tuweze kupata way forward ktk kujaribu kunusuru maisha ya mbunge wetu. Na pia tujiandae kama lolote linatokea ni kwa namna gani tutawaadhibu wale wote ambao mazingira na ushahidi mwingiene utaonesha kuwa wapo nyuma ya tatizo hili la mbunge wetu.

Jamani huyu ni mbunge wetu, ni lazima tumuoneshe kuwa tunampenda na tunampigania kama ambavyo amekuwa akitupigania siku zote za yeye kuwa mbunge wetu.

Tujowe awammweto, abando habha bhikolonda okotokinela. Tobaboneswe okote tokaja bando ba kokenelwa kwa namna hii.

Mwanzilishi wa thread hii anajifanya ni mtu wa kutoka Kyela lakini kile alichoandika mwisho wa uzi wake sio kinyakyusa ambayo ndio lugha ya watu wa huko hivyo anadhihilisha kuwa anajalibu kupima reaction ya wanaKyela juu ya mbunge wao!! Nia yako sio nzuri na ninakuhakikishia wewe na hao unaowatumikia hamtafaulu katika harakati zenu.
 
Inafaa sana kuchwachukulia hatua wahusika hawa wauaji na wale waliozembea wajibu wao
 
mh!!! nangojea kw ahamu kuona kama kweli kyela wataiacha ccm wakati mapololo yako ccm, na mbeya kwa wa ubwabwa na pilau wakati wa uchaguzi acha tu! nakumbuka persen yule balozi wa denmark hpa nchini miaka ile alishindwa kukabidhi mradi wa maji pale kyela kwa kuwa nyama ya ngombe haikuwepo kwenye sherehe
 
Mojawapo ya maeneo ambayo ni misukule ya ccm ni kusini, amkeni kataeni hili balaa ona sasa watu wenu mashujaa wanateketea na bado mnaichekelea ccm
Mkuu mapenzi ya chama hayachagui sehemu unakotoka unataka tuamini kuwa CDM ni chama cha Watu wa Kaskazini na Wakatoliki?
 
Jamani tuchangie hoja vizuri,Mm huyu ni mbunge wangu,sioni sababu ya kuhusisha ugonjwa wa mbunge wangu Dr H Mwakyembe na CCM, yeye mwenyewe na wapiganaji wa Ufisadi wakina Sita hawajawahi kutuambia na kulitangazia taifa kuwa CCM ndiyo imemdhuru Dr H Mwakyembe waliomdhuru ni kikundi cha watu wachache ambao wao wanawaita mafisadi na wala si CCM jamani kama huna cha kuchangia kaa kimya usitake kupotosha watu kwa utashi wako wa kisiasa kyela ni jimbo la CCM damu damu kama wapinzani hamuamini njoeni tutawathibitishia kwa vitendo sisi huku huwa hatutaki mtu mwenye porojo!

GOd me!hujui unachokisema au kiwango chako cha unafiki kimepindukia sana kiasi cha nyeusi kiita nyeupe mchana kweupe.ushauri wangu uwe unaenda kwenye maombezi
 
Inanikumbusha sakata la Aboud Jumbe Mwinyi na watu wa Kyela miaka ilee ya Mwalimu Nyerere
Unakumbuka eh ,msoma mashairi kipofu mzee Ahmad(kama nimekumbuka vizuri)maarufu Kipofu wa mkoa ndie aliyechafua hali ya hewa pale bomani,nilikuwa mdogo wakati ule lakini bado nina kumbukumbu na lile tukio Kyela ili zizima na baba zetu wakasomwa hadi gereza la Kawetele kwenye baridi kali(Kyela ni joto kama Dar)lakini wapi baba zetu ndio wakawa sugu
 
Mi hata sioni umuhimu wa ubunge wa huyu mnafiki. Kwa kweli wanakyela hawana cha kukukumbuka zaidi ya kukwonea huruma kibinadam. Umeshindwa kuturudishia maji yetu, mabomba yapo, umeshindwa kutawanya umeme vijijin, afya, shule, barabara da kwa kweli alipoachia kasyupa ndo had sasa. Tulikwambia ulipokuja kijijin kwetu uame ccm ukasema unaipenda sn. Mku najua we ni mbishi na mnafki sn ndo vinavokumaliza. Hatuna cha kumskitikia make kila kijiji anachoenda wanampiga mawe na vilevile analana za wazee akumbuke sku alipokusanya hela za kuludisha maji na kulala mbele nazo.



Hizi ni chuki binafsi, nadhani wewe ni mmmoja wa waliokosa ubunge. Hizo kazi ni za mbunge au? Ni vizuri ujifunze kazi za maendeleo zinaletwa na nani la sivyo ubunge hautauweza
 
Jamani mbona mnachanganyikiwa mara mnamgombania huko Kyela mara CCM, CDM nk huyu Mwakyembe amefundisha sheria Mlimani hakuchagua mnyakyusaacheni matatizo yenu yeye amewafumua Mafisadi na wote walioleta EPA Dowans, kagoda nk mbona humu JF tulikuwepo na kuzipata hizo document hatukufanya lolote
hata YESU aliuwawa kwa kuwatetea mataifa
mwacheni Mwakyenbe
 
Wewe mi ni mwanakijiji cha ikolo. Nimesoma ngamanga na ikolo. Tumechoka kunywa maji na vyura. Omberike apo nkamau gwango
Yeap_na huko ikolo,ngonga,lugombo,katumba etc,..ndio hali ya maji sio nzuri kabisa,wakati mabomba yapo vizuri kabisa,...anyway_sipendi kuhusisha hili na siasa....ila time will tell.
 
Back
Top Bottom