EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
TUNDU LISSU
Mwanasehria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, alisema mkuu wa wilaya ana mamlaka ya kuamuru mtu aliyefanyakosa mahali ambako hakuna polisi akamatwe.
Kama kuna polisi kwenye eneo la kosa hayo mamlaka hawezi kuwa nayo, na kama akitoa amri hiyo atakuwa anawajibika kutoa maelezo na sababu za kumkamata mtu huyo kwa hakimu wa wilaya.
"Alichokifanya DC wa Kinondoni ni uvunjaji wa sheria na tutamshughulikia hadi ataikimbia hiyo wilaya," alisema Lissu.
KIBATALA
Akizungumzia kuhusu mamlaka ya mkuu wa wilaya kutoa amri ya kukamatwa mbunge, mwanasheria Peter Kibatala alisema amefurahi kutokea kwa kesi hiyo na anaomba suala hilo kwenda mahakamani kama shtaka la jinai.
Alisema kesi hiyo itasaidia kuhoji mamlaka ya mkuu wa wilaya na namna ambavyo anayatekeleza.
"Vyovyote iwavyo lazima tuhakikishe tunawasilisha malalamiko kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ili kupata uamuzi wa nini hasa mipaka kati ya serikali na maafisa wake na wabunge hasa wa upinzani," alisema Kibatala.
FREDERICK KIHWELO
Kwa upande wake mwanasheria wa mbunge huyo, Frederick Kihwelo alisema jambo la msingi katika suala hilo ni kuhakikisha cheo hicho kinaondolewa ili kiweze kuwaacha polisi wafanye kazi zao kwa uhuru.
"Inasikitisha kuona mkuu wa wilaya ni kada wa CCM, mjumbe wa siasa wa wilaya wa CCM na ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hivyo ni bosi wa OCD na ofisa usalama wa wilaya," alisema.
Aliwataka wale waliopewa mamlaka hayo kuhakikisha wanatumia mamlaka hayo kwa busara badala ya kutumia nguvu na jeuri.