Naungana na muleta hoja na wachangiaji wote kuwa shule za kata ni tatizo. Naomba nitoe angalizo kuwa tusiwe na mtazamo hasi tu bali tuzione kuwa zinaweza kuwa ni nyenzo nzuri ya kutusogeza mbeme. Tusisahau tulikotoka: kumbuka azimio la UPE, ktk azimio hili wale waliokuwa wamemaliza drs laa 7 waliitwa kufundisha shule za msingi na wanavijiji walihizwa kujenga madarasa- naskumbuka nulisoma drs la 1 kwenye jengo la udongo lililoezekwa kwa nyasi na hivi sasa ni degree2. Kule india wamefanya maendeleo makubwa ktk elimu kwa kuwa na shule km hizi za kata, wao hawakuishia hapo bali walifanya hivihivi hata kwa taasis za elimu ya juu. Kwa maoni yangu huu ni wakati muafaka kupendekezza nini kifanyike na si kubeza tu kwani sehemu kubwa ya hawa wanaoenda shule za kata hawana option nyingine.
Gama unapotaka kufanya biashara ama shughuli yoyote lazima ufanye kitu inaitwa visible study! Kwanza tunasema hawa lengo lao halikuwa baya bali walikurupika! Walocpy mahala na wakapaste hapa! Unafungua shule huna manpower unaita shule! Umeandaa walimu wa kutosha! Matokeo wakaleta walimu vodafasta!
Pamoja na kutaka watoto wa wakulima wapate elimu! Walitakiwa waweke nayo mazingira ya kusoma yawe ya uhakika.
Hata hawa wazazi wakihamasishwa kujenga mabweni wanaweza kuitikia wito na wakajenga lakini hawawezi kupata waalimu!
Wanapeleka waalimu watoto ambao akisimama na mwalimu hakuna nidhamu maana vijana hawa kutongozana sio ajabu! Yaani walikuwa nao juzi tu kamaliza kapelekwa vodafasta anarudi anataka kumfundisha huyu reproduction! Wakati ashakum sio matusi weshavuliana nguo!
Mimi sina hiyana sana ila serikali nayo itimize wajibu wake. Ipeleke walimu wa kutosha huku kwenye kata na pia tuhamasishe mazingira mazuri ya kusoma na kwa walimu wapewe mazingira ya kufanya kazi. Kuna walimu najua wanaka over 35km na wanaenda na kurudi kwao kila siku. Atafundisha saa ngapi huyu! Unamkuta saa tatu na nusu mpaka saa nne ndo anatokwa na mijasho anawahi kipindi! Atafundisha kweli! ama atapiga blah blah siku iende akakamue ngombe ya mwenzawazimu mwisho wa mwezi!
AM, kuna tatizo gani jwenye vodafasta?. Tuna mifano mizuri ya shule moja maaufu hapa nchini ambayo iliajiri waalim wengi kutoka kenya ambao hawakuwahi kuingia drs la ualimu na ilikuwa maarufu with very high schoool fee. Unakumbuka jinsi azimio la UPE lilivyo punguza kiwango cha kutojua kusoma na kuandika?,pendekeza, unafikiri shule hizi zisingejengwa watoto hawa wangekuwa wapi?
AM, kuna tatizo gani jwenye vodafasta?. Tuna mifano mizuri ya shule moja maaufu hapa nchini ambayo iliajiri waalim wengi kutoka kenya ambao hawakuwahi kuingia drs la ualimu na ilikuwa maarufu with very high schoool fee. Unakumbuka jinsi azimio la UPE lilivyo punguza kiwango cha kutojua kusoma na kuandika?,pendekeza, unafikiri shule hizi zisingejengwa watoto hawa wangekuwa wapi?
sikuwah kulisikia neno shule za kata b4 2006 na kati ya shule zilizotajwa na mimi nayoifahamu KIKUYU SEC iliyopo Dodoma huwez kuiita shule ya kata hata coz haikuwa ktk mpango huo.Hawa hawatoki shule za kata za kiwete. Ni zile shule za kata za awali. Mbona wengine tumesoma shule hizo hizo. Japo umaarufu wa jina hili umekuja kipindi cha huyu mbayuwayu. Zilikuwa zinajitahidi sana. Lakini sasa huwezi kuzitofautisha na hizi za sasa. Hali zake ni mbaya sana.