Shule hizi zisifutwe. Tujaribu kuangalia faida zake baada ya miaka kadhaa ijayo. Uwepo wake utawafanya wanajamii husika pamoja na serikali kuwajibika. Walimu na vitendea kazi vimekuwa vikiongezeka japo si kwa kasi sana, ila ni swala la muda na jitihada kwa wadau wote.
Wanafunzi wengi wa sasa ni vilaza na hawajali. Jaribu kutizama hata kwa shule zilizokuwa zikisifika awali zi wapi sasa. Katika mazingira ya mjini kwenye vyombo vingi vya habari mwanafunzi anashindwa kumjua hata waziri mkuu!
Wanafunzi wamekuwa walevi, wahuni na wazazi wengi hawafuatilii maendeleo ya watoto wao wakidhani ni kazi ya walimu peke yao.
Ni bora ndege mmoja mkoni kuliko wengi msituni.
Shule za kata zisifutwe.
Nami nawasilisha.
Babkey unafahamu Wizara ya afya huendesha opresheni na kufungia vituo vyote vya aftya ambavyo havikidhi vigezo ili kuokoa maisha ya watu wanaopatya huduma hapo?
Unadhani haifai pia hatua kama hii ikachukuliwa kwa shule hizi za kata kufungiwa mpaka pale shule inapokidhi vigezo (sio kwa serikali kufanya hivyo peke yake bali na wananchi kushiriki) ili kuokoa vijana kutokuwa mambumbumbu zaidi?
Mwaka jana 80% wamefeli, mwaka huu sitazamii tofauti, na mwakani na labda baada ya miaka hiyo kadhaa ya kupima, je huoni ni wengi tutakuwa tumewaua kitaaluma?
Kwa nini zisifungiwe kwa muda (SIO ZIFUTWE TAFADHALI) hadi zikidhi?
Naendelea kusimama pale pale. Kwenye swala la afya haliitaji mzaha hata kidogo, vivyo hivyo kwenye elimu. Tukumbuke moja ya sababu za kufeli 2010 ni kwa wanafunzi kutochujwa kidato cha pili.
Pia hamasa inakuwepo baada ya kuonekana udhaifu flani. Ni rahisi zaidi kuhamasisha jamii ikiwa inaona uhalisia kuliko kubaki na nadharia pekee.
Inauma kuona wanafunzi wanafeli, lakini inauma zaidi wakibaki kuzura mitaani. Wengi waliosoma shule za serikali wanajua taabu iliopo. Wanafunzi wengi hutoka kwa jitihada binafsi. Walimu walituambia kwa tunapata 10-25% kutoka kwao, nyingine tuhangaike wenyewe.
Ni ukweli usio pingika kuwa pamoja na kuwa shule za kata zina matatizo mengi sana na hata kuitwa magofu,ni dhahiri kuwa vijana wano maliza huko upeo umebadilika na kuelewa ni nini maana ya siasa na hii ndio sababu kuu ya kura za ccm kupungua uchaguzi uliopita na sidhani kwa hali hii kama ccm itavuka 2015