Maoni kuhusu uwekezaji katika Kampuni ya uzoaji takataka

Quraish Hussein

New Member
Mar 6, 2023
2
1
Ndugu Zangu Habarini

Nina wazo la kufungua kampuni ya ukusanyaji na uzoaji taka ngumu katika sekta mabali mbali kama taasisi, mashule, majumbani nk.

Lakini naomba kujua ni zipi changamoto za mradi huu pia zi zipi fursa za kukuza mradi huu. Pia nataka kujua namna ya uendeshaji wa mradi huu.

Kwasababu, napata changamoto kujua maamuzi sahihi pale ambapo, ukiwa mtaani au katika jamii, unapokea taalifa za huduma hafifu ya uzoaji taka katika jamii hizo, hapo unajua kwamba kuna uhitaji wa kuwekeza katika huduma hii. Lakini changamoto kinzani inakuja kwamba hapa mjini hiyo huduma inapatikana na makampuni yapo yanayotoa huduma hii, je changamoto inayowafanya wamiliki wa makampuni haya kutoa hizo huduma ipasavyo ni nini?

#biashara #ujasiriamali #Takangumu #Uchumi #uwekezaji #biashara
 
Back
Top Bottom