Uwekezaji zaidi kutoka China kuleta kuwanufaisha watanzania na uchumi wa Tanzania

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
fdsafsafa.jpg


Mwishoni mwa mwezi Aprili mamlaka za Tanzania ziliualika ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China kutoka mkoani Guangdong nchini China kwa lengo la kufahamisha fursa za uwekezaji nchini Tanzania, wakati Tanzania ikiendelea na utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya viwanda. Mamlaka hizo ziliualika ujumbe wa China kutokana na ukweli kwamba, China imekuwa moja ya wawekezaji muhimu na nchi inayochochea ipasavyo maendeleo ya viwanda nchini Tanzania.

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ongezeko la uchumi wa Tanzania limekuwa likichochewa na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI), ambalo kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2021 na Shirika la maendeleo ya biashara na viwanda duniani (UNCTAD) thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja nchini Tanzania kwa mwaka 2021 ilikuwa ni dola za kimarekani milioni 922 zikiwa zimeongezeka kwa asilimia 35 ikilinganishawa na dola za kimarekani milioni 695 za mwaka 2020.

Kwa mujibu wa ripoti ya kila mwezi iliyotolewa mwezi Machi mwaka huu na kituo cha uwekezaji cha Tanzania (TIC), China ni chanzo kikuu cha uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni ikifuatiwa na Marekani, na uwekezaji mkubwa kutoka nje uko kwenye sekta za ujenzi wa majengo, uzalishaji viwandani na sekta ya usafirishaji. Kwa watu wanaofahamu vizuri maendeleo ya sekta za ujenzi na uzalishaji viwandani za Tanzania, wanafahamu kabisa kuwa China imekuwa ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya sekta hizo. Mabadiliko makubwa yaliyotokea katika miaka ya hivi karibuni hasa kutokana na ujenzi wa majengo mapya ya ghorofa ya kisasa yanayoendelea kuonekana katika mji wa Dar es salaam na kwenye mingine ya Tanzania, pamoja na miundombinu mingi ya barabara na usambazaji wa huduma kama vile maji na Tehama, yanatokana na makampuni ya China.

Uamuzi wa mamlaka za Tanzania kuualika ujumbe kutoka mkoani Guangdong, China unatokana na ukweli kwamba, mkoa huo una nguvu kubwa ya kiuchumi na una maendeleo makubwa katika sekta za ujenzi na uzalishaji viwandani. Uchumi wa Guangdong (GDP trilioni 2.98) unakaribia kuwa sawa na wa Uingereza (GDP trilioni 3.4) na ukiwa umeuzidi ule wa Italia (GDP trilioni 2.71), hali inayofanya mkoa huo peke yake kuweza kuwa nguvu kubwa ya kuhimiza maendeleo ya karibu sekta zote nchini Tanzania.

Licha ya kuwa Tanzania imekuwa ni moja ya nchi 10 duniani zenye maendeleo ya kasi kiuchumi duniani katika muongo mmoja uliopita, ukweli ni kwamba bado Tanzania iko nyuma sana kwenye sekta za uzalishaji. Ndio maana Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji cha Tanzania (TIC) Bw. John Mnali, alisema makampuni kutoka Guangdong yanayokaribishwa zaidi kuwekeza nchini Tanzania, ni yale yatakayowekeza kwenye sekta za mafuta na gesi, uchimbaji wa madini, utalii, kilimo, ufugaji, uvuvi na Tehama. Mbali na kuwa mkoa wa Guangdong ni tajiri, lakini pia umepiga hatua kuwa kubwa kwenye maendeleo ya sekta zote hizi.

Ziara ya ujumbe wa wawekezaji kutoka mkoa wa Guangdong nchini Tanzania, unatokana na ushirikiano kati ya Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania (TIC) na ubalozi wa Tanzania nchini China. Kama wawekezaji kutoka mkoa wa Guangdong au mikoa mingine ya China wataweza kuingia na kuwekeza Tanzania kama kituo cha uwekezaji cha Tanzania (TIC) kinavyotarajia, hii ni itakuwa ni habari nzuri kwa Tanzania na watanzania. Kwani licha ya serikali ya Tanzania kuweza kupata mapato ya kodi, watu wa Tanzania wanaweza kupata ajira, na hata uzalishaji na mchango wa sekta hizo kwenye maendeleo ya uchumi wa Tanzania vitaongezeka.
 
Back
Top Bottom