Maoni juu ya kilichotokea kwenye matokeo ya Shule ya Sheria (Law School of Tanzania)

Sep 4, 2022
8
9
Habari Ndugu wadau,

Napenda kutoa maoni yangu juu ya kile kilichotokea katika shule ya sheria
Nianze kwa kuuliza je, mfumo wetu wa elimu upo vizuri!?

Je, mfumo wa elimu unaruhusu mchakato wa namna gani pindi tunapoomba nafasi za elimu katika vyuo vikuu?

MAONI
01. Mfumo haumuandai mwanafunzi kukabiliana na yale anayoyakuta chuoni mwanafunzi wa PCB anaweza kusoma biashara

Je, ni sahihi Tahasusi zilege kuandaa watu wa namna flani na sio liwe daraja tu la kuelekea chuo kikuu.

02. Mfumo ni huria sana. Sidhani kama ni sahihi kwa mtu kuweka matokea tu na kuchaguliwa katika kozi fulani inapaswa mfumo uruhusu mtu uyo kufanyiwa interview kabla ya kuingia kwenye kozi husika ili kuona kama anakidhi viwango sidhani kama matokeo yanatosha kumfanya mtu achukue kozi fulani.

03. Mfumo unaruhusu hisia na sio professinalism. Mfano unakuta mtu kaaplly vyuo vitano koz tano tofauti labda biashara kwingine uhandisi kwingine elimu kwingine uongozi na hata sheria je! uyu mtu yupo seriuos na anavyovitaka au anafanya bahati nasibu.

MWISHO
Kilocho tokea ni funzo kwamba mfumo wetu wa elimu ni mbovu sio tuu kwenye sheria bali katika kila idara serikali kwa kupitia wizara ya elimu ishughulikie hili.!
 
wanafunzi wa zama hizi ni wavivu hawataki kosoma ila wanataka kufaulu !!!

Wengi wao wanasoma ili wapate degree au hata masters ili waajiriwe au wapandishwe vyeo.....matokeo yake ni udanganyifu mtupu.

unamkuta mtu ana masters lakini kichwani hamna kitu...mweupeeee......
 
Back
Top Bottom