matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,653
- 15,481
Sio kila unachokiomba, Sio kila kanisa linachokiomba Mungu ndio huwa anajibu. Mengine yanayokiuka kanuni za maombi hujibiwa na mashetani.
Mfano: Ile tabia ya kuombea watu wafe, wapigwe visukari,presha, wafirisike, wateseke, wasambaratike na kudhaliliika hata kama wamekukosea vipi, maombi haya huwa Mungu haangaiki nayo bali mashetani.
Kazi ya Mungu ni kuokoa, kuponya, kurekebisha na kutoa uzima kisha uzima tele. Kazi ya shetani ni kuua, kutesa, kufirisi, kushusha ma kudhalilisha.
Katika Mapambano yetu ya kiroho hatuombei watu mabaya, tunaombea roho na majini yaliyojificha nyuma yao na kuongoza ubaya ulio ndani yao. Wengi wanatumika bila kujua. Mkomavu kiroho haombei mtu mabaya. Kama amekuchosha sana mwambie Mungu amnyenyekeze. Mungu ananjia maelfu ya kunyenyekeza watu ikiwemo hata kuruhusu wapumzike mavumbini ili amani itawale.
Kabla hujakurupuka na kukurupushwa na imani mwendokasi za kibishoo za kisasa za kukamia watu na kuwatakia mabaya, Mwambie Mungu akufunulie aina ya ya vita unavyopigana ili ujue mahali sahihi pa kuelekeza mashambulizi yako kwa ufanisi.
Luka 9:54 ~56
Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Ni hayo tu.
Karibu kwa neno lolote. Kama umeelewa andika amina.