Maombi yanayojibiwa na mashetani

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,373
Sio kila unachokiomba, Sio kila kanisa linachokiomba Mungu ndio huwa anajibu. Mengine yanayokiuka kanuni za maombi hujibiwa na mashetani.

Mfano: Ile tabia ya kuombea watu wafe, wapigwe visukari,presha, wafirisike, wateseke, wasambaratike na kudhaliliika hata kama wamekukosea vipi, maombi haya huwa Mungu haangaiki nayo bali mashetani.

Kazi ya Mungu ni kuokoa, kuponya, kurekebisha na kutoa uzima kisha uzima tele. Kazi ya shetani ni kuua, kutesa, kufirisi, kushusha ma kudhalilisha.

Katika Mapambano yetu ya kiroho hatuombei watu mabaya, tunaombea roho na majini yaliyojificha nyuma yao na kuongoza ubaya ulio ndani yao. Wengi wanatumika bila kujua. Mkomavu kiroho haombei mtu mabaya. Kama amekuchosha sana mwambie Mungu amnyenyekeze. Mungu ananjia maelfu ya kunyenyekeza watu ikiwemo hata kuruhusu wapumzike mavumbini ili amani itawale.

Kabla hujakurupuka na kukurupushwa na imani mwendokasi za kibishoo za kisasa za kukamia watu na kuwatakia mabaya, Mwambie Mungu akufunulie aina ya ya vita unavyopigana ili ujue mahali sahihi pa kuelekeza mashambulizi yako kwa ufanisi.

Luka 9:54 ~56
Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.

Ni hayo tu.
Karibu kwa neno lolote. Kama umeelewa andika amina.
 
Sio kila unachokiomba, Sio kila kanisa linachokiomba Mungu ndio huwa anajibu. Mengine yanayokiuka kanuni za maombi hujibiwa na mashetani.

Mfano: Ile tabia ya kuombea watu wafe, wapigwe visukari,presha, wafirisike, wateseke, wasabaratike na kudharirika hata kama wamekukosea vipi, maombi haya huwa Mungu haangaiki nayo bali mashetani.

Kazi ya Mungu ni kuokoa, kuponya, kurekebisha na kutoa uzima kisha uzima tele. Kazi ya shetani ni kuua, kutesa, kufirisi, kushusha ma kudhalilisha.

Katika Mapambano yetu ya kiroho hatuombei watu mabaya, tunaombea roho na majini yakiyojificha nyuma yao na kuongoza ubaya ulio ndani yao. Wengi wanatumika bila kujua. Mkomavu kiroho haombei mtu mabaya. Kama amekuchosha sana mwambie Mungu amnyenyekeze. Mungu ananjia maelfu ya kunyenyekeza watu ikiwemo hata kuruhusu wapumzike mavumbini ili amani itawale.

Safi
 
Clear Malisa anasema adui yako muombee mabaya
Mathayo 5:43-44,46-47

[43]Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

[44]lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

[46]Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

[47]Tena mkiwasalimia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
 
Usimsikilize Malisa. Msikilize Yesu.
Tatizo waumini wa kisasa mnapenda watu kuliko kauli za Mungu.
Leo umeongea Kitu kizuri Sana matunduizi ni kitu kila siku nakipigania "Upendo"..Hujui tu

Ukikosa Upendo hata unacho Sali,Imani yako ni bure...

1 Wakorintho 13:13

[13]Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
 
Sio kila unachokiomba, Sio kila kanisa linachokiomba Mungu ndio huwa anajibu. Mengine yanayokiuka kanuni za maombi hujibiwa na mashetani.

Mfano: Ile tabia ya kuombea watu wafe, wapigwe visukari,presha, wafirisike, wateseke, wasabaratike na kudharirika hata kama wamekukosea vipi, maombi haya huwa Mungu haangaiki nayo bali mashetani.

Kazi ya Mungu ni kuokoa, kuponya, kurekebisha na kutoa uzima kisha uzima tele. Kazi ya shetani ni kuua, kutesa, kufirisi, kushusha ma kudhalilisha.

Katika Mapambano yetu ya kiroho hatuombei watu mabaya, tunaombea roho na majini yakiyojificha nyuma yao na kuongoza ubaya ulio ndani yao. Wengi wanatumika bila kujua. Mkomavu kiroho haombei mtu mabaya. Kama amekuchosha sana mwambie Mungu amnyenyekeze. Mungu ananjia maelfu ya kunyenyekeza watu ikiwemo hata kuruhusu wapumzike mavumbini ili amani itawale.

Kabla hujakurupuka na kukurupushwa na imani mwendokasi za kibishoo za kisasa za kukamia watu na kuwatakia mabaya, Mwambie Mungu akufunulie aina ya ya vita unavyopigana ili ujue mahali sahihi pa kuelekeza mashambulizi yako kwa ufanisi.

Luka 9:54 ~56
Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.

Ni hayo tu.
Karibu kwa neno lolote. Kama umeelewa andika amina.
hapa nimekuelewa Mkuu,
nenda hapo kwa mama n'tilie mwambie akupe soup na chapati 7 za moto nakuja kulipa
 
Leo nimejifunza kitu na naamini kitanisaidia..kuna mtu anamuombea mwenzake afe nikawa najiuliza ni sawa hii..mbona kama MUNGU hayupo hv? Ila ni kweli yule mtu anapata misukosuko sana...

Lkn leo nimeelewa kuwa baadhi ya maombi hujibiwa na mashetani hasa maombi mabaya ahsanteni sana!
 
Mathayo 5:43-44,46-47

[43]Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

[44]lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

[46]Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

[47]Tena mkiwasalimia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
Je, mnao waamini ya kuwa taifa teule la wana wa Mungu israeli wanawapenda adui zao!? (Wapalestina)
 
Mkuu Sijawahi Kuwa upande wa Kidini wowote wala sijawahi kuwa Katika upande wowote wa Waabuduo mabaya..

Instead naisoma biblia kama Refference ya Muongozo wangu na Quran pia Na Bhavagad Gita na Mahabarat pia na kitabu chochote kinacho Hubiri Amani Kwa watu wote na kurudisha Undugu TulioUharibu kwa Kudhani Tuko tofauti na kujidanganya kwa kujiwekea matabaka ya Kijinga na kipumbavu

" Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu."(
Quran 41:33-34 (Suratul Fuss'ilat)

kwenye Bhagavad Gita pia kuna Aya inasema..

"Yule anayehisi furaha na huzuni ya wengine, aliye na utulivu wa ndani, asiye na ubinafsi, na anayetambua uwepo wa Mungu kwa kila kiumbe, huyo ni mtu aliye katika hali ya upendo na urafiki wa kweli." (Bhagavad Gita 12:15)

Pia

"Yeyote aliye na mawazo ya upendo kwa wote, asiye na chuki kwa yeyote, mwenye amani na uvumilivu, upole na unyenyekevu, aliye na akili imara, moyo ulio safi, na ambaye hujitolea kwa kujidhibiti na akili thabiti, anaweza kuitwa mtu aliyejitolea kwa Mungu." (Bhagavad Gita 12:13)

Namalizia kwa Kuquote mstari ndani ya Biblia..

1 Wakorintho 13:2-4,6,13

"Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo."

SIJUI MKUU UMENIELEWA HAPO..
HAKUNA TAIFA TEULE LENYE KUFURAHIA UHARIBIFU ..
WAWE WAARABU AU WAYAHUDI AU WATANZANIA
 
Unakuta mtu anajifanya mlokole anasali balaa kila weekend anakesha makanisani. Ila MUNGU anamletea mtihani mdogo tu wa fukara kuja na shida dukani kwake na kuomba kukopeshwa kitu kidogo aidha chakula au pesa ili akatatue shida na yeye ataufeli huu mtihani vizuri sana kwa kujibu kuwa SINA au haitawekezekana biashara sio nzuri.

Kumbe moyoni ni ile roho ya nasaidia masikini ili nipate nini sasa? Hapo akienda kwa mwamposa anatoa pesa za sadaka kede wa kede.

Aisee.
 
Back
Top Bottom