Manyara: Ujenzi wa Barabara ya lami ya km 25 kutoka Labbay hadi Haydom sasa unaanza rasmi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) inatarajia kujenga kwa kiwango cha lami miradi mitatu mikubwa ya barabara mkoani Manyara ambayo itaunganisha mkoa huo na mikoa ya Jirani.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema hayo leo tarehe 19 Mei 2023 mji mdogo wa Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara kwenye Utiaji Saini wa Ujenzi wa Barabara ya lami ya km 25 kutoka Labbay hadi Haydom.

Ametaja miradi ya barabara ambayo imepangwa kutekelezwa na bajeti ya mwaka 2023/2024 inayotarajia kusomwa Bungeni Jumatatu ya Tarehe 22 Mei 2023 ni pamoja na kilometa 389 za lami kutoka Karatu Mkoani Arusha, kwenda Mbulu na Haydom mkoani Manyara, Sibiti, Lalago- Maswa mkoani Simiyu.

Mhandisi Kasekenya ameongeza kuwa Mradi wa pili wa barabara utakaojengwa ni km 424 kutoka Kiberash wilayani Handeni mkoani Tanga, kupitia Kibaya mkoani Manyara, Goima, Chemba, Dosee, Farkwa, Kwa Mtoro, mkoani Dodoma hadi mkoani Singida na tatu ni km 430 kutoka Kongwa mkoani Dodoma, Kibaya wilayani Kiteto, Losinyai wilayani Simanjiro mkoani Manyara hadi Mbuda mkoani Arusha.

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng: Rogatus Mativila akitoa taarifa fupi wakati wa kutia saini mkataba na Kampuni ya JIANGXI GEO –ENGINEERING GROUP LIMITED kwa ajili ujenzi wa barabara ya lami ya km 25 kutoka Labbay hadi Haydom unaogharimu shilingi bilioni 42.271 amesema kilomita hizo 25 zinakamilisha kilomita 50 kati ya kilomita 113 za barabara ya Serengeti Southern bypass zilizopo ndani ya mkoa wa Manyara.

Eng: Mativila ameongeza "Nitoe Shukrani za dhati kwa Serikali yetu kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huu, Wakala ya Barabara (TANROADS) itasimamia utekelezaji wa mradi huu na kuhakikisha kuwa Mkandarasi anazingatia viwango vya kiufundi (Technical Standards) na mradi unakamilika kwa wakati, nitoe wito kwa Mkandarasi kufanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu ili kazi zote zikamilike ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango na gharama zilizokubalika.
1684519956798.jpg
1684519956753.jpg
1684519958442.jpg
1684519958413.jpg
1684519959241.jpg
1684519959213.jpg
1684519960004.jpg
 
Back
Top Bottom