Manji apewa saa 48 Kuhama Quality Plaza

Kweli hiki sasa ni kituko......yaani huyu jamaa ni gwiji katika kumwaga mapesa kwa kilabu cha Yanga lakini inapokuja kuipa serikali kilicho chake awa na kigugumizi........nina wasiwasi hata TRA kule hatekelezi wajibu wake kulingana na sheria...............
 
ni nini faida ya kumtaka ahame na si kumtaka alipe deni
vinginevyo afilisiwe mali inayolingana na thamani ya deni?
 
Wala tusimcheke jamaa hapa ndivyo tunaona akili za watu waliopo kwenye position kadhaa. Watu wanapigwa na viyoyozi na kukaa kwenye kiti vya helikopta wakati huo huo mshikaji anatumia udhaifu wao ku-make MONEY
 
Huyu si ndo yule tajiri mfadhili wa yanga na kama nakumbuka kuna wakati alilipia fedha wa watazamaji wote wapenzi wa yanga waliokwenda kuangalia mechi ya yanga na timu ambayo siikumbuki.Manji ni mtu anayeheshimika katika jamii kama ni kweli alipe fedha hiyo ili ziweze kwenda kututatua matatizo ya wananchi wa chini.
 
Grandma's farm..........$$$$$$:target:
 
Imekuwaje wamemuachia miezi yote hio bila kulipa kodi mpaka deni limekuwa kubwa hivyo? Sasa akishahama watampeleka mahakamani kudai hio kodi au ndio wamemalizana?
 
Huyu si ndo yule tajiri mfadhili wa yanga na kama nakumbuka kuna wakati alilipia fedha wa watazamaji wote wapenzi wa yanga waliokwenda kuangalia mechi ya yanga na timu ambayo siikumbuki.Manji ni mtu anayeheshimika katika jamii kama ni kweli alipe fedha hiyo ili ziweze kwenda kututatua matatizo ya wananchi wa chini.

Anaheshimika kwa lipi Mkuu?? Mbona unatatizika kirahisi namna hiyo? Tuhuma zake za ufisadi hujazisikia ukalinganisha na michango ya Yanga?
 
ni nini faida ya kumtaka ahame na si kumtaka alipe deni
vinginevyo afilisiwe mali inayolingana na thamani ya deni?

Serikali ya kishoga hiyo... Nenda mwambie asogee yakhe! .. nakuambia ondoka yakhe. Badala ya kutoa amri ya kumfikisha mahakamani, eti anatakiwa aondoke. Aondoke tuu!
Eee Mungu ibariki nchi yangu Tanzania!
 
Manji hakufanya utapeli. Haya na matokeo ya conspiracy kati yake na baadhi ya watu PSPF kwa sababu haiwezekane makubaliano yawe loose kiasi hicho kama watu hawakuwa compromised. Hii mifuko ya Pensheni inahitaji kuangaliwa kwa macho mawili na hasa kuhusiana na procurement zao na investment options wanazozi-pursue. kwa sasa wamejikita zaidi katika real estate badala ya kupanua customer base yao, na hii yote ni kwa sababu kwenye procurement ndo kuna KITU KIDOGO. Matokeo yake returns za hizo nyumba wanazojenga au kununua ni kidogo sana. Mfano, makusanyo ya pango kwa PSPF ni shilingi bilioni moja tu kwa mwaka wakati makusanyo ya michango ya wanachama kwa sasa ni shilingi bilioni 17 kwa mwaka. Ku-recover bilioni 40 ya kununua quality plaza itachukua miaka 40 wakati ukiongeza wanachama kiasi hicho unakipata ndani ya miaka miwili. Wasiwasi wangu ni pale soko la nyumba litakaposhuka. Hela za wanachama zitarudije?
 
Cha kushangaza lawyer wa PSPF ni miongoni mwa waliokuwa lawyers wa manji.
 
Manji si wa kufukuzwa namna hiyo. Jamani wakuu walishasema wakikamata mafisadi uchumi wa nchi utayumba, maana mafisadi wanaushikilia.
Danganya toto hiyo wakuu
 
Back
Top Bottom