Ta-kibombo
JF-Expert Member
- Dec 4, 2015
- 632
- 463
Kahama ni moja ya miji inayokua kwa kasi sana nchini. Pamoja na hilo, nadhani pia ni moja ya miji michafu sana nchini. Mitaro mingi ya barabarani inatiririsha maji machafu ya bafuni na yakwenye chemba za vyoo. Kuna baadhi ya mitaa ata ukipita kwa haraka unapokewa na harufu kali. Hivi idara ya Afya ipo kweli? Imeshindwa kweli kukabiliana na ili tatizo tena lipo wazi kabisa ata kwa mtu ngumbalu anaona?
Baadhi ya mitaa ukipita karibu kila nyumba mifuniko ya chemba za vyoo na bafu ipo wazi inaachwa maji yanatapika kuingia kwenye mitaro. Kata ya majengo ndio imekithiri zaidi hii tabia japo karibu mitaa yote ya huo mji kuna hii tabia.
Pili, usafi wa mazingira kiujumla hali ni mbaya, usafi unafanyika katikati ya mji pekee ambalo ni eneo dogo ila pembezoni unaweza tapika kwa uchafu. Wananchi badilikeni jalini mazingira yanayowazunguka, haingii akilini mama ntilie anauza chakula mbele yake kumejaa uchafu na maji ya bafu yanatiririka.
Wahusika wajibikeni.