Maneno Matatu.

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,515
6,489
Samahani wandugu, najua hili si jukwaa la lugha lakini haya maneno nadhani yanahusu sana hapa MMU.

Naomba kwa anayejua anisaidie tofauti ya haya maneno matatu ili niweze kuyatumia ipasavyo;

1. Zinaa
2. Uasherati
3. Uzinzi.
 
Zote ni kitu kimoja. Zinatofautiana viwango tu.
Uasherati ipo juu.
 
Zinaa- inatokana na neno Zini. Zinaa ni 'nomino' na Zini ni 'kitenzi'
Uasherati- Ni kwa mtu ambae hajaoa au kuolewa kufanya ngono.
Uzinzi- mtu kutoka nje ya ndoa yake.
(mawazo yangu tu)
 
uko sahihi ila niongeze kidogo kuwa uzinzi ni tabia ya kufanya zinaa. kimsingi hata uasherati ni aina mojawapo ya uzinzi. so uzinzi unacover vyote. hata mtu amabye hajaoa akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine ni kusema kuwa anafanya mapenzi na mtu asiye mke wake na hivyo ni uzinzi pia. na huu ndio uliopewa jina uasherati ila bado kimsingi ni uzinzi uleule. kuna mtu ametaka kujua na ngono pia ni nini? ngono ni tendo la kijamiiana ama coitus kwa kingereza. ni neno laini kutamka kwa kiswahili kwa mujibu wa maadili yetu ila kuna neno gumu kidogo kutamka ama kuandikika na naamini unalielewa. mara nyingi tabia ya uzinzi hujuimuisha ama hukamilishwa na kukolezwa na zawadi ya tendo ngono, ila in some circumstances waweza kuwfanya uzinzi bila ngono kufanyika. kibiblia, tendo lolote la kunajisi imani pia hufananishwa na uzinzi, mfano kuabudu sanamu nk
 
Asanteni kwa ufafanuzi, ila nilivyowaelewa(sijui kama kichwa changu kigumu) ni kwamba kwa ujumla maneno hayo matatu tafauti, katika matumizi yake hakuna tofauti.
 
Zinaa- inatokana na neno Zini. Zinaa ni 'nomino' na Zini ni 'kitenzi'
Uasherati- Ni kwa mtu ambae hajaoa au kuolewa kufanya ngono.
Uzinzi- mtu kutoka nje ya ndoa yake.
(mawazo yangu tu)

Kwanza nimekutandika na thanks moja matata sana kwa majibu yako mazuri ila muheshimiwa mjumbe nina swali la nyongeza,kwa mnyumbulisho huo wa uzinzi na uasherati,zinaa inaangukia wapi katika hayo makundi mawili au inatengeneza kundi la tatu.
 
uko sahihi ila niongeze kidogo kuwa uzinzi ni tabia ya kufanya zinaa. kimsingi hata uasherati ni aina mojawapo ya uzinzi. so uzinzi unacover vyote. hata mtu amabye hajaoa akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine ni kusema kuwa anafanya mapenzi na mtu asiye mke wake na hivyo ni uzinzi pia. na huu ndio uliopewa jina uasherati ila bado kimsingi ni uzinzi uleule. kuna mtu ametaka kujua na ngono pia ni nini? ngono ni tendo la kijamiiana ama coitus kwa kingereza. ni neno laini kutamka kwa kiswahili kwa mujibu wa maadili yetu ila kuna neno gumu kidogo kutamka ama kuandikika na naamini unalielewa. mara nyingi tabia ya uzinzi hujuimuisha ama hukamilishwa na kukolezwa na zawadi ya tendo ngono, ila in some circumstances waweza kuwfanya uzinzi bila ngono kufanyika. kibiblia, tendo lolote la kunajisi imani pia hufananishwa na uzinzi, mfano kuabudu sanamu nk

Nenda kaangalie mwenyewe,nimetafuta jinsi ya kukutwangia thanks mbili imeshindikana ila ulikuwa unastahili.

Kama nimekuelewa vizuri ni kama haukubaliani na mnyumbulisho alioutoa Babkey hasa baada ya kuonesha kuwa zinaa ndo shina huku uzinzi ikiwa ni tabia ya kufanya zinaa,je hakuna maneno yanayotofautisha kati ya zinaa ya aliye katika ndoa na ya yule ambaye hayuko katika ndoa.Kwani mfano ulioutoa wa uasherati haukusema kama mwanamke nae hajaolewa au yuko ndani ya ndoa.Utanisamehe wengine ni slow learners.
 
.............. hata mtu amabye hajaoa akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine ni kusema kuwa anafanya mapenzi na mtu asiye mke wake na hivyo ni uzinzi pia. ................

Nenda kaangalie mwenyewe,nimetafuta jinsi ya kukutwangia thanks mbili imeshindikana ila ulikuwa unastahili.

Kama nimekuelewa vizuri ni kama haukubaliani na mnyumbulisho alioutoa Babkey hasa baada ya kuonesha kuwa zinaa ndo shina huku uzinzi ikiwa ni tabia ya kufanya zinaa,je hakuna maneno yanayotofautisha kati ya zinaa ya aliye katika ndoa na ya yule ambaye hayuko katika ndoa.Kwani mfano ulioutoa wa uasherati haukusema kama mwanamke nae hajaolewa au yuko ndani ya ndoa.Utanisamehe wengine ni slow learners.

asante che kalizozele kwa kunikumbusha, nilipitiwa tu kuweka bayana. ni kwamab ile sentensi kwenye post yangu kama nilivyinukuu hpo juu ilipaswa kusomeka kuwa "hata mtu amabye hajaoa/kuolewaakiwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine ni kusema kuwa anafanya mapenzi na mtu asiye mke/mume wake na hivyo ni uzinzi pia"

kimsingi uzinzi ni tabia ya kufanya zinaa na kitenzi cha vyote viwili ni neno kuzini na shina la vyote ni neno "zini" ni sawa na kusema ukulima-kulima-lima, nafikiri sasa umenielea japo mi si mtaalamu sana wa sarufi ya kiswahili
 
Back
Top Bottom