mwanatumaini
Senior Member
- Sep 2, 2013
- 161
- 54
nami nakuunga mkono,mpaka sasa sijaona anayeweza kumfunika NYERERE
Sijaridhika bado na uzito wa Nelson Mandela ukilinganisha na baadhi ya viongozi wengine wambao wamefanya makubwa katika ukombozi wa bara la Afrika na baadhi ya mambo muhimu ulimwenguni. Jambo la pekee kwa Mandela ni kufungwa kwa miaka 26, na baada ya kufunguliwa makubaliano ya ANC ni kumpa nafasi ya kuongoza nchi ambapo alidumu kwa awamu moja na kuamua kuachia ngazi pengine sababu ya matatizo ya kiafya ndio alitaka upweke asibughudhiwe. Zaidi ya kupigania haki za Waafrika huku kusini hakuna tofauti na wapigania uhuru wengine katika bara hili.
Kwa kulinganisha na mmoja ambaye amekuwa katika vichwa vya waafrika wengi Julius Nyerere naona kwa mtazamo wangu Nyerere yuko juu zaidi kwa juhudi kubwa alizofanya kupigania ukombozi wa bara la Afrika, kwani alijitolea bila hofu na hata umoja wa Afrika kuweka makao makuu ya ukombozi nchini Tanzania. Hata vyama vya wapigania ukombozi makao yao yalikuwa Tanzania, hali kadhalika ANC maskani yao yalikuwa Tanzania, karibu na mji kasoro bahari (Morogoro) ambako sasa ni chuo kikuu cha kilimo (Sokoine University).
Naweza kutafsiri kama mataifa ya magharibi yamefanya jitihada kubwa kumkuza zaidi kwa kile kinachoonekana kujaribu kufunika yale yaliyofanywa nao kipindi cha ubaguzi kwa vile walikuwa ni wazungu wenzao. Lakini kupima kwa vigezo halisi binafsi naona Nyerere yuko juu zaidi ya Mandela, na tena kuna wengine wengi tu wenye kustahili heshima zaidi yake hapa Afrika kuliko yeye. Mataifa ya magharibi yametuteka nasi tumefuata wayatakayo.