FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,392
- 4,469
Wala usijaribu kulinganisha kati ya Mandela na Nyerere.....
Kwa ufupi tu, Nyerere alikuwa bonge la dikteta, aliyevuruga maisha na hata kuuwa waliompinga kisiasa.
Uchumi wa nchi ulikufa kabisa... No infrastructure, barabara zilikufa, viwanda vilifilisika, na biashara ilikufa simply because alikuwa ana experiment na ujamaa!
Elimu aliivuruga vuruga hadi kufikia ilipo sasa...
Maisha ya Mtanzania yalikuwa duni, shida (hakuna hata vyakula) na ya kudhalilishwa kila siku. Waliofanya kazi kwa nguvu walipokonywa mali zao na kufungwa. Waliokuwa waadilifu walifukuzwa kazi kwenye redio!!! Walioneemeka ni mamluki ya waliomshangalia na kumshabikia kisiasa tu.... Bonge la dikteta Nyerere
Amekaa kitini miaka 23, lakini aliiacha nchi masikini mara kumi zaidi ya alivyoikuta....
Utamlinganisha na Mandela huyu???
Hamjajuwa na hamtotaka kujua siri na ukweli wa nchi ilivyoendeshwa chini ya Nyerere. Alitafuta misifa ya eti African liberation, imetusaidia nini Watanzania? Zaidi ya kuishi umasikini, elimu mbovu na sasa kupigana kabali??
Hisia zako zinatosheleza tunaosoma ulichoandika tuone sababu za kwa nini wewe upo hapo ulipo na Nyerere alikuwa pale alipokuwa.
Ni kukosa fadhila kumtaja Mandela na harakati zake bila ya kumtaja Nyerere...ingawa najua wapo wengine pia....ila Mwalimu ana nafasi kubwa kwenye hili.
Wengi mnaongozwa na hisia binafsi mlizonazo kwa kuwa tu si waumini wa UMOJA....UPENDO na KUJALI WENGINE....sioni ajabu kwa baadhi yenu kumuona mtu aliyekuwa tayari kutumia kila alichonacho kwa ajili ya wengine kwamba hakufanya kitu kwa kuwa tu matumbo yenu hayakushiba yale matamanio mnayoendeshwa nayo....matamanio yaliyojaa ubinafsi..uchoyo...chuki...husda...roho mbaya...na ukosefu wa fadhila.
Hebu endeleeni kufuatilia shughuli pale qunu....nadhani Nyerere wanamtaja....