Jerrymsigwa
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 14,082
- 8,340
Eti amekuzwa na Wazungu,what a stupidity?
Uliza mtu yoyote toka South Africa mweusi atakwambia ni nini
So mi ndio stupid ama aje boss? Angalia mihemko yako isikwaze watu wengine mkuu
Eti amekuzwa na Wazungu,what a stupidity?
Uliza mtu yoyote toka South Africa mweusi atakwambia ni nini
Unataka kusema Nelson Mandela amekuza uchumi wa S.Afrika?
Nadhani ulinganifu sahihi kati ya hawa viongozi ni mchango wao ktk kuikomboa afrika na hapo ndio Nyerere atabaki kuws mtu wa pekee.
jukwaa la siasa hili!!! Hmmmm...
Em nirudi zangu mapenzini mie... Mmu oyee
Anastahili mandela kuheshimiwa alifungwa miaka 26 kwa ajili ya kupinga ubaguzi wa rangi ili kuwakomboa waafrica weusi africa ya kusini, aliwasamehe waliomfunga nani anaweza? Wazazi wake walimuomba kuachana na harakati za siasa lakini mandela alisimamia msimamo wake anatisha, maisha yake ya ujana yameishia gerezani hakupata muda wa kukaa na familia na kuwatunza wazazi wake kama mtoto anavyotakiwa kufanya kwa wazazi rest in peace mandela dunia inakila sababu ya kukukumbuka uliletwa na mungu kwa kusudi malumu
Sikuwahi kusikia hii!
Kwanza, kuwalinganisha viongozi uliowataja na Nyerere ni makosa. Nyerere hawezi kulinganishwa na yeyote kwa kuwa wakati wake ulikuwa na changamoto zake ambazo haziwezi tena kuwepo sasa. Pili, waraka ulioambatanishwa hapa is a poor work of art . Nilipinga barua pepe iliyosambazwa siku za nyuma ikimhusisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM na Waziri wa Mambo ya Ndani......this too doesn't worth a penny!This document tells us a lot about these friends of ours how close they are to Nyerere.
Umedandia gari kwa mbele mjomba, lengo langu nilikuwa nauliza kama nyerere alifungwa Jela? acha kudandia issue zilizokupita umri!komaa kiakili ndugu yangu, unapotumia muda wako kuandikia mambo finyu namna hiyo utajichelewesha sana. Typo ndogo kama hizo siyo jambo la kushanganza na kukufanya usielewe maana ya post nzima. Iwapo kwenye post hiyo. hayo maneno mawili tu ndiyo uliyoelewa basi inabidi ujitahidi sana kukomaza akili zako kuweza kuona mengine.
Sijaridhika bado na uzito wa Nelson Mandela ukilinganisha na baadhi ya viongozi wengine wambao wamefanya makubwa katika ukombozi wa bara la Afrika na baadhi ya mambo muhimu ulimwenguni. Jambo la pekee kwa Mandela ni kufungwa kwa miaka 26, na baada ya kufunguliwa makubaliano ya ANC ni kumpa nafasi ya kuongoza nchi ambapo alidumu kwa awamu moja na kuamua kuachia ngazi pengine sababu ya matatizo ya kiafya ndio alitaka upweke asibughudhiwe. Zaidi ya kupigania haki za Waafrika huku kusini hakuna tofauti na wapigania uhuru wengine katika bara hili.
Kwa kulinganisha na mmoja ambaye amekuwa katika vichwa vya waafrika wengi Julius Nyerere naona kwa mtazamo wangu Nyerere yuko juu zaidi kwa juhudi kubwa alizofanya kupigania ukombozi wa bara la Afrika, kwani alijitolea bila hofu na hata umoja wa Afrika kuweka makao makuu ya ukombozi nchini Tanzania. Hata vyama vya wapigania ukombozi makao yao yalikuwa Tanzania, hali kadhalika ANC maskani yao yalikuwa Tanzania, karibu na mji kasoro bahari (Morogoro) ambako sasa ni chuo kikuu cha kilimo (Sokoine University).
Naweza kutafsiri kama mataifa ya magharibi yamefanya jitihada kubwa kumkuza zaidi kwa kile kinachoonekana kujaribu kufunika yale yaliyofanywa nao kipindi cha ubaguzi kwa vile walikuwa ni wazungu wenzao. Lakini kupima kwa vigezo halisi binafsi naona Nyerere yuko juu zaidi ya Mandela, na tena kuna wengine wengi tu wenye kustahili heshima zaidi yake hapa Afrika kuliko yeye. Mataifa ya magharibi yametuteka nasi tumefuata wayatakayo.
nakubaliana na wewe ila nashukuru mungu waafrika tunaelewa ukwewli na hatukubali kupelekwa kibubusa na western mediaMandela aliyepigania usalama wa wazungu ni mtu muhimu kwa mataifa ya magharibi, lakini Mugabe anayepigania haki za waafrika walio wengi ni mtu hatari kwa nchi za magharibi, hii ndio hali halisi na ndicho kinachoendelea katika sakata hilo la kuenziwa Mandela ambaye inaonekana kama mdau mmoja alivyosema ni kuongeza mafuta kwenye utambi.
Mugabe tu anampita mandela kwa ushujaa kwa kuwapokonya ardhi wazungu na kuirudisha kwa waafrika. Nyerere ndio engine ya ukombozi afrika. Hakuna kiongozi wa ukombozi afrika ambaye hapakua na mkono wa nyerere kumtengeneza; kuanzia kina mondlane, samora, augustino neto, sam nujoma, oliver tambo hadi mandela mwenyewe. Msisahau oliver tambo ndiye kiongozi aliyeongoza anc miaka yote mandela akiwa jela nakufariki dunia kabla ya ukombozi wa SA. Muhimu kila kiongozi amecheza role yake na kwa wakati wake. Ila historia ikitendewa haki, nyerere ndie baba wa ukombozi afrika.
haya bwana we subiri kuabudiwa, wakati wenzio wana fanya kazi, ukifanya vizuri watu wata sema tu, sio kwa kupiga kampeni au magazeti, China walifanya kazi wakafikia hapo walipo, vivyo hivyo kwa wajerumani, leo hii kenya tunasema wana strong economy eac nk walifanya kazi hawakutumia mitandao au magazeti kufikia hapoJambo la kawaida kujadili matukio ya wakati kwa kuwa yanatufanya kama kioo kujitazama tulikotoka, tulipo na tunakoenda, wakati wenzetu wanajadili haya mambo katika vyombo mbalimbali ya kimataifa sisi tunasema wanaoleta mada za kujadili wana wivu. Tutafika kwa mwendo huu?
haya bwana we subiri kuabudiwa
Hii ni nafsi kwetu kujifunza namna wenzetu walivyofanikiwa kumjengea mazingira Madiba kuabudiwa hivyo wakati sisi tuhahangaika kutafuta kasoro kadhaa kuwadhalilisha viongozi wetu ambao wamefanya makubwa si kwa nchi yetu tu ila kwa bara zima la Afrika na dunia.