Mamlaka za Uteuzi wa Viongozi zinadhihirisha wazi kuna tatizo kwenye utaratibu wa "Vetting"

Kwa muda wa miaka 3 ya utawala wa Rais Samia, kumekuwa na Teuzi na Tenguzi au kubadilishwa kwa nafasi za Kiutawala kwa wanaoteuliwa na wakati mwingine bila hata kuelezwa sababu.

Samia amekuwa akiteua na kutengua au kuwarejesha watu walioondolewa kazini kwa sababu mbalimbali. Na wapo ambao ameendelea kuwakumbatia licha ya kuwa na kashfa mbaya kiuongozi.

Baadhi ya Viongozi hao ni pamoja na Makonda, Chalamila, Biswalo Mganga, Kingai na wengine wengi.

Hapa tu inaonesha aidha kuna shida katika idara ya Usalama wa Taifa eneo la Mahusiano kwa Umma au Rais anapuuza makandokando yaliyopo nyuma ya anaowateua kwa maslahi yake binafsi.
Kwa tulipofika hii nchi sio salama kabisa tunadanganyana tu.
 
Hata uwe na CV iliyoshiba pages 1000 lakini kama hauna connection sahau teuzi Mkuu.

Nape aliteuliwa Waziri akiwa hana hata Shahada ndiyo amepata kama sio mwaka jana basi mwaka juzi.

Kwahiyo hakuna Vetting inafanyika zaidi ya Connection tu
Waziri siyo lazima awe Mtaalam. Siyo hitaji la kisheria wala kikatiba.
Hata hivyo, waziri akiwa msomi na Mtaalam wa fani husika kwenye wizara, itaongeza ufanisi.
 
Waziri siyo lazima awe Mtaalam. Siyo hitaji la kisheria wala kikatiba.
Hata hivyo, waziri akiwa msomi na Mtaalam wa fani husika kwenye wizara, itaongeza ufanisi.
Sahihi Mkuu, ila kuna haja hiki kipengele kibadirishwe kimepitwa na wakati
 
Kwa muda wa miaka 3 ya utawala wa Rais Samia, kumekuwa na Teuzi na Tenguzi au kubadilishwa kwa nafasi za Kiutawala kwa wanaoteuliwa na wakati mwingine bila hata kuelezwa sababu.

Samia amekuwa akiteua na kutengua au kuwarejesha watu walioondolewa kazini kwa sababu mbalimbali. Na wapo ambao ameendelea kuwakumbatia licha ya kuwa na kashfa mbaya kiuongozi.

Baadhi ya Viongozi hao ni pamoja na Makonda, Chalamila, Biswalo Mganga, Kingai na wengine wengi.

Hapa tu inaonesha aidha kuna shida katika idara ya Usalama wa Taifa eneo la Mahusiano kwa Umma au Rais anapuuza makandokando yaliyopo nyuma ya anaowateua kwa maslahi yake binafsi.
Waache wale keki mubashara!
 
Nani kakuambia usalama ndo wanafanya vetting. Usalama ndo wanaongoza kuingia Kwa vetting za undigunaization nitajie usalama 1 unaemjua ambaye ni ginius au chuo unachokijua kina walimu wakufundisha huo usalama. Sisi Bado sana ndo mana mtu akivaa suti tunamwita usalama au akipiga picha na kiongozi. Bado bidhaa zote zinazouzwa kariakoo ni fake na zinatoka nje na Bado Kuna usalama. Usalama wakuwakamata wakina Madeleka.Mwabukusi,Slaa kuvamia club na kukamata watu wenye min sket kuwa ni machangu siku akija michell Obama Kwa anavyo vaa watamkamata kuwa anajiuza.
 
Mi naona mitandao ina tija kuliko hao mnaowaita usalama. Ona kwenye uuzwaji wa Bandari iliwaona hao mnaowaamini kuwa ni usalama,mbona mambo yameisha na qamasai nayo yataisha sikubhizi ukiwa chawa unaitwa usalama.
 
Back
Top Bottom